SIKU
MUHIMU KATIKA MAISHA YAKO
ziko siku pengine nyingi zilizo za Muhimu sana kwa mwanadamu katika
kuwepo kwake hapa Duniani. Siku muhimu ya kwanza ni siku uliyozaliwa, na siku
ya pili ambayo ni kubwa kuliko zote tangu kuzaliwa ni siku hii/hiyo uliyo
okoka, na siku ya tatu muhimu ni siku utakapopumzika katika Kristo Yesu.
PONGGEZI KUU KWAKO
Hakika, unastahili pongezi kuu kwa uamzi ulioufikia sasa, uamzi wa
kumwamini na kumkiri Yesu kuwa BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAKO, ni uamuzi wa
maana na hatua kubwa kuliko hatua yoyote katika maisha. Hii ni kwa sababu pia
watu wengi hawapati neema ambayo wewe umeipata, hivyo Huduma ya (Ni Siri Kuu, kupitia Mwl. Goodluck Kazili)
na waamini wote pamoja na walioko mbinguni tunakupongeza kwa uamuzi wako.
Ni wazi umuhimu wake unaweza usionekane haraka, lakini thamani yake ni kubwa
kuliko mambo yote kwako hapa Duniani.
THAMANI ULIYOIPATA
Uko ufalme wa nuru (MUNGU), tena uko ufalme wa giza, hivyo wewe siyo
tena wa ufalme wa giza bali ni wa ufalme wa nuru yaani wa MUNGU mwenyewe
aliyeumba mbingu na nchi katika Kristo Yesu Pamoja na Roho
Mtakatifu. Thamani kubwa kwanza uliyoipata ni ile ya kuondolewa kaitka ufalme
wa giza shetani na kuingizwa katika
ufalme wa Mungu. Na apa
inathibitishwa hivi
“Naye alituokoa kutoka katika nguvu za giza akatuhamisha na kutuingiza
katika ufalme wa Mwana wa pendo lake, ambaye katika Yeye tuna ukombozi, yaani
msamaha wa dhambi (Wakolosa 3:13-14)”
Thamani hii imetokana na upendo wa Yesu, ambaye aliitoa Damu yake
kusudi kwa hiyo uweze kutakaswa, hapa anasema, “Yeye atupendaye na kutuosha
dhambi zetu kwa damu yake. (Ufunuo 1:5b)”
Hata hivyo jua kuwa ulipokuwa haujaokoka/ haujazaliwa mara ya pili kwa
roho haukuwa na thamani katika ufalme wa Mungu, na usingeweza kuuona wala
kuuingia kwa hakika, maana Yesu mwenyewe anasema Lakini wewe sasa kwa njia ya
Roho, umezaliwa mara ya pili, hivyo umepata sifa ya kuuona na kuuingia ufalme wa
Mungu. Sasa wewe ni wa thamani sana mbinguni na Duniani.
UMUHIMU WA KUOKOKA/WOKOVU
Kuokoka au kupata wokovu si suala la dini, wala suala la kanisa
fulani, wala haki ya dhehebu fulani, bali ni mpango mahususi tena kamili wa
Mungu kumuokoa na kumkomboa mwanadamu kwa njia ya imani, maana hapa maandiko
husema “kwa sababu ukimkiri Yesu Kristo kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na
kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu
alimfufua katika wafu, UTAOKOKA. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata
haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu. (Warumi 10:9-10)” na si
jambo jema hata kidogo kufikiri kuwa wokovu ni wa watu wa dhehebu fulani. Bali
ni baraka tena ni haki tena ni faradhi kufikiri na kujua kwa hakika kuwa wokovu
ni mpango wa Mungu wa kumuokoa kila mwanadamu. Ni vibaya sana dhehebu
kujimilikisha wokovu, na ni vibaya sana dhehebu kuukataa wokovu na kuona kuwa
ni kitu cha watu fulani.
Ni kweli na hakika kuwa mtu asiyeokoka, hawezi kuuona
wala kuuingia ufalme wa mbinguni. Hapa Yesu anasema “amini amini nawaambieni mtu
asipozaliwa mara ya pili hawezi kuuona ufalme wa mbinguni. (Yohana 3:3). lakini
maneno haya kwa wengine yalionekana kuwa magumu, kwa kujiuliza inawezekanaje
mtu kurudi tumboni mwa mama yake na kuzaliwa tena mara ya pili? Katika fahamu
zetu kama wanadamu haiwezekani kabisa, lakini hapa Yesu anabainisha tena kwa
msisitizo zaidi kwa kusema ““amini, amini, nakuambia mtu asipozaliwa kwa
Maji na kwa Roho hawezi kuuingia ufalme wa Mungu (Yohana 3:5)” Katika
mafafanuzi ya usemi huu, anasema “kilichoza;
liwa na mwili ni mwili nakilichozaliwa kwa roho ni roho”, hapa alimaanisha
kuwa unapozaliwa mara ya kwanza unazaliwa katika tumbo la mama yako, hapo wewe
ni mwili kabisa, lakini mwili hautaurithi ufalme wa mungu. Hivyo kama umezaliwa
na mama yako ambaye ni mwili, basi hata wewe ni mwili, na kwa sababu hiyo
usipozaliwa katika roho huwezi uuona wala kuuingia ufalme wa Mungu. Kuzaliwa
katika roho ni kwa njia ya imani ya kumwamini Kristo Yesu, na kutiwa muhuri
yaani kubatizwa. Lakini hapo kinachohitajika tena ni ile kukiri hicho
unachokiamini, yaani huyo Kristo unayemwamini moyoni mwako kumkri, ambapo
kukirki huko kunakufanya uokoke, kunakufanya upate wokovu. awaye yeyote
asikudanganye wala kukuhubiri injili yoyote inayokanusha habari hizi, maana huo
ndio uzima wako, wala jambo liwalo lolote lisikutoe katika kuamini huko
kunakotajwa maana thamani yake
ni zaidi ya chochote. Hapa Yesu ananena “kwani atafaidiwa nini mtu akiupata
ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya
nafsi yake? (Mathayo 16:26)”. Hakuna uwezacho kutoa na kuwa fidia ya
nafsi yako, bali wokovu pekee ndio jibu na uzima wa nafsi.
WOKOVU NI MCHAKATO
Suala la wokovu huanza siku moja,
lakini halikamiliki ndani ya siku moja hiyo hiyo, maana ni mchakato ambao
unamhitaji mtu mwenyewe kuhusika kikamilifu kwa msaada wa huyo Roho Mtakatifu.
Ndiyo maana kati ya vitu muhimu ambavyo mtu anavihitaji mara anapo okoka, ni
kumpokea Roho Mtakatifu.
Kuokoka na kutokuwa na roho
mtakatifu ni sawa na kumvua samaki wa kufuga kisha ukamwacha bila maji, lazima
tu atakufa, ndivyo alivyo mtu anayeokoka na kuendelea kuishi bila ujazo wa Roho
Mtakatifu. Ama ni kama mtu anunuaye gali na kuiendesha bila kuwa na oili, gali
hiyo lazima itanoki injini na itakufa kabisa.
Ndugu uliyeokoka, unahitaji Roho
Mtakatifu sasa, ili uingie katika hatua nyingine ambayo sasa utaanza kumjua
Mungu. Maana ni kweli kuwa hatupati uzima wa milele ile tu kuokoka, bali
kuokoka ni hatua ya msingi wa kutupeleka kwenye hatua za kumjua Mungu ambao ndio uzima wa milele. “kama
vile ulivyompa mamlaka juu ya wote wenye mwili, kusudi wote uliompa awape uzima
wa milele. Na uzima wa milele ndio huu, wakujue wewe Mungu wa pekee, wa kweli
na Yesu kristo uliyemtuma. (Yohana 17:2-3)”. Wokovu unafikia hatua ya
utimilifu mara unapofika kiwango cha kumjua Mungu katika kweli. Hatua hii
huwezi kuiingia bila kuwa na Roho Mtakatifu
Maa na
hakuna ajuaye mambo ya Mungu ila Roho Wa Mungu. “Maana ni nani katika binadamu
ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ua binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo
mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu. (1Wokorintho 2:11)”
Hivyo hakuna awezaye kumjua Mungu
asipojulishwa na Yesu kwa njia ya Roho Mtakatifu. Na ndiyo sababu Yesu
aliwasisitiza sana wanafunzi, kuwa ni muhimu sana Yeye aondoke ili kusudi Roho
Mtakatifu naye aje ambae atawafundisha kumjua Baba yaani Mungu kwa huyo Roho
ambaye watampokea mara baada ya Yesu kuondoka. “lakini mimi nawaambia iliyo
kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana mimi nisipoondoka, huyo msaidizi
hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu. Naye akisha kuja
huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu. (Yohana
16:7-8)”
Hivyo maadamu umeokoka, kwa maana
ya kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yako, hapo umestahili kumpokea
Roho Mtakatifu. Ambaye Yesu anampeleka kwako makusudi tu akufunulie kumjua
Mungu. “Akasema, nimekabidhiwa vyote na baba yangu; wala hakuna amjuaye Mwana,
ila baba; wala hakuna amjuaye Baba ila Mwana, na yeyote ambaye Mwana apenda
kumfunulia. (Mathayo 11:27)”
Kwa ufafanuzi huo, wokovu huanza
na Imani moyoni, kisha kukiri kile ulichokiamini. Huo tunaita kuokoka, lakini
mara baada ya kuokoka, sasa unapaswa kumpokea/kujazwa Roho Mtakatifu, ili
akufikishe mahali unapotakiwa kufika yaani kumjua Mungu.
Si wewe tu ambaye umeokoka na
inawezekana ukawa huna Roho Mtakatifu, bali wako wengine. Tena kwenye maandiko
wanatajwa watu ambao walikuwa wameokoka lakini hawajui hata kama kuna kitu
kinaitwa Roho Mtakatifu maana hata kusikia tu hawakuwahi kusikia.
“Paulo akiisha kupita kati ya
nchi za juu, akafika Efeso; akakutana na wanafunzi kadha wa kadha huko;
akawauliza, je! Mlimpokea Roho Mtakatifu mlipoamini? Wakamjibu, la, hata
kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu hatukusikia. (Mdo 19:1-2)”
Lakini haikuwa haki kwao kuokoka na kuishi bila kuwa na Roho
Mtakatifu. Hapo sasa ndipo walipoamini upya kwa kubatizwa kisha wakampokea Roho
Mtakatifu wote kwa idadi yao. “Na Paulo alipokwisha kuweka mikono yake juu
yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao; wakaanza kunena kwa lugha, na kutabiri. Na
jumla yao walipata wanaume kumi na wawili. (Mdo 19:6-7)”
Mwl. Goodluck Kazili
(NI SIRI KUU/THE GREAT MYSTERY)
Hakiuzwi/ kimeamuliwa na Mungu kama Sadaka
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni