Ni Siri Kuu - The Great Mystery

Ni Siri Kuu - The Great Mystery
"Wakati ule Yesu akajibu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga. Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyopendeza mbele zako.

Jumatano, 10 Februari 2016

FUNGUO ZA UTAWALA (KEY OF DOMAIN)

Na Mwl; Goodluck Kazili

"Wakati ule Yesu akajibu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga. Naam, baba , kwa kuwa ndivyo ilivyopendeza mbele zako. (Ni Siri Kuu)

1. MAARIFA (Knowledge)
2. NGUVU ZA KIROHO (Spritual power)

Maarifa humuwezesha mtu kutawala, nguvu za roho humuwezesha mtu kutiisha

wakati Mungu anamuumba mtu, alikusudia mtu huyo aitawale nchi na vyote lakini pia na kuvitiisha (Mwanzo 1:26). huwezi kutawal bila kuwa na maarifa, kadhalika huwezi kutiishi kama huna ngvu

wakati wote anayetawala ni yule mwenye maarifa zaidi. Mungu alimpa mtu uwezo wa ziada kimaarifa zaidi ya viumbe wote, na kwa hayo maarifa anawatawala. Mwanadamu angepewa uwezo wa kimaarifa sawa na wanyama wengine basi asingeweza kuwatawala bali kingetumika kigezo cha pili cha kutiisha na hapo kwa vile mwanadamu asivyokuwa na nguvu basi simba, tembo, na wanyama wengine ndio wangetawala.

hivyo utawawala wowote ule unategemea maarifa na nguvu. Mtu asiyekuzidi maarifa hawezi kukutawala, labda kwa kigezo cha pili yaana nguvu. mfano kiongozi, huwaongoza au huwatawala watu kwa kutumia maarifa na nguvu ya sheria. hata kama utakuwa unamzidi maarifa bado anaweza akakutawala kwa kutumia nguvu ambayo inaweza ikawa ile halisi au ya kisheria.

unataka kutawala ni lazima uwe na maarifa zaidi na ngvu pia. lakini kwa vile tunavyopaswa kuenenda kwa roho hauhitaji nguvu za mwili bali za roho, maana ile kuwa na maarifa hukupa pia nguvu za mwili. maana maarifa ni sawa na nguvu (knowledge is equevalent to power) 

itaendelea....

SK-Siri Kuu by
Goodluck Kazili

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni


Kunihusu

Picha yangu
"Wakati ule Yesu akajibu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga. Naam, baba , kwa kuwa ndivyo ilivyopendeza mbele zako. (Ni Siri Kuu)

Tafuta katika Blogu Hii