Ni Siri Kuu - The Great Mystery

Ni Siri Kuu - The Great Mystery
"Wakati ule Yesu akajibu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga. Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyopendeza mbele zako.

Alhamisi, 28 Agosti 2014

WAJUA KUWA WE NI MFALME NA KUHANI!

kongamano la Maombi ya Shule na Masomo

Na Goodluck Kazili

UMENUNULIWA NA KUFANYWA KUWA UFALME NA KUHANI KWA MUNGU KATIKA NCHI
 
Si hadithi wala simulizi, bali ni kweli na hakika kuwa Kristo alichinjwa akawanunua watu wa kila kabila , lugha, jamaa, na taifa na akawafanya kuwa ufalme na makuhani wanamiliki juu ya nchi.
Si tu bahati kupata nafasi ya kusoma na kusikia habari hii, bali pia ni neema ya MUNGU kwako, hivyo nakusihi kwa upendo wake Yeye aliyetuumba uzitafakali habari hizi kwa kina nazo zitakufaa na kukusaidia kwa wakati wake.
Kwa msaada wa Roho Mtakatifu nalipenda nikushirikishe habari za nafasi yako kwa MUNGU, katika kanisa, katika nchi/taifa au jamii na familia yako. Si rahisi kujua nafasi yako, lakini imekupasa kuifikiria kwa kuwa hakuna atakayefikri kwa ajiri yako bali ni wewe mwenyewe.
Iko nafasi mhimu na kubwa mbele za MUNGU uliyo nayo, hivyohivyo ulivyo, japo nyumbani wanaweza wakawa wanakudharau na kukuona kuwa si lolote. Lakini mimi leo kama sauti ya MUNGU kwako jijue kuwa una nafasi kubwa na ya heshima mbele za MUNGU. Na nafasi hiyo ni ya mhimu sana kwako . haijalishi una maisha ya dhambi kiasi gani, lakini bado MUNGU ni m,wema kwako, maana maandiko yanasema “Tena zitokazo kwa Yesu Kristo shahidi aliye mwaminifu, mzaliwa wa kwanza wa waliokufa na mkuu wa wafalme wa dunia. "Yeye atupendaye na kutuosha dhambi zetu katika damu yake. Na kutufanya kuwa ufalme na makuhani wa MUNGU, naye ni Baba yake ; utukufu na ukuu una Yeye hata milele na milele amina”. (ufunuo 1:5-6)
Mpendwa katika Kiristo Yesu, nakusihi kwa neema hii; basi ujitahidi kumpenda MUNGU na kutafuta sana kumjua Yeye ili kwa msaada wake maisha yaweze kukamilika. Maana hakuna maana ya maisha pasipo MUNGU mwenye kuyafanya maisha. Na kwa kuwa sisi tuliompokea Kristo tulifanyika kuwa watoto wa MUNGU, basi imetupasa kuyatambua haya ya kuwa yapo kwa ajiri yetu.
Ni mhimu kukumbuka kuwa, jambo lililo jema huja kwa wakati wake, basi hakika hili ni jambo jema. Kwa kuwa kama ungelijua tangu hapo kuwa wewe ni kuhani juu ya nchi katika ufalme wa MUNGU, basi pengine ungekuwa na hatua kubwa. Hata hivyo nakukumbusha kuwa hakuna wakati utakao kuwa mwema kwako zaidi ya wakati huu.
Hivyo nakusihi ufikiri kama mtu mhimu, ambaye anategemewa sehemu nyingi na watu wengi.  Tena maneno haya usiyasahau, elimu ipo ili kukupa maarifa, na kwa kuwa kuna namna mbili, basi ni mhimu kuwa na maarifa ya pande zote, kwa kuwa unaishi pande zote. Ni hatari sana kutokuwa na maarifa juu ya nmna hizi mbili.
Kwa hakika yapo maarifa ya roho na yapo maarifa ya mwili. Maarifa haya yote ni mhimu sana kwako, japo maarifa ya roho yanaonekana kuwa na thamani kubwa. Yanaonekana ya thamani kwa kuwa si wengi wanaobahatika kuyapata, kwa sababu hawayatafuti. Sasa sikushauri wewe ujaribu kutoyatafuta, itakuwa hatari sana. Tafuta maairfa ya roho na haya ya mwili kwa kuwa yote yatakusaidia katika maisha yako yote ya sasa na ya badae, hata baada ya kufa.
Ningeweza kukuandikia mengi, lakini kwa ufupi huu, naomba utafakari sana jinsi unavyowaza na unavyoenenda, je namna hiyo itakusaidia kufika hapo alipokukusudia MUNGU? Ikiwa ni ndiyo MUNGU akutie nguvu katika juhudi hizo, na ikiwa siyo basi MUNGU  akusaidie ili ujitahidi kwa dhati kuubadili mwenendo na mawazo yako. Uyatambue haya kuwa yamekujia kwa wakati sahihi wa wewe kubadilika na kuanza kufikri sawasawa na makusudi ya MUNGU aliyekuumba. Usipoteze muda ni wakati wako maana “ Nao waimba wimbo mpya wakisema wastahili kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua mhuri zake,kwa kuwa ulichinjwa ukamnunulia MUNGU kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa, ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi” ufunuo 5:9-10
Haya ndiyo nalipenda nikushirikishe japo kwa ufupi, MUNGU akubariki .
Goodluck Kazili  0765-129960

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni


Kunihusu

Picha yangu
"Wakati ule Yesu akajibu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga. Naam, baba , kwa kuwa ndivyo ilivyopendeza mbele zako. (Ni Siri Kuu)

Tafuta katika Blogu Hii