Katika ulimwengu wa sasa, siku ya
jumapili, ndiyo inayojulikana sana kuwa siku ya mapumuziko, hata katika nchi
yetu siku hiyo kiselikali na katika taasisi karibu zote ni siku ya mapumuziko.
Siku hii imewalazimisha hata wale ambao kwao isingewafaa kupumuzika, kupumuzika,
kwa kuwa iko kisheria kuwa siku ya mapumuziko.
Siku hii huitwa siku ya kuabudu,
tena huitwa siku ya mapumuziko, tena huitwa siku ya mwisho wa wiki, japo wengine
huiita mwanzo wa wiki.
Waadventist/wasabato, wanaona
kitendo hiki cha kuifanya siku ya jumapili kuwa siku ya mapumuziko siyo sawa,
tena siyo sawa kabisa kuifanya siku ya kuabudu. Hivyo ukienda maaeneo ambayo
wanapatikana wengi, kama ni kijijini, siku ya jumapili wakati hawa wakitembea
kwenda kanisani, wao utakutana nao wakiwa wameweka jembe begani wakielekea
shamba. Kama ambavyo, na hawa wengine jana juma mosi walibeba jembe kwenda
shamba.
Ukiangalia katika torati, suala
la kushika sabato ni moja ya Amri kuu. Ambapo mtu aliyeivunja hukumu yake
ilikuwa kifo. Mfano mwanamke mmoja
anatajwa katika maandiko aliyeokota kuni siku ya sabato, na kwa kuwa huyo
alikuwa wa kwanza kufanya kitendo hicho tangu amri zilipotoka, basi wengi
walingoja kuona nini atafanywa mtu yule. Lakini kama ilivyokuwa imeandikwa,
mwanamke yule aliuawa na hakuna aliyejaribu kufanya kazi tena siku ya sabato.
Mambo ni tofauti zama hizi, siku
hii ya jumapili, hata kwa hao wanaoiita sabato yao, yaani pumziko lao bado huwa
wanafanya kazi. Mbali na ile kwamba siku imebadilishwa kutoka juma mosi na kuwa
jumapili, lakini bado pia jumapili hii, haitendewi haki.
Kabla ya kuzungumuzia kuhusu
mabadiliko ya kuibadilisha sabato kutoka juma mosi na kuwa jumapili tuitazame
jumapili kama sabato japo tutazungumzia mabadiliko hayo kwa kina.
JUMAPILI
Jumapili siku ya
kupumuzika/sabato, je ni kweli Wewe huwa unapumuzika? Juma pili siku ya kuabudu
je wewe unakusanyika pamoja wenzako kuabudu?. Maana hata baada ya Israeli
kutoka Misri waliamuliwa kukusanyika sikua ya kwanza na ya saba. Na kusanyiko
hilo liliitwa Takatifu. “siku ya kwanza kutakuwa kwenu na kusanyiko
takatifu, na siku ya saba kutakuwa kusanyiko takatifu; haitafanywa kazi yoyote katika
siku hizo, isipokuwa kwa hiyo ambayo kila mtu hana budi kula, hiyo tu ifanyike
kwenu. (Kutoka 12:16)”
Maana ya sabato ni pumuziko, kama
kweli juma pili ni sabato kwa nini haupumuziki, mbona ndiyo siku ya kufanya
biashara, mbona ndiyo siku ya kufua, mbona ndiyo siku ya kusoma, mbona ndiyo
siku ambayo wengine hata kazini huenda. Usabato wa siku ya jumapili uko wapi?
Hilo ni swali lako, ujiulize.
Nina hakika kuwa, hakuna
anayefanya hivyo ambaye ana ushahidi unaomruhusu kufanya hivyo. Najua wengi tutatumia agano jipya kuweka
utetezi na hasa ile Yesu aliyomponya siku ya sabato. Ni kweli, kama wewe
daktari basi nenda kafanye huduma maana yafaa sana, Kama unatoa huduma ya
uokozi basi fanya hivyo maana yafaa sana na ni haki. Lakini kama unaenda
kufanya biashara, umegeuza kuwa siku ya kufua, umegeuza uwa siku ya kusoma na
hasa mitihani ikikaribia, tena umegeuza kama siku ya kumalizia kazi zako
zilizobaki, tena umeigeuza kama siku ya kusafiri, tena ofisi wanakulazimisha
kwenda kazini nawe umekubali, huitendei haki hata kidogo siku hii ya jumapili,
tena humtendee haki Yeye aliyeamuru mapumuziko na ibada kwa siku hiyo.
Sasa nitaeleza kitu hapa nawe
utajishauri. Mwaka 2009/, Mungu alisema nami, kuwaambia wanafunzi ambao
walikuwa wakienda kujisomea siku ya jumapili waache na badala yake wapumuzike
na kuitumia siku hiyo kumtafakari Mungu na kujisomea Neno la Mungu, Lakini
hawakusikia. Nakumbuka sana wakati huo, nilikuwa kiongozi wa maombi, wapendwa hawa
walikuwa na kawaida hii, Walikuwa wanaamuka asubuhi wanaenda kwenye ibada ya
kwanza, ikifika saa 3 asubuhi wanakuwa wametoka kwenye ibada tayari, kisha
wanachukua vitabu na kwenda shule kujisomea hadi jioni.
Tena walitengeneza mtandao wa kuombea
mitihani yao miezi 3 hivi kabla ya mtihani kufika, wanafunzi hao walikuwa
kitado cha sita. Niliposema nao kuhusu hilo, hawakunielewa, basi nikawaacha.
Walipoendelea na kazi hiyo ya kusoma, basi nikiwa njiani naelekea kanisani
kwenye kipindi nikifika karibu na uwanja wa ndege pale Dodoma, Sauti ikanijia
kusema, watu hawa hawajaniheshimu, kwa sababu hiyo, hawatafanikiwa kama
wanavyotazamia sitawafanikisha ijapokuwa wananiomba kwa bidii. Tulipkutana
kwenye kipindi, nilisema maana nilitajiwa na matokeo ambayo wangeyapata.
Nakumbuka sana wakati huo walikuwa wameshamaliza mtihani wa mock. Na walikuwa wamefaulu
sana, hivyo nilipowaambia matokeo watakayopata kwa sababu wameshindwa kufuata
maelekezo ya kuiheshimu siku ya jumapili/sabato kwa kupumuzika, lakini ni kama
walibeza na kuona kama mtu nichezae na jambo lisilowezekana.
Basi tuliendelea katika hali
hiyo, yuko mtu mmoja ambaye alitii na kuacha ambaye alikuja kuniambai kama
ushuhuda. Matokeo yalipotoka, wale wapendwa hawakuamini kilichotokea, na kwa
ushahidi yule mmoja aliyeacha akafaulu kwa daraja la kwanza na hakutegemewa
hata kidogo. Wakati huo waliofaulu vizuri walikuwa 2 miongoni mwetu tuliokuwa
katika kundi lile, japo mimi nikiwa kidato cha tano. Wako walioelewa kilichotekea na wengine
hawakuelewa mpaka leo. Mungu hakuwafanikisha vile alivyokusudia, japo baadhi
walifaulu kwa arama za kuwawezesha kuendelea na vyou lakini si kiwango kizuri
kilichokusudiwa na walichotazamia.
Jumapili ni siku ya mapumuziko,
mwanafunzi usisome, mfanya biashara usifanye biashara, mfanya kazi usifanye
kazi kama si kazi iliyoainishwa yaani hizo za huduma ya uokozi, mama na Dada
nyumbani usiitumie kufua nguo, usiitumie kumalizia kazi zako au kupunguza,
usiitumie kujipa kazi. Sote tusiitumie kusafiri. Siku ya jumapili itumie
kupumuzika kwa kumwabudu Mungu, kumtafakari, kujifunza Neno, kumsifu, kuwatia
moyo wengine, kuwafariji wengine, kuwahubiria wengine nakwa ujumla kuujenga
mwili wa kristo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni