Ni Siri Kuu - The Great Mystery

Ni Siri Kuu - The Great Mystery
"Wakati ule Yesu akajibu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga. Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyopendeza mbele zako.

Jumamosi, 4 Novemba 2017

TAREHE 4, JUMA MOSI YA NI SIRI KUU


TAREHE 4; JUMA MOSI YA NI SIRI KUU

“Wakati ule Yesu akajibu, akasema Nakushukuru, Baba, BWAna wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga, naam Baba kwa kuwa ndivyo ilivyopendeza mbele zako. (Math 11:25)

Kama leo tungekuwa mashariki ya kati na tukiwa kama Wayahudi, leo haingetupasa kufanya kazi yoyote ile Zaidi ya kushinda hekaluni tukimwabudu BWANA na kujifunza kuishi na kushika Amri zake.

Lakini leo mambo ni tofauti kabisa, ni wachache tu miongoni mwetu ambao leo ilionekana kuwapasa kushinda hekaluni/kanisani kumwabudu BWANA na kujifunza kushika amri zake.

Haikanushiki kuwa, ndivyo walivyoagizwa wayahudi, kufanya hivyo siku zote za maisha yao, kadhalika ndivyo walivyoagizwa wanadamu wote tangu uumbaji.

Lakini swali la kujiuliza, ni kwa nini haiko hivyo hivi leo kwa wengi wetu?
Kwa nini jamii tu ya wayahudi kadhaa ndio waliohusika na suala la kuabudu leo, tena kwingineko kote mbali na huko Israeli, ni ndugu waitwao wa Adventist/Wasabato ndio waliofanya hivyo

“kwa maana ameinena siku ya saba mahali Fulani hivi, Mungu alistarehe siku ya saba, akaziacha kazi zake zote; (Wae 4:4)”
Na hapa anaongeza “Basi imesalia raha ya sabato kwa watu wa Mungu. (Waeb 4:9)”

Haipingiki kwamba jumamosi ni siku ya saba kwa majira ya hapo Mashariki ya kati, ambayo ni siku maalumu ya kupumzika. Japo jambo hili, huonekana kama jambo la wayahudi, wasabato, ambao msingi wa kutenda kwao hivyo ni maagizo ya torati.

Lakini tuitazame siku Yenyewe. Juma mosi, ni siku ya kuabudu, tena ni siku ya kazi, lakini pia kwa wengine ni siku ya starehe mbali na pumuziko takatifu/sabato.  Juma mosi Kila mtu anaitumia anavyotaka na anavyoona inamfaa, na wala hakuna sheria yoyote ambayo inawataka watu wote kuitumia siku hiyo kwa matumizi maalumu kama ilivyotajwa kwenye torati.

Katika mazingira yetu, ofisi za selikali baadhi zinafunguliwa, japo ni nusu siku. Ofisi za taasisi binafsi zenyewe hufanya kazi kama kawaida, ukija upande wa wanafunzi, madarasa ya mitihani ya taifa huwa wanaenda, japo si siku rasimi inayohesabika kuwa ya masomo.
Je, siku hii inatendewa haki? Hasa kwa kuzingatia matumizi ambayo Mungu aliyakusudia yatumike. Kama mazingira yangekuwa yale ya bustanini, na kwa agizo lile la kupumuzika siku ya saba, basi ni hakika kuwa, leo wote tungeshinda kwenye nyumba za Ibada kumwabudu Mungu, au lakini tusingefanya kazi.

Mabadiliko mengi, kuanzia uasi, hata  wakati wa ujio wa Yesu, umeifanya siku hii, ipoteze umaarufu wake, na nafasi yake katika wanadamu.

Nani anahusika katika hili? wa kwanza Mwanamke, wa pili Mwanaume, kwa pamoja Adamu. Wa pili Yesu Kristo.  Najua kumtaja Yesu kama mhusika ni kama hatujaenda sawa, lakini anahusika sana, maana kama si ujio wake basi, wote walio wa Imani ya Mungu mwenyezi wangeabudu leo.
Lakini je!, tulioenda kuabudu leo ndio tulio na haki, na tena je sisi tusioenda kuabudu leo hatuna haki katika hili?

Karibu kwenye Tarehe 5, Jumapili ya Ni siri kuu,
Hapo ndipo siri ya siku hizi mbili itakapofunuliwa.

By Mwl. Goodluck Kazili (Ni Siri Kuu – The Great Mystry)

(October)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni


Kunihusu

Picha yangu
"Wakati ule Yesu akajibu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga. Naam, baba , kwa kuwa ndivyo ilivyopendeza mbele zako. (Ni Siri Kuu)

Tafuta katika Blogu Hii