KONGAMANO
LA 8 LA MAOMBI YA TAIFA TANZANIA 2013
MADA: KUOMBA
TOBA NA UPATANISHO KWA AJIRI YA SELIKARI ILI KUPATA
KIBARI NA KUWA NA UHUSIANO
WA KUDUMU MBELE ZA MUNGU
Daniel 9:1-27
MUHIMU KUHUSU MADA ILIYOTANGULIA:
Mada ilikuwa: "KUJENGA NAFASI HALISI
YA KANISA KATIKA NCHI"
Katika mada hii, tuliangalia na
kuomba juu ya lango la kanisa kuwa imara katika nchi. Tuliomba toba juu ya
kuhusuriwa Kwa lango hilo, tukaomba kuimarishwa kwa lango hilo, tukaomba
kutumiwa vema na Mungu ili kufanya mapenzi yake, tukaomba juu ya kuchukua
wajibu wake wa kuiongoza selikali katika njia bora ya kiMungu. Tulikuwa na
mfululizo wa makongamano 3 ya kuombea kanisa, ambapo tulianza terehe 10/4/2012
na kukamilisha 15/12/2012.
Wakati huu tumepewa “kuomba
toba na upatanisho kwa ajiri ya selikari ili kupata kibari na kuwa na uhusiano
wa kudumu mbele za mungu”. eneo hili tutajifunza yale ambayo Mungu anataka
tuyajue juu ya nafasi Yake katika selikali, pamoja na nafasi ya selikali mbele
za Mungu, na wajibu wa kanisa katika selikali.
DONDOO
Nafasi ya
selikari mbele za Mungu
Nafasi ya Mungu katika selikari
Wajibu wa
kanisa katika selikali mbele za Mungu
UTANGULIZI:
Ni jambo la mhimu sana katika
nchi, kuwa na mtazamo chanya juu ya misingi ya nchi na uwepo wake katika dunia
inayoonekana na ile isiyoonekana yaani ulimwengu wa roho. Imani yangu ni kuwa
unajua “kushindana kwetu sisi si juu ya damu na
nyama, bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya
majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho, Waefeso 6:13”. Misingi ya nchi yoyote hujengwa katika
ulimwengu wa roho kwanza kabla ya kujengwa upande wa mwili. Ni wazi kuwa, kwa
kuwa kuna falme, mamlaka na jeshi la pepo wabaya katika maeneo haya haya ya
dunia, swali la kujiuliza ni hili, je huo ufalme, mamlaka na jeshi la pepo
linafanya kazi juu ya nani au jeshi hilo linamrinda nani na lipo kwa ajili ya
kupigana na nani?
Ni hakika kuwa ulimwengu huu ni
mwendelezo wa ulimwengu wa roho, ambapo mfumo na namna unavyoongozwa inafanana
kwa sehemu kubwa na ile ya ulimwengu wa roho, ndio maana huwa kuna kuathiliana
kati ya watu wa dunia yaani wa mwili na wale wa roho. Hata hivyo tunajua kuwa
yako madaraja kadhaa yanayoikamilisha dunia kwa upande wa watu. Kwa mfano kuna
mtu, familia, ukoo,kijiji,kata, tarafa,wilaya, mkoa, kanda, taifa, bara,dunia.
Madaraja haya huadhili au kuathiliwa kuanzia mtu hadi dunia. Athali haiwezi
kutokea ambayo chanzo chake itakuwa nchi, bali kwa mtu au familia/kundi dogo
linaweza kuvuluga hali ya nchi, pia mtu au familia/kundi dogo linaweza kuiweka
nchi katika hali njema, hata maandiko yanathibitisha “ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu,
watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya;
nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao, 2
Nyakati 7:14”.
Karibu Usome na Kujifunza, Roho Mtakatifu yuko tayari kukusadia vema; Amina
UFAHAMU JUU YA NCHI/TAIFA LA TANZANIA
Hadi sasa Tanzania ina miaka 51,
lakini Tanganyika ina kadiliwa kuwa na miaka 10,000 tangu watu waanze kuishi,
kwa ushahidi wa kiakilojia. Hatuwezi kutazama hali ya nchi kwa kuitazama miaka
hiyo 51, bali tunatakiwa kutazama tangu kuwepo kwa aridhi ya Tanzania, na pale
watu walipoanza kuishi.
Japo ni vigumu sana kupata histori,
lakini kujua ukweli kwa namna ya roho inawezekana kwa kuwa kisichokuwepo ni
ushahidi wa kimwili, ila ushahidi wa mambo ya roho upo, “kwa maana twajua torati asili yake ni ya
rohoni-Warumi 7:14a”.
Wakati Mungu anaiumba dunia,
Tanganyika iliyozaa Tanzania aliiumba, na kusudi lile lile tunalolisoma kwenye Maandiko la Mungu kuiumba dunia ndilo kusudi la Mungu kuiweka Tanganyika-Tanzania,
(tunatumia Tanganyika kwa kuwa ndiyo asili, kwa kuwa Tanzania imepatikana
kisiasa, yaani baada ya kuungana na Zanzibar). Na kwa kuwa kila jambo
analolifanya Mungu huwa na maana kubwa, basi uwepo wa Tanganyika una maana sana
kwetu tuliowatanganyika na wazanzibari,
kwanza mbele yetu wenyewe, mataifa mengine na mbele za Mungu mwenyewe
aliyetuweka.
Nchi yetu iliumbwa kwa ajiri ya
Mungu, nasi tukawekwa ili kutawala, nchi hii ni mali ya Mungu, kwa kuwa dunia
na vyote viijazavyo ni mali ya Mungu. Hata hivyo sisi tunaoishi humu, tumepewa
kazi moja kuu, kuitawala nchi na kila kilicho ndani na juu ya nchi kwa maana ya
kilicho aridhini na kilichoko juu ya aridhi “Mwanzo 1:26-31”.
Hivyo ni mhimu kukumbuka kuwa
kusudi la Mungu juu ya Tanzania halijakuwepo kuanzia mwaka 1961-64, bali
lilikuwepo tangu ilipowekwa misingi ya dunia. Na kwa kuwa kusudi la Mungu
ilikuwa kuwa na utawala mwingine wa namna ya mwili huku duniani, na ikampendeza
kuiweka Tanganyika, basi ni mhimu kulitazama kusudi hilo ili kuijua Tanzania na
mstakabali wake katika misingi ya roho na mwili.
Tanganyika iliumbwa kama nchi na
wala siyo taifa, kwa kuwa hakuna mahali palipoumbwa kama taifa, na tukishataja
suala la nchi basi tunagusa lasiri mali, kwa kuwa nchi ni aridhi. Na kusudi la
Mungu haliko kwa watu wa Tanzania, bali kwa nchi ya Tanzania, kwa kuwa angeweza
kuzaliwa yeyote Tanzania, na kama kusudi lingekuwa kwa watu, basi
tusingetawaliwa na kuongozwa kwa muda wa miaka zaidi ya 85,(wakati wa ukoloni)
ambao ni umri unaoizidi Tanzania, lakini bado mambo yaliyofanyika yana maana
kubwa katika kukamilisha kusudi la Mungu juu ya nchi.
Nchi hukamilika inapokaliwa na
watu, na hapo ndipo kusudi la Mungu hukamilika. Kwa kuwa ukamilisho wa kusudi
la Mungu ni pale nchi inapokawaliwa na watu, na kutawala kwa misingi ya Mungu.
Tanzania ina eneo lenye ukubwa wa kilomita za muraba laki
tisa elfu arobaini na tano na mia mbili na tatu (945,203), ni nchi ya 31 kwa
ukubwa wa eneo, katika eneo hilo aridhi ni asilimia 93.8 katika 100, na eneo la
maji ni asilimia 6.2 ya jumla ya eneo lote. Idadi ya watu kwa mujibu wa sense
zilizowahi kufanyika sense ya kwanza mwaka wa 1967= milioni 12 laki 3 elfu 13
mia 469,( 12,313,469) sense ya pili mwaka wa 1978= milioni 17 laki 5 elfu 12
mia 610,(17,512,610) sense ya tatu mwaka wa 1988= milioni 23 elfu 95 mia 885
(23,095,885) sense ya nne mwaka wa 2002= milioni 34 laki 4 elfu 43 mia 603
(34,443,603).
Sense ya tano ya 2012 inakadiliwa
kuwa na watu milioni 45,798,475, kadilio la miaka ijayo, kufikia mwaka 2020 inakadiliwa kuwa 57, 102,896. Kwa idadi hiyo inaonesha kuwa
nchi ya 30 kwa idadi ya watu. Kwa kila eneo la kilomita mbili linakaliwa na
watu 46, msongamano huu, unaiweka kuwa nchi ya 124 kwa msongamano wa watu, ndio
nchi kubwa zaidi Afrika ya Mashariki.
Tanzani inajulikana kama nchi
masikini sana Duniani, katika viwango vya kimataifa, japo katika uhalisia
Tanzania si nchi masikini, bali ni Taifa masikini. Kwa maana utajiri ulio
kwenye aridhi ya Tanzania ni zaidi ya utajiri ulio kwenye mataifa
yanayohesabika kuwa nchi tajiri.
Kabla ya ukoloni hatukuwa na
taifa la Tanzania, wala Tanganyika, isipokuwa kulikuwa na koo, pamoja na
makabila mbalimbali yaliyokuwa na utawala wao, hivyo hatukuwa na jamii moja
ya Tanganyika wala Tanzania kwa kuwa haikuwepo
mipaka halisi ya nchi kiutawala. Mnamo mwaka wa 1884, katika nchi ya ujerumani
iliyoko uraya, ulifanyika mkutano wa kuigawa afrikana ili kuiweka chini ya
utawala (ukoloni). Wakati huo ndipo mipaka ilipochorwa na Tanganyika ikawa
taifa na nchi yenye mipaka halisi, iliyotambuliwa na umoja wa mataifa baadae.
Wakati huo ndio ulikuwa mwanzo wa kuja kwa habari za Kristo, kwa njia ya
umisheni, ulikuwa unafanywa na wazungu. Hata hivyo, jamb la kuleta habari njema kama maandiko
yalivyokuwa yametangulia kusema, bado ilionekana kuwa ni tatizo kwa kuwa
ilihusisha masuala ya utawala wa kinyonyaji yaani ukoloni.
NAFASI YA SELIKARI MBELE ZA MUNGU
Selikari kwa maana ya utawala, ni
chombo kilichowekwa/kinachowekwa na Mungu kwa kusudi la kusimamia/kuhudumia
watu wake katika mambo yote ya mwili. Selikali siyo mtu bali ni
mamlaka(authority) ambayo ipo kwa ajiri ya kutekeleza mambo makuu matatu. Kujenga uchumi imara kwa watu wake, kuwa na siasa safi, na kutoa huduma zote za kijamii
KUJENGA UCHUMI IMARA:
Uchumi wa nchi na watu wake anayehusika kuujenga ni selikali, hili ni
jambo moja mhimu linalotambulisha utendaji wa selikali (mamlaka). Japo kuna
vitu ambavyo huisaidia selikali kujenga uchumi imara kwa watu, hata hivyo vitu
vyote ni wajibu wa selikali kuwa navyo, isipokuwa tu maliasili ambazo ziko nje
ya uwezo wa mwanadamu. Uchumi wa nchi uko kwenye nchi, ikimaanisha kuwa uchumi
wan chi uko kwenye aridhi. Lakini hatuwezi kutaja uchumi bila watu.
Maana ya uchumi, ni kuzalisha na kutumia
lasilimari zilizoko ili kukidhi mahitaji yaliyopo, lasilimari hizo ni kama zile
za asili na zisizo za asili, lakini hata hivyo zisizo za asili hutokana na zile
za asili.
UFAHAMU
WA KIROHO JUU YA UCHUMI
Hapo mwanzo hapakuwepo na uchumi,
kama tuuonavyo leo, lakini mara ya kwanza kabisa Mungu alimwagiza Adamu kuilima
aridhi na kuitunza, huo ulikuwa mwanzo wa uchumi katika kitabu cha “Mwanzo
1:28-31”. Pia watoto wa Adamu, Kaini na Habiri, walikuwa wakifanya kazi
zilizotambulisha nafasi yao na uchumi wao.
Dhambi inaonekana kuwa tatizo la
uchumi, kama vile lilivyo tatizo la uzima wa milele “Mwanzo 3:17” dhambi
iliathili aridhi, na hauwezi kuwa na uchumi bila kuwa na aridhi ukiwa kama
taifa au nchi. Wakati Mungu alipoilaani aridhi, kwa sababu ya dhambi ilikuwa na
tafsiri ya kuulaani uchumi, kwa kuwa maisha ya mtu kwenye mwili yalitegemea
sana ardhi “Akamwambia Adamu, kwa kuwa umeisikiliza
sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema usiyale;
ardhi imelaaniwa kwa ajiri yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za
maisha yako, michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni; kwa
jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia aridhi, ambayo katika
hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi
wewe nawe mavumbini utarudi.
Laana hii vipengele vyake vyote vinagusa uchumi tu, kwa kuwa kipengele cha
kifo hakikuwa laana bali yalikuwa matokeo ya kuvunja sheria, na aliambiwa
mapema kuwa akila hayo matunda hakika atakufa.
Dhambi iliharibu suala la uchumi,
kuwepo kwa dhambi kulifanya suala la uchimi kuwa tatizo, kwa maana ya kuwa
ilifanya mtu ahangaike ili kuwa na uchumi mzuri, hali njema ya uchumi
tunayoiona kwa baadhi ya watu, na kwa baadhi ya nchi/mataifa, ni kidogo sana
ukilinganisha na ilivyokuwa imekusudiwa, kabla ya dhambi kuvuruga.
Lakini hata hivyo, kwa maana
halisi ya uchumi tuijuayo leo, inaonesha kuwa uchumi uliletwa na dhambi, maana
ya sasa ya uchumi “ ni kutumia malighafi zisizotosheleza ili kukidhi mahitaji
ya mwanadamu” hivyo kama kuna utoshelevu basi suala la uchumi tusingekuwa nalo,
lakini kwa sababu ya upungufu uliopo, tunalazimika kuwa na wazo la kusuruhisha
tatizo na kuzalisha na kutumia lasilimali kidogo zilizopo ili kutimiza mahitaji
yaliyoko, Na tunajua kuwa bila dhambi huo upungufu usingekuwepo.
Adamu ni mzaliwa wa kwanza, nje
ya nafasi ya Yesu, na kwa kuwa yeye ni lango la wanadamu wote na mataifa yote,
hivyo wote huhesabiwa kuwa wametenda dhambi ileile aliyoitenda Adamu. Jambo
hili ni kwa sababu ya, kila mtu hupita kwenye lango lilelile la Adamu, hivyo
kinachosababisha tuhesabiwe kuwa tumetenda dhambi si kutenda dhambi kwenyewe
bali mahali tunapopita na kutokea
tunapokuja duniani ndipo panapofanya tuhesabiwe dhambi.
Baraka kuu ya hapa duniani ni
uchumi imara, wala siyo wokovu, kwa kuwa wokovu haupo kama Baraka, bali ni
neema ambayo ipo kwa kila mtu. Lakini suala la uchumi si neema ambayo imewekwa
kwa kila mtu, bali ni maarifa, ujuzi na ufahamu wa namna ya kuujenga ili uwe
imara, ndicho kigezo kikuu. Ukisoma maandiko, kuanzia kitabu cha mwanzo, habari
za Ibrahimu hadi kufika kwenye agano jipya, mafundisho na Baraka zilizoamriwa
nyingi ni za uchumi, hata hivyo agano la kale lote lemetaja Baraka kuu mbili,
nayo ni ya uchumi na afya tu. Agano jipya limetaja wokovu pekee kwa wingi sana
na msisitizo uko kwanye wokovu uletao
uzima.
Mfano Mungu alimuahidi ibrahimu
kumrithisha kizazi chake nchi ya kanani, ambayo imejaa maziwa na asali, lakini
ni ukweli kuwa nchi ya kanaani haina hivyo vitu kwa kiwango tunachosoma kwenye
maandiko, hii ni kwa sababu kilichokuwa kinaelezwa ilikuwa zaidi ya maziwa haya
tuyajuayo kwa jinsi ya mwili. Kwa kuwa lugha ya roho huweza kutumia kitu
kiletacho taswira tu kwenye ulimwengu wa mwili, kwa mfano Mungu alipozungumza
suala la maziwa, ni hakika kuwa alitaja vitu vyote vijulikanavyo kuwa bora na
hasa vyakula, pia ilipotajwa asali ilimaanisha vitu vyote vilivyo vitamu kwa
aina yake kuwa vitakuwa vimejaa katika nchi ya Kanaani.
Hata hivyo kuna uhalisia wa sasa
katika vitu hivyo vilivyotajwa katika nchi ya Kanaani ambayo sasa ni Israel.
Kwa maelezo haya bado inaonesha kuwa jambo kubwa lilikuwa la uchumi, hata
kilichosababisha wao kwenda Misri ilikuwa haja ya uchumi na hata
kilichowakwamisha kutokutoka Misri ni uchumi uliokuwa umeunganisha na miungu ya
misri.
Ukisoma maandiko kwenye agano la kale hakuna mahali
ambapo uzima wa milele umetajwa, kama
tuujuavyo leo, hata kwa wale waliopata kuelewa, walichojua kuwa wakisha kufa
watalala pamoja na ndugu zao, wala hapakuwa na ufahamu juu ya siku ya mwisho,
hadi kufikia wakati wa nabii Amosi karibu mwaka 750 K.k.
Amri 10 za Mungu na sheri zaidi
ya 420 walizopewa wana wa Israel, karibu zote zilikuwa zinagusa hali ya uchumi
wao. Hii ina maana kuwa zilikuwa za kujenga uhusiano mwema na Mungu ambapo
matokeo yake ilikuwa kupata uchumi mzuri pamoja na afya, tofauti na sasa ambapo
matokeo makubwa ni uzima wa milele.
Ukiangalia vema, utagundua kuwa,
walipovuja sheria hizo, hali yao ya uchumi na afya ilileta shida, kwa maana ya
kuwa uhusiano wao na Mungu ulipokuwa mubaya, basi matokeo yalikuwa kwenye
uchumi na afya zao. Na hapa utagundua kuwa , suala la dhambi haliachani na
uchimi pamoja na afya ya mtu. Baraka za afya na uchumi zimetajwa kwenye
“Kumbukumbu la torati 28:1….”
Uchumi wa mtu, una misingi yake
katika roho au una mlango wake ambao
hujulikana kama agano, hutofautiana na ngazi ya Taifa japo taifa na uchumi wake
huanzia kwa mtu, mwisho huwa kuna uchumi wa mataifa. Ni mhimu kuelewa mgawanyo
huu wa makundi matatu yanayopokea uchumi kutokana na mfumo wa ulimwengu wa roho.
Kwenye ulimwengu wa roho, uchumi
hukaa ndani ya mtu, ila kuna muda unaoamriwa juu ya mtu huyo na uchumi ulio juu
au ndani yake. Hata hivyo majira yapo kwa kila mtu kulingana na uhusiano wake
ulivyo katiaka ulimwengu wa roho. Mfano, ndoto ya Farao“Mwanzo 41:1….” Haikuwa
inagusa uchumi wa misri pekee bali hata ule wa kanaani. Lakini kilichofanyika
ni kuwa Farao alikuwa na uchumi ndani
yake, lakini Baraka yake ilikuwa Kanaani ambyo ilikuwa ndani ya Yusufu. Yusufu
alikuwa na maarifa juu yauchumi, pia alikuwa na Baraka ya uchumi, ndio maana
alipoingia kwa Potifa, maandiko yanasema Mungu alimfanikisha Potifa mambo yake
kwa mkono wa Yusufu. Lakini Yusufu mwenyewe hakuwa na uchumi, ila akifika
mahali penye uchumi basi Baraka yake ilikuwa inauchanua ule uchumi.
Jambo hili ni mhimu sana kwa kuwa
wako watumishi wengi ambao wana Baraka za uchumi, lakin wao hawana uchumi, si
ajabu mtu kumuombea awe na uchumi imara, na akafanikiwa kwa maombi na namna
alizopewa na mtumishi huyo, lakini unaweza kumkuta mtumishi huyo ana hali
mbaya. Kwa hili kinachofanyika Mungu anamuunganisha na watu wenye uchumi, ili
Yeye aachilie Baraka yake na atakapofanikiwa basi haitakuwa kwa ajiri ya huyo
mtu peke yake bali pia itakuwa kwa ajiri ya huyo mtumishi.
Mali zilizopatikana baada ya Yusufu
kuingia misri zilikuwa kwa ajiri ya misri na watu wa nyumbani mwa Yusufu. Hata
katika habari ya watumishi waliowekwa na Mungu kuwahudumia watu katika Israeli,
Mungu aliweka utaratibu huu, Kiongozi alipewa Baraka, ambazo akiziachilia
kwako, unafanikiwa katika mambo yako, ambapo sasa itakubidi kuchukua sehemu ya
mafanikio yako na umpe huyo kiongozi/mtumishi, na huo ndio ujira wa Mungu
katika Baraka anazozitoa.
Mfano mwingine, nabii Eliya
wakati wa njaa, alimtaka Yule mwanamke amtengenezee mikate, lakini Yule mama
alitaka kulalamika kwa kuwa alikuwa ameishiwa, Eliya akamshrutisha amalizie
unga huo uliobaki, baada ya mama Yule kufanya Kama alivyoagizwa, matokeo yake
ilikuwa kupata chakula tele,Kwa kuwa chombo kile kilijazwa mara dufu. Hapa
tunaomna kuwa Eliya alikuwa Na Baraka, Ni mhimu kujua mahali ambapo au mtu
ambaye ana Baraka zako, Kama marekani walivyogundua kuwa Baraka yao iko
Israeli, wakafanya kuwafadhili na kuwatunza kwa uwezo wao wote na sasa ndio
nchi pekee yenye uchumi imara duniani.
Uchumi wa Taifa
Uchumi huu wa taifa huwa na msingi
wa mtu/familia, uchumi huu una misingi ya kwenye aridhi na kisha humalizikia
kwa watu. Mfano Israeli walikuwa wakitembea Na Baraka za uchumi, hivyo nchi ya
kanaani haikuwa na Baraka hiyo wasipokmuwepo wana wa Israel, ndio maana hata
kama mtu ataitumia ile aridhi, haitatoa mazao, lakini ikitumiwa na mtu wa uzao
wa Israel hutoa mazao sana.
Uchumi wa dunia
Ni uchumi ambao chanzo chake
huanzia kwenye mtu/familia kasha huja taifa ndipo tunapopata uchumi wa dunia,
uchumi huu hutegemea Baraka zilizoko kwenye mataifa. Mfano halisi ni Baraka
aliyopewa Ibrahimu juu ya mataifa, “Mwanzo 22:18”, alifanya agano na Mungu
lililokuwa linagusa maisha ya uzao wake na mataifa. Wakati ibrahimu alipewa
haki ya kuwa Baraka kwa uzao wake na mataifa, Daudi alipewa ufalme Isaya 11:1,
wakati Yakobo alipewa haki ya taifa, ndio maana hadi leo tuna taifa la Israel
ambalo ni jina lake.
Kwa maelezo haya yanaonesha wazi
kuwa Israel kama taifa na nchi ina dhamana kubwa katika uchumi, utawala na
taifa katika dunia.
Tangu hapo mwanzo Mungu
alipoilani aridhi, hakukuwa kana namana ya kusitawi uchumi mpaka kwa Baraka
maalumu, na jambo hili lilianza kwa Ibrahimu, na Mungu aliunganisha hali ya
mafanikio ya watu na mataifa kwa Ibrahimu, “Na katika
uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia; kwa sababu umeitii sauti yangu
Mwanzo 23:18”. Na katika
ukweli huu, unagundua kuwa hakuna taifa lisilomkiri Ibrahimu ua Yesu kwa
aganola Ibrahimu lenye uchumi imara. Hata hivyo yako mengine yawezayo kutokea
ili kukamulisha maandiko yanayotaja siku za mwisho, ambapo wale wasio wa Kristo
watapata nguvu za Kiuchumi, na kuitawala dunia. Mafano mataifa yanayoanza
kupata nguvu nje ya kumkubali Kiristo ni moja ya alama ya kutimiza ufunuo huu.
Wakati Yesu alipokuja duniani,
kulifanyika mabadiliko ya aina tata
Uchumi, ufalme ambapo ndani yake
tunapata wokovu, na taifa. Na katika kuutazama ukweli huu utagundua kuwa kabla
ya Yesu kuzaliwa mataifa/falme zilizokuwa zinatawala dunia hakuna inayojulikana
kwa sasa, kwa kuwa yalitokea mabadiliko makubwa sana kwenye maeneo hayo matatu
mhimu katika dunia. Mfano, falme kama z aroma, uyunani na uajemi, babeli,
zilizokuja kufuatiwa na Iraq hazina nguvu hata kidogo. Ujio wa Yesu ulifunga
mlango wa ustawi ambapo ilikuwa tangu kwa Adamu, Wakati huo Yesu alichukua hiyo
nafasi akafanyika kuwa mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote wa walio hai na walio
kufa.
Utagundua kuwa nchi karibu zote
zina mafanikio yatokanayo na misingi ya Kiroho, mfano nji ya malekani ina
mafanikio makubwa kwa sababu ya Israel, hata
ulaya pia ina mafanikio kwa sababu ya kumabariki ibrahimu, na wakati
wanapopunguzi zile Baraka hata uchumi wao unayumba, na marekani kwa kuwa anajua
hili, ndiye aliyebaki na msimamo juu ya Israeli na ikiwa atalegeza msimamo wake
basi huu ndio utakuwa mwisho wa kustawi kwake, amtaifa yaliyobaki nai yale
yanayoembea kwa Baraka za ishimael kwa kuwa naye alipewa Baraka hizo japo
hazikuwa kubwa kama za Isaka. Mfano mataifa ya uarabuni yote yanauchumi
unaoelekeana na Baraka za Ishimaeli, na ndio maana hawawezi kuwa sawa na
mataifa mengine yasiyo kuwa na Baraka hizo wala walio chini ya Isaka “mwanzo 21:8….”
Hivyo ugonvi wa mataifa
yanayopokea Baraka kupitia kwa ibrahimu, nay ale ya Ishimaeli hayako kwenye
uchumi ila yako kwenye ufalme. Kwa kuwa tofauti za imani, hazina uhusiano na
uchumi ila ni mambo ya kifalme au utawala, hivyo unagundua kuwa lango la
Ibrahimu kwa upande wa uchumi ni kubwa,na ndio msisitizo mkubwa ulio kwenye
agano, msisitizo wa agano jipya upo kwenye ufalme- uzima wa milele.
Hapa unakumbuka kuwa matazamo wa
watu waliookoka na kushika tu agano jipya, huzingatia na msisitizo wao uko
kwenye habari za ufale-uzima wa milele, sualala uchimi hawahangaiki nalo, lakini Mungu aliviweka vyote kwa maana nzuri
sana, kwa kuwa wokovu ni kwa ajiri ya roho, uchumi ni kwa ajiri ya mwili. Na
kwa kuwa hapo mwanzo kwenye agano la kale msisitzo war oho haukuwepo sana zaidi
ulikuwa wa mwili, ndio maana Baraka zote ambazo zimetajwa kwenye maandiko
zinahusu uchumi na afya tu, wakati wa agano jipya msismitizo ulikuwa kwenye roho, mwili
umeonekana kuwa adui, ndio maana ukisoma barua za Paulo, amezunguzia sana kuwa
mwlil ni Adui Warumi sura ya 6 hadi ya
8. Pia kwenye Mathayo 6:31 “bali utafuteni kwanza ufalme wake(mbinguni) nahaki
yake; na hayo yte mtazidishiwa”
Wapo waonao kuwa ni bora kuwa na
uchimi kwanza kasha wokovu ndipo ufuate, wakiamini kuwa usipokuwa na uchumi bsi
hata suala la wokovu litakusumbua. Na wengine wanaona bora kuwa na wokovu
kwanza kwa kuwa huo uchumi hata ukiukosa bado una tumaini la uzima wa milele.
Lakini tukiyatazama hayo maneno ya Yesu, yanatupa uhakika kuwa ndani ya ufalme
kua uchimi pia , kwa kuwa aliposema na mengine mtazidishiwa alimaanisha na uchumi. Lakini p[ia katika mfano alioutoa wa
lazalo, unaonesha kluwa unaweza kuwa na uzima bado uchumi usiwe nao wakati
uwapo duniani, pia unaweza kuwa na
uchumi lakini uzima usiwe nao.
Hata hivyo suala la wokovu na
uchimi kwa nchi zinazoendelea, bado ni changamoto kubwa, kwa kuwa hata sehemu
kubwa ya mahubiri na mafundisho yao yanahusu uchumi, na muujiza wao mkubwa ni
wa uchumi na afya. Hata hivyo ukweli wa mambo ni kuwa wengi wao maarifa ya
uchumi hawana lakin suala la uzima na afya kwa ujumla lina kipaumbele sana.
Mafano kama utasikia tangazo la mkutano wa injili kwa hakika vittajwa vitu
viwili, yaani wokovu na uponyaji wa magonjwa, hii ni kwa sababu mafanikio
katika uchumi ni kidogo sana hata katika sala zao, angalau kuna mafanikio
katika maombi ya magonjwa japo hata hivyo wengi wao wamekuwa wakihusianisha na
nguvu za giza. Lakini hapo yako matabaka mawili, kuna wale waishio mjini na
hasa angalau wenye mafanikio ya kiuchumi, ambao ni daraja la wafanyabiashara,
wasomi, wafanya kazi, hawa wao hupendelea mahubiri na mafundisho yanayohusu
habari za uchumi, mfanokatika wanafunzi wengi wao hupenda mafundisho na
mahubiri yanayowapa msaada wa namana ya kufanikiwa katika masomo na uchumi kwa
ujumla, habari za wokovu na maarifa ya roho kwao ni changamoto.
Kwa ngazi ya taifa, ni kweli kuwa
kila taifa linakipaumbele chake katika masuala ya roho, vivyo hivyo kila
mtumishi anakipaumbele chake. Na ukivichunguza utagundua kuwa vipo vinavyolalia
upande wa agano la kale, na vingine viko upande wa agano jipya,
Mfano
Afrika kuna vipaumbele kama
wokovu na uchumi, msisitizo wa kenye wokovu uko kwenye uzima wa milele pamoja
na afya ya mwili, pia kupata mafaniko ya kiuchumi.
Amerika na ulaya kuna vipaumbele
kama kuabudu, hii ni kwa sababu wao hawana shida sana ya kiuchumi wala kiafya,
hivyo kwa upande wa Mungu ni watu wenye kupenda kuabudu kuliko kuomba na kutaka
msaada wa Mungu. Kusema hivi haimaanishi kuwa wao hawaombi, isipokuwa mkazo wao
hauko kwenye mambo ya uchumi na afya.
Mashariki ya kati hasa Israel,
kuna vipaumbele viwili, ufalme na ibada, huko ndiko kuna mambo ya kifalme
pamoja na moyo wa ibada.
Uarabuni na asia, kuna vipaumbale
vya wokovu na kuabudu.
Vipaumbele hivi vyote vina chanzo
na sababu zake, mfano kwa upande wa Amerika na ulaya si mahali ambapo mtu anaweza
kuwahubiria habari za kuwa na uchumi na afya kwa kuwa wamejaliwa katika hayo.
Sawa na upande wa Israeli, habari za utawala kwake ni mhimu sana kuliko vyote
kwa kuwa, wao ndio saa ya dunia, hivyo kila mabadiliko yanayotokea kwao
yanaigusa dunia.
Kutokana na maelezo yote hayo
juu ya uchumi ni wazi kuwa suala la uchumi lina misingi yake zaidi ya vile
linavyotazamwa kwa baadhi yetu. Kwa kuwa hakuna mahali popote ambapo uchumi
umehusianisha na shetani, bli uchumi huhusianishwa na dhambi. Hivyo katiuka kuomba
juu ya uchumi ni mhimu kujua misingi iliyojengwa kabla imesimamia kwenye nini,
sulemani aliomba hekima akapewa na utajiri. Kama hakuna hekima basi ni ngumu
sana kuwa na utajiri. Kwa kuwa mataifa mengi yalipofanikiwa kiuchumi walimsahau
Mungu kabisa, uchumi uliwalewesha wakaona kuwa ndio kila kitu.
Hivyo katika kuombea nchi yetu,
ni mhimu tushugulike na dhambi pamoja na hekima ya utawala, hapo tunaweza
kufanikiwa katika kunusuru hali ya nchi yetu kwa upande wa uchumi.
Katika suala la utawala, ni jambo
mhimu sana katika selikali, nchi isipokuwa na viongozi wazuri ni hakika kuwa
haiwezi kuendelea, kwa kuwa suala la maendeleo linagusa uongozi pamoja na mfumo
ulioko. Kwa hali hii, tukitaka amani iwepo katika nchi, ni lazima tushugulike
na uongozi pamoja na lango lake ambalo huwa kwenye mawazo na imani.
Suala la uongozi lina uhusiano
mkubwa na suala la familia na marafiki, kwa kuwa kuna uongozi wa wito, na ule
wa kujiita au kuitwa na marafiki, dini, au familia. Hata hivyo ni mhimu kujua
kuwa suala la uongozi si Baraka bali ni mfumo na mtu aliyewekwa kuwa kiongozi.
Kwa mfano kiongozi wa kwanza wa
Israeli katika habari ya wafalme alikuwa Sauli, katika utawala wake, kitu
kinachoitwa utii hakuwa nacho, na mtu asiye na utii, ina maana hana hekima ya
kutosha, na kama hana hekima ya kutosha, basi huyo lazima atakosea. Na kosa la
kiongozi wan nchi ni pigo kwa nchi.
Nafasi ya uongozi ni mhimu sana
katiaka nchi, kuliko kiongozi mwenyewe, kwa kuwa kiongozi ni mtu tu, lakini ile
nafasi anayopewa inamfanya awe zaidi ya mtu. Hivyo jambo kuwa si kiongozi bali
ni ile nafasi ya kiongozi na kitu ambacho imebeba. Hata hivyo ni mhimu kujua
kuwa kiongozi hafanyi yaliyo yake, bali hufanya ya Yule aliyempa nafasi ya
kukaa kwenye hiyo nafasi. Hakuna mtu awezaye kutimiza kiu na haja ya mioyo ya
watanzania wanaokaribia milioni 47 kwa akili na hekima yake, bila msaada wa
roho. Pia ni jambo bay asana kama hakuna maaono yoyote, tunaweza kulaumu mfumo
uliopo kila siku lakini kama hakuna maono ya Mungu juu ya nchi basi, hakuna
jambo tuwezalo kulifanya. Hivyo kwetu waombaji ni mhimu kuwa na maono ya juu ya
nchi, kasha tusimamie hayo.
Hivyo katika yote yako mambo
makuu matatu, moja ni maono, mbili ni nafasi yenyewe ya utawala kwa lugha
nyingine tunaweza kusema kiti chenyewe, na tatu ni mtu mwenyewe yaani kiongozi
mwenyewe.
Mfano mzuri unaogusa kiongozi
mwenyewe na nafasi yake kwa watu wake ni huu wa mfalme Daudi
“Ndipo moyo wake Daudi ukamchoma baada ya kuwahesabu hao watu.
Naye Daudi akamwambia BWANA, nimekosa sana kwa haya niliyoyafanya; lakini sasa
Ee BWANA, nakusihi uondoilee mbali uovu wa mtumishi wako; kwani nimefanya
upumbavu kabisa. Na Daudi alipoondoka asubuhi, neon la BWANA likamjia nbii
Gadi, mwonaji wake Daudi, kusema, Nenda, nenda ukanene na Daudi, BWANA asema
hivi, nakuwekea mambo matatu; katika haya uchague moja, nikutendee hilo. Basi
Gadi akamwendea Daudi, akamweleza, akamwambia, basi, miaka ya njaa ikujilie
katika nchi yako? Au miezi mitatu ukimbie mbele ya adui zako, huku
wakikufuatia? Au siku tatu iwe tauni katika nchi yako? Fanya shauli sasa,
ufikiri ni jawabu gani nimrudishie aliyenituma. Naye Daudi akamwambia Gadi,
nimeingia katika mashaka sana; basi sasa natuanguke katika mkono wa BWANA; kwa
kuwa rehema zake ni nyingi; wala nisianguke katika mkono ya wanadamu . basi BWANA akawaletea
tauni tangu asubuhi hata wakati ulioamriwa; nao wakafa watu kutoka Dani mpaka
beer-sheba sabini elfu Samweli 24:10-16”
ni hakika kuwa ukisoma maneno haya,
unaweza usitamani nchi yetu kuwa kwenye nafasi hiyo mbele za Mungu, ukitazama
yanayofanya na baadhi ya viongozi. Kwa kuwa kama kosa la kiongozi linaweza
kusababisha uchungu wa msiba kiasi hicho, ina maana kwa uongozi wetu basi wat
wangeisha. Ni bora kuwa hivi kuliko kuwa na nafasi kubwa mbele za Mungu, bila
kushugulikia nafasi ya kiongozi na kiongozi mwenyewe.
WAJIBU WA SELIKALI KATIKA MAMBO YA KIJAMII MBELE ZA MUNGU
Huduma zote za jamii kama vile, hospitali, umeme, maji,
shule, soko, n.k ni wajibu wa selikali, lakini hata hivyo mambo haya
yameunganishwa na uchumi, kwa kuwa uchumi usipokuwa mzuri basi huduma hizi
hazitatolewa vyema.Hivyo mambo makuu mawili yanalifanya hili liwe sawa.
WAJIBU WA KANISA JUU YA SELIKALI
UHUSIANO
WA LANGO HILI LA KANISA NA NCHI PAMOJA NA TAIFA:
Kama ilivyoelezwa mwanzo kuwa lango la kanisa kuhusianishwa
na nchi na taifa ni kuwa: mpango wa kwanza kabisa wa Mungu ilikuwa nchi na
taifa vitawaliwe kwa sheria za mbinguni au za ulimwengu wa roho. Na wakati
mwanadamu alipokuwa kwenye bustani ya
edeni namna iliyokuwa inamuongoza ilikuwa namna ya roho. Lakini ulipotokea uasi
ulipindua ile namna ya roho iliyokuwa imewekwa kumuongoza mwanadamu na
kuchukuliwa na namna ya mwili. Lengo la Mungu kuweka namna ya roho ni kwa kuwa
vitu vya roho viko imara na ni vya uhakika, na kwa kuwa Mungu ni roho basi
ilikuwa ni lazima mwanadamu aongozwe na namna ya roho na Mungu alikuwa
amemfunika na namna ya roho inayotosha kuongoza dunia.
Kwa kuwa dhambi
ilitokea na kuvuruga mfumo huo, mwanadamu alikuwa anaishi kwa kuongozwa na namna
ya dunia na wara siyo ya Mungu, isipokuwa kwa wachache waliopata neema ya
kumuelekea Mungu aliwapa namna hiyo ya roho. Mfano Henoko.
Ilipofika wakati wa Ibrahimu Mungu alipoingia Agano na
Ibrahimu baada ya kuona kuwa Ibrahimu atamuelekea Mungu. Baada ya miaka mia nne
Mungu alianza kutekeleza Agano lake. Alimtumia Musa kutekeleza mambo ya agano
lake na Ibrahimu, lakini wakati huo bado hata wana wa Israeli walikuwa
wanatawaliwa na namna ilele ya mwili. Na kwa kuwa ili uishi na Mungu ni razima
uongozwe na taratibu za Mungu ambazo ni za urimwengu wa roho, Mungu alimchukua
Musa na kumueleza utaratibu mpya wa maisha yao wanayotakiwa kuishi na wara si
kama zamani. Walipewa amri kumi na sheria ndogondogo zilizoikamilisha utaratibu
wanaotakiwa kuishi, ikumbukwe sheria hizi zilikuwa zimetoka kwenye ulimwangu wa
roho wa Mungu Baba Mwenyezi, kwa kuwa hakuna sheri itokayo kwa Mungu isiyo ya
ulimwengu wa roho( Warumi 7:14).
Hapo Mungu alitaka kuwatengenezea maisha aliyokuwa
ameyakusudia tangu mwanzo kwenye bustani ya Edeni kabla ya uasi. Baadae wakati
wa nabii samweli Wana wa Isreli
walikataa kuwa chini ya utawara wa Mungu badara yake wawe na mfalme
atakayewaongoza, ambaye watakuwa wanamuona na kuenda naye vitani kama
ilivyokuwa kwa mataifa mengine.
Mungu aliwakubalia na akafanya ule Mlango aliokuwa
anautumia katika kuwaongoza akauweka juu ya namna hiyo ya utawara waliyoitaka
ya kuwa na mfalme mwanadamu. Mlango huo ulikuwa kanisa, na uliwekwa kuwa
kiongozi wa selikari ya mwili waliyoitaka, hivyo japo kuwa alikuwepo kiongozi
wa mambo ya mwili, lakini bado Mungu aliweka kiongozi katika lango lile la
kanisa kuwaongoza watu na mfalme wao (1 Cor 6:4).
Na ni ukweli kuwa hukuna mfalme aliyewekwa katika Israeli na asipewe kiongozi
yaani nabii wa kumuongoza, hata kama angekuwa imara kiasi gani lakini bado
kwenye lango la kanisa kuna kiongozi aliyewekwa kuwaongoza wote. Hata wakati wa
Daudi japo alionekana kuwa imara sana mbele za Mungu, lakini hiyo ilikuwa
nafasi ya kifalme , kwenye nafasi ya kanisa manabii walikuwepo kama Mwongozo,(2Samweli
24:10-19)
Maelezo hayo
yanaonesha kuwa kusimama kwa nchi na taifa kunategemea pia namna kanisa
lilivyosimama.
Kanisa ni mwangalizi na kiongozi wa selikali na watu wake,
na tunaposema selikali na watu wake inamaanisha kuwa kanisa linaiongoza selikali kufanya sawasawa
na mapenzi ya Mungu ili Mungu asiadhibu nchi hiyo na taifa hilo.
Pia kanisa ndiyo kiongozi wa viogozi wa selikali, mwenye
wajibu wa kuwafanya watimize mapenzi ya Mungu katika nchi na taifa kwenye lango
hilo la uongozi katika mwili.(1 Cor 11:16).
Nabii Danieli aliyekuwa amewekwa kusimama kwenye lango la
kanisa alipoona mambo hayako sawa aliingilia kati na kuomba maombi mazito ya
kuepusha hasira ya Bwana isiipate nchi na taifa lake, (Danieli 9:3-19), pia
Ezekieli alipewa kazi ya kufanya ili kufuta uovu wa nchi na taifa lake kwa kuwa
yeye alikuwa kwenye lango la kanisa (Ezekieli 4:4-9).
Roho Mtakatifu akujaze zaidi ya ulichosoma na kujifunza
kwa msaada zaidi niandikie kwenye email: gkazili@yahoo.com, au tuma ujumbe no 0765-129960
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni