Ni Siri Kuu - The Great Mystery

Ni Siri Kuu - The Great Mystery
"Wakati ule Yesu akajibu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga. Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyopendeza mbele zako.

Jumatatu, 29 Februari 2016

THAMANI YA MTU WA NDANI (NAFSI)

SK-Siri Kuu
 

THAMANI YA MTU WA NDANI (NAFSI)

Na Mwl; Goodluck Kazili

"Wakati ule Yesu akajibu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga. Naam, baba , kwa kuwa ndivyo ilivyopendeza mbele zako. (Ni Siri Kuu)

Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?. (Mathayo 16:26)
Hakuna kitu chenye thamani katika ulimwengu huu, kama nafsi ya mtu. Nafsi yako ndicho kitu chenye thamani kuliko chochote unachokijua katika ulimwengu huu, ndiyo sababu Yesu aliuliza au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?. Je! ulimwengu mzima thamani yake inalingana na thamani ya nafsi yako? hapana haiwezi kufikia. Na hivyo hakuna chenye thamani kuliko nafsi yako.

Hata hivyo ajabu ni kwamba, mtu mwenyewe haithamani hiyo nafsi yake bali anathamini vitu ambavyo nafsi ilipewa ili kuvitumia. mfano mtu hataki kuokoka kwa madai kuwa atashindwa kuifaidi dunia na raha yake. Mtu kama huyu, tatzo lake ni ufahamu tu wa kutokujua thamani ya kila kimoja na matumizi yake na sababu ya kuwekwa hivyo vitu.

Hata hivyo, ni muhimu kujua kuwa kuna utu wa ndani na utu wa nje. tena utu wa nje uliumbwa kwa ajili ya utu wa ndani, kama tu nyenzo ambayo mtu wa ndani anapewa ili atumie kwa matumizi yake.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni


Kunihusu

Picha yangu
"Wakati ule Yesu akajibu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga. Naam, baba , kwa kuwa ndivyo ilivyopendeza mbele zako. (Ni Siri Kuu)

Tafuta katika Blogu Hii