Ni Siri Kuu - The Great Mystery

Ni Siri Kuu - The Great Mystery
"Wakati ule Yesu akajibu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga. Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyopendeza mbele zako.

Ijumaa, 2 Mei 2014

UTATU MTAKATIFU NA KUSUDI KWA MTU (MUNGU BABA, MUNGU MWANA, MUNGU ROHO MTAKATIFU)



UTATU MTAKATIFU NA KUSUDI KWA MTU
(MUNGU BABA, MUNGU MWANA, MUNGU ROHO MTAKATIFU)

DONDOO:
UTANGULIZI
SEHEMU YA KWANZA
Ø  NAFASI YA MUNGU BABA KATIKA DUNIA/MWANADAMU/MTU
Ø  NAFASI YA MUNGU MWANA KATIKA DUNIA/MWANADAMU/MTU
Ø  NAFASI YA ROHO MTAKATIFU KATIKA DUNIA/MWANADAMU/MTU
SEHEMU YA PILI
NYAKATIA TATU MHIMU
Ø  KUUMBWA ULIMWENGU
Ø  BAADA YA UUMBAJI AGANO JIPYA
Ø  UJIO WA KRISTO: AGANO JIPYA
SEHEMU YA TATU
UGAWAJI WA MADALAKA
Ø  KUTOKA KWA MUNGU HADI KWA YESU KRISTO
Ø  KUTOKA KWA YESU KRISTO HADI KWA ROHO MTAKATIFU
SEHEMU YA NNE
MAMLAKA NA UHUSIANO BAADA YA UGAWAJI MADALAKA
Ø  MAMLAKA YA MUNGU NA UHUSIANO WAKE NA MWANADAMU
Ø  MAMLAKA YA YESU NA UHUSIANO WAKE NA MWANADAUMU
Ø  MAMLKA YA ROHO MTAKATIFU NA UHUSIANO WAKE NA MWANADAMU
SEHEMU YA TANO
UMHIMU NA ULAZIMA WA KUJUA NA KUFUATA UTARATIBU HUU
Ø  KUSUDI LA MUNGU KWA MWANADAMU
Ø  UTILIMILIVU WA KUSUDI
Ø  HITIMISHO

SEHEMU YA NNE
MAMLAKA NA UHUSIANO BAADA YA UGAWAJI MADALAKA
Ni mhimu kufahamu kuwa utendaji kazi wa Mungu umebadilika sana kulingana na vipindi ambavyo vimepita. Hali hiyo inapelekea mfumo pia wa mwanadamu kutakiwa kubadilika katika uhusiano wake na Mungu. Kitu kilichowakwamisha wayahudi hadi leo wengi wao wasimwamini Kreisto ni kutokujua mabadiliko ya utendaji kazi wa Mungu na uhusiano wake na wanadamu. Japo maandiko yalikuwa yametangulia kueleza wazi kuwa kutakuwa na mabadiliko: Yeremia 31:3
Hakika Mungu ni mmoja lakini mwenye nafsi tatu za utendaji kazi, kusema mwenye nafsi tatu ni mhimu kuelewa kazi ya nafsi ni kupambanua na kufanya maamuzi. Hivyo kwa ufupi na tafsiri ya karibu tunaweza kusema kuwa Mungu anapambanua na kufanya maamuzi katika maeneo matatu au kwa namana tatu. Hivyo kwetu wanadamu husema yuko Mungu Baba, Mungu mwanaNeno, na Mugnu Roho Mtakatifu: kwa maana wako watatu washuhudia[mbinfuni, Baba, na Neno, na Roho Mtakatifu, na watatu hawa ni umoja. Kisha wako watatu washuhudiao duniani], Roho, na maji, na damu na watatu hawa hupatana kwa habari moja, (1Yohana 5:8-9a)
Hata hivyo ni mhimu kujua kuwa, utenfaji kazi huo, ambao umebadilika katika vipindi maalumu ambavyo vina maana kubwa kwetu.
Ukisoma kwenye maandiko matakatifu utakutana na wakati ambao Mungu alikasilishwa na akaamua kumupa mamlaka malaika ya kuwaongoza wana wa Israel; kutoka 32: 34: basi sasa uende ukawaongaze watu hawa mpaka mahali paloe ambapo nimekwambia habari zake; tazama Malaika wangu atakutangulia; pamoja na hayo siku nitakayowajilia nitawapatiliza kawa ajili ya dhambi yao.

Hata hivyo tuna wakati wa kujiuliza kwa nini Mungu hakuwapa Mwana  ndiye awaongoze; hakika yake ni kuwa muda wa Mungu kujifunua kupia Mwana ilikuwa bado, pia ni wazi kuwa nafasi ya taifa moja hakukuwa na ulazima wa kujifunua kupitia mwana wakati ulimwengu mzima ulikuwa na shida, hivyo kwao malaika alitosha, hata hivyo ukiendelea kusoma unaona kuwa Musa alikataa kwenda na malaika.
Na jambo hili ndilo ambalo limefanyika kwa wayahudi japo si kwa kukataa kwenda na Yesu ila kwa kutokujua kuwa utendaji kazi katika dunia hauko tena chini ya nafsi ya Mungu Baba bali Mungu mwana.
Ilipofika kipindi Fulani cha wakati kama unabii ulivyokuwa umeonyesha Mungu alihamisha mamlaka yake ya kuisimamia dunia na kuweka chini ya Nafsi yake iliyo mwana yaani nafsi ya pili ya utendaji kazi ambayo ni Mwana;  
Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa Tumepewa motto mwanamume na uweza wa kifalme utakuwa bagani mwake; naye ataitwa jina lake, Msahuri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani (Isaya 9:6). Pia kaitka Mathayo  1:21Naye atazaa mwana , nawe utamwita jina lake Yesu, maana ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao, Hayo yamekuwa ili litimie neon lililonenwa na Bwna kwa ujumbe wa nabii akisema, Tazama bikra atachukua mimba naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi.  


Ugawaji wa mamlaka hii ulikuwa na maana kubwa sana, hasa kwa ajili ya ukombozi wa mwanadamu, kwa maana ya kuwa Mungu aliamua aitoe nafsi yake ambayo ni mwana ili aifanye kuwa upatanisho kwa dhambi kati ya wanadamu na Mungu. Hii humaanisha kuwa Mungu hatamtazama mwanadamu tena moja kwa moja isipokuwa ataitazama nafsi yake/mwana kisha ndani yake atamuona mwanadamu. Na kwa kuwa katika nafsi hiyo ilitolewa damu ambayo huwasafisha dhambi zao, hivyo Mungu hataiona dhambi kwa kuwa watakuwa wametakaswa.
Haikutosha tu kuzaliwa kwa Yesu na kuwapa msingi wa namana ya kuishi maisha mpya yaani ya Kikristo, bali walitakiwa wakae nae ili kupata msaada zaidi wa kuendelea kuufahamisha ulimwengu hiyo namna mpya na ukombaozi ulioletwa na Mungu kwa wanadamu kupitia nafsi Yake. Na kwa kuwa kazi ya nafsi ya pili yaani mwana ilikuwa kutoa damu na maji kwa ajili ya ukombozi na utakaso wa dhambi, kazi ya kuendelea kushuhudia ukombozi hou haikuwa ndani ya nafsi mwana balili ilikuwa ndani ya uwezo wa nafsi Roho Mtakatifu; hivyo baada ya nafsi Mwana kumaliza kazi yake ilikuwa ni lazima nafsi nyingine ije kwa ajili ya ukamilisho.
Hapa huwa kuna changamoto kubwa kwa kuwa watu wengi wanaishia kwenye nafsi ya pili yaani mwana; wakijua kuwa baada ya kuokoka, kubatizwa na kutakaswa kwa damu ya Yesu hudhani kuwa mambo tayari, na wakati mwingine hufikri wanaweza kuyaishi hayo maisha ya utakatifu walioupata kupitia kwa mwana. Kumbe ni lazima kumalizia na hatu nyingine mhimu sana ya nafsi ya tatu yaani Roho Mtakatifu kwa kuwa huyo nidye kila kitu baada ya mtu kuokoka, kubatizwa na kutakaswa.
Maandiko yameweka wazi mambo haya japo watu hawayazingatii, na ndio maana wanakwama sana katika huduma zao, imani yao, na hata katika kutunza wokovu hou walioupata.
Ukisoma habari za Yesu ni baada tu ya kubatizwa alichukuliwa na Roho kwenda kujaribiwa nyikani. Kwa hali ya kawaida kulikuwa na haja gani ya Yesu kuchukuliwa na Roho Mtakatifu; (Math 4:1). Baada ya Yesu  kukaribia kuyondoka kwenda mbinguni aliwaambia wanafunzi/ mitume; Lakini mtapokea nguvu, akisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu;nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria na hata mwisho wa nchi, (matendo 1:8)
Hawa hawakuwa na sifa ya kuwa mashahidi wa Yesu kabla Roho mtakatifu hajawajilia, ni mhimu kujiuliza vema maana hawa wanafunzi walikuwa wamekaa na Yesu mda wa miaka mitatu na nusu akiwafundisha tena wakitembea naye na wakihubiri  na kufanya ishara na maajabu mengi, lakini bado kuondoka kwa Yesu walikuwa hawana sifa za kuwa mashahidi wake hadi Roho mtakatifu atakapowajilia. Ukijiuliza unagundua kuwa  kazi hiyo haikuwa ya Yesu/Mwana bali ilikuwa imewekwa ndani ya Roho Mtakatifu. 
Kwa uelewa zaidi kuna wakati wanafunzi wa Yesu hawakuwa wanapendezwa na taarifa za kuwa Yesu ataondoka, kisha Yesu akawaambia; Lakini mimi nawaambia iliyokweli; yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana mimi nisipoondoka, huyo msaidizi hatakuja kwenu, bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu,(Yohana 16:8). Hapa unaona kuwa kumbew Roho Mtakatifu yupo, lakini hajapewa hiyo kazi, na Yesu anasema nitampeleka kwenu halafu ukiendelea kusoma zinatajwa kazi atakazozifanya ambazo amepewa mamlaka haimaanishi ndizo kazi anazoziweza tu ila kwa duniani amekuja kufanya hizo; Naye akisha kuja huyo natauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na  hukumu, (Yh 16:9).

 Ukipendezwa na somo hili na unahitaji mwenelezo wake tuma email gkazili@yahoo.com au tuma ujumbe no ya simu 0752165609 au 0716050663.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni


Kunihusu

Picha yangu
"Wakati ule Yesu akajibu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga. Naam, baba , kwa kuwa ndivyo ilivyopendeza mbele zako. (Ni Siri Kuu)

Tafuta katika Blogu Hii