Ni Siri Kuu - The Great Mystery

Ni Siri Kuu - The Great Mystery
"Wakati ule Yesu akajibu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga. Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyopendeza mbele zako.

Alhamisi, 7 Aprili 2016

UJUMBE MAALUMU KWAKO

Mwl; Goodluck Kazili

Tumia muda wako japo mfupi kusoma haya, na kuyatia katika fahamu zako, maana huendayakakufaa ikiwa Roho wa Mungu atakusaidia kuyafahumu vema.
 
Unafkiri vipi ukifanya kitu kwa lengo flani kisha kile kitu ulichokifanya wewe kikakataa au kushindwa kufanya vile utakavyo, hapo utajisikiaje? Na je! utafanya nini? Hivi unajua kwa nini dunia iliumbwa! Na kwa nini wewe uliumbwa! na aliyeiumba hii dunia alikusudia nini! na aliyekuumba wewe alikusudia nini!. Ukimuuliza mama yako na baba yako kama wako hai watakwambia kwa nini waliamua kukubali wewe uwepo kwenye dunia hii! Lakini ikiwa wao tu wasioweza kukufanya wewe, ila tu walitumiwa kukuleta, ikiwa ni kweli walikuwa na malengo na ujio wako, vipi aliyekufanya kabisa, aliyekupa uhai ndani yako, akili ya kufikri na kutambua, nafasi yake kwako ni ipi?. Ni sawa kuwa Yeye ni Mungu, lakini kuwa Mungu, na wewe kumtambua kuwa Mungu haifanyi kitu kikubwa, isipokuwa kikubwa ni yale malengo ya aliyekufanya yanapokuwa yametekelezwa.

Hayo unayoyafanya, kabisa ni moja ya malengo ya Mungu, kwamba uyafanye, mbali na yale yasiyokubalika ambayo unaweza kuwa unayafanya kimakosa. Hivyo mbali na hayo mabaya, hayo mema ambayo unayafanya na kuyapata, ni sehemu halisi ya malengo ya Mungu kukuweka kwamba upate kuyafanya. Lakini hayo yanakuridhisha na kukufurahisha wewe, je unafkri kitu gani ambacho kwa dhahili wewe ukikifanya chaweza kumpendeza huyo aliyibeba dhamana yako na aliyekuleta kwa malengo makuu kabisa, ambaye anahuzunika kila siku kwa sababu tu wakati mwingi humfanyii kila anachotamani kutoka kwako?. 
Ijapokuwa huchoki kumuomba na kuhitaji msaada kwake, lakini je! kwa kuwa wajibidisha katika kumuomba ndilo jambo linalompendeza, au je ni mzazi gani ambaye anaweza kumfurahia mtoto wake kwa kuwa anamuomba tu kila siku ikiwa mtoto huyo hafanyi mengine yanaupendeza moyo wa huyo mzazi?. 
Je wewe utafurahishwa na mtoto atakayekuomba na kukulilia kila siku umsaidie katika mahitaji yake tu? Au hata kama ungekuwa na rafiki ambaye Yeye ni kukuomba tu, wala hafanyi jambo lolote linaloupendeza moyo wako, hivi kweli utapendezwa na huyo mtu?  Ikiwa hautapendezwa ndivyo ambayo Yeye aliyekuumba hapendezwi na Wewe kumuomba tu usiku na mchana kwa ajili ya mahitaji yako, bali ingefaa sana kama ungeomba pamoja kufanya kile ambacho kinaupendeza moyo wake
 Mungu kabla hajakufanya wewe, alikufanyia kwanza mahitaji utakayoyatumia, wakati wote utakaokuwepo, alipoiumba dunia na vitu vyote vilivyomo, hivi aliviumba kwa ajili ya matumizi yako. Na wa sababu hiyo kila kitu unachokiona ni kweli kuwa kipo kwa ajili ya matumizi yako, iwe vitu vya mbingu, anga na nchi vyote alivifanya kwa ajili ya matumzi yako.
Ikiwa Yeye alifanya hayo kabla ya wewe kuletwa hapo kwanza, humaanishwa kuwa, anajua mahitaji yako kuliko wewe unavyojua. Na kuna mengnie aliyoyaweka ambayo bado hujui matumizi yake lakini nayo aliyaweka kwa ajili ya wewe kuyatumia. Na kwa sababu hiyo, kila iitwapo leo kinagunduliwa kitu kipya ambacho alikifanya kwa ajili ya matumizi. 
Na mengine hadi sasa hayajagunduliwa lakini yapo, na aliyaweka kwa ajili ya matumizi yako. Ikiwa Yeye aliyajua vema mahitaji yako na akayatanguliza kwanza kabla hata ya wewe kuja, imekuwaje sasa kujisumbua sana kwa ajili ya hayo, hata kumsahau Yeye?
 Imekuwaje kutumia muda mwingi kupita kawaida kwa ajili ya kuyatafuta hayo mahitaji aliyokuwekea kuliko hata kumtafuta Yeye, au hata kumpendeza Yeye ambaye ni vyote katika vyote?
Swali hilo, ni la ufahamu tu wa kawaida, ambalo unapaswa kujiuliza, maana ikiwa Yeye aliyeingia gharama ya kufanyia hayo yote, lakini leo unajisumbua kwa ajili ya hayo aliyoyafanya tena kwa ajjili yako, lakin leo unakaa mbali naye kwa kuyatafuta na kuyasumbukia hayo, ni lazima utafakari sawasawa je! unajitendea haki? 
Tena je! Unamtendea haki? Kwa nini uwe kama mtu anayemuonea, je! Itahesabika kuwa wamuonea Yeye? Maana ijapokuwa kwa sasa itaonekana hivyo, lakini Yeye hata tahayarika kamwe, maana ameiweka siku moja tu ambayo kila jambo litafunuliwa wazi, na makusudi yake yatawekwa bayana na hapo, utajichukia wewe na hayo uliyojidhatiti kuyafanya na utayaona kuwa hayakufaa kitu ni heri ungeyaacha hata kumtafuta Yeye usiku na machana. 
Maana ijapokuwa  kwa sasa yanaonekana mbele ya macho ya watu wote kuwa yanafaa, lakini yatakuwa batili mbele ya macho ya watu wote. Maana si kwa shauli lake jinsi unavyoishi bali kwa ushupavu wa matakwa yako, tena kwa mfumo wa dunia ambao unawashurutisha wote kuenenda kwa namna hiyo.
Lakini Yeye aliyekufanya hatanyamanza kusema nawe hata wakati atakapokutwaa kwa malipo ya njia zako. Maana ijapokuwa ugumu umeonekana katikati ya watu wote lakini hataacha kuyathibitisha Maneno yake na shauli lake atalisimamisha mahali pa juu ili kila mtu atie ufahamu na ambaye hatatia ufahamu atalipwa katika hayo.
Ni vema kama leo, utaketi chini na kuyatafakari haya, maana ni kwa salama yako kuyatia katika ufahamu, na kuyapatia ufumbuzi, maana ni hakika kuwa Yeye hana furaha na Wewe katika mwenendo wa Mambo mengi, hasa kwa kutokufanya lile ambalo laufurahisha moyo wake. Lakini je ikiwa hauko hivyo, ujumbe huu wakusu wewe? Hapana wamuhusu huyo asiyefanya jambo hili kwa hakika.
Furaha ya Bwana, ni kupokea anachostahili kwa uradhi wa moyo wake, alipoumba minguni alikusudia kitu, na hicho kimefunuliwa wazi hata kwetu. Kadhalika alipoumba dunia, alikusudia kitu cha pekee, kitu hicho kilifunuliwa wazi majira na nyakati alipoichukua Nafsi aliyoifanya hapo kwanza, na ku uumba  mwili na k uiambia nafsi “kaa ndani ya huu mwili ili utawale hii dunia na vyote kwa ajili yangu”
Na kama aliiweka hiyo nafsi katika mwili ili itawale dunia kwa ajili yake aliye mfalme mkuu katika falme zote, basi hii nafsi ilipewa heshima ambayo hata malaika na wote walioko mbinguni hawakupewa. Maana malaika na jeshi lote la mbinguni humwabudu Yeye na Yeye ndiye mtawala, lakini kwa nafsi hii ya mwanadam/ya kwako aliipa heshima ya kumwabudu Yeye na kutawala dunia kwa ajili yake.
 Hata hivyo, nafsi iliasi na kujifanyia utaratibu wa kwake, na kutawala kwa ajili ya kujifurahisha katika vitu hivyo alivyovifanya kwa ajili ya nafsi ambavyo ingevitumia vema na kumletea Yeye aliyevifanya utukufu. Nafsi hii, katika uasi huo na upotofu huo kwa madaganyo makuu, ilipotoka hata kumuacha Yeye aliyeituma, ikaamua kujitia katika ubatili wa kujifurahisha kwa vitu hivi na kumpa nafasi yeye aliyeasi hapo kwanza yaani ibilisi.

Ni kweli, suruhu ya haya ilikuwa kuufuta utawala huo na hizo nafsi alizozifanya na kuzipa heshima ya kutawala kwa ajili yake. Lakini kwa jinsi alivyoipenda hiyo nafsi kupita kikomo, alivumilia na kutaka kuikomboa, akiingia gharama kila iitwapo leo ili kuirejesha katika makusudi yake. 
Lakini nafsi hii, ifananishwe na nini? Maana kama ni upotofu ulioiingia basi umeifungia mbali na makusudi ya Mungu, kwa kuwa katika kuwaza kwake, huwazi tu kujifurahisha na siyo kujifurahisha katika kumfurahisha Yeye aliyeifanya. Nafsi hii yautumia mwili uliopewa kuutumia kwa ajili ya Mungu, yautumia katika ubatili na kumsukumia mbali Mungu, kwa madanganyo na upotofu mkuu.

Lakini ingekuwa heri sana, kama utayatia moyoni haya, na kujua kuwa, Mungu anataka nini leo? Je! Si kujinyenyekesha mbele zake, kumpa sifa na heshima na utukufu anaostahili, kumfanyia ibada ya kicho cha moyo, kwa kutenga kwanza muda wa kujisongeza mbele zake, ili Yeye naye ahusiane na hii nafsi aliyoifanya? Tena ajiburudishe moyo wake kwa hiyo nafsi kwa kurejea mbele zake kila wakati, maana ikiwa aliipenda kiasi cha kuingia gharama kubwa ya ukombozi, si furaha yake sana aionapo hiyo nafsi ikijihudhulisha mbele zake, kwa kumpa utukufu kwa kuwa ndio ijala ya kazi yake na makusudi ya hayo.

Basi sasa, nakusihi katika pendo lake, uyatie haya katika fahamu zako, na nafsi yako isipotoshwe na mwili wala mfumo wa dunia hii, bali ugeuke na kurejea nyumbani katika shauli na kusudi lake, yaani kutenga muda wa kujihudhulisha mbele zake, ukiwa binafsi na katika wengi, kwa kumpa utukufu na ile tu kukaa mbele zake. 
Jambo hilo ndilo jambo analolifurahia, na hilo analitaka sana kutoka kwako! Na kwa kufanya hivyo, atakuwa Mungu kwako katika uhalisia, nawe utakuwa mtu wake, naye ataisimamia nafasi yake vema, kwa kuwa nawe uatakuwa umejidhihilisha kwake katika uhalisi. Hapo ndipo utakapovikwa utukufu kama utukufu ule wa mwanzo aliokukusudia ambao ni mkuu kuliko ule wa malaika.
Heshima yako itazidishwa katikati ya mbingu na nchi, na vitu vya mbinguni vitamtukuza Yeye kwa ajili yako, kwa kuwa alikufanya kwa ajili ya huo utukufu uletwao mbele zake uwe mkuu sana.
Jitafakari tena na uyapambanue hayo, ili angalau kwa muda udumuo, ufanye jambo la kufaa, kwa ajili yako na kulitimiza shauli la kuwepo kwako.
Mwisho:
Ikiwa utahitaji msaada wa mafafanuzi zaidi, nitumie ujumbe au nipigie, nami nitamuomba huyu aliyetia haya ndani yangu, akupe ufafanuzi huo wa kukufaa zaidi

UTUKUFU UMRUDIE YEYE ALIYETUFANYA SOTE NA VYOTE

(Ni Siri Kuu)

Mwl; Goodluck Kazili
Phone:  0765129960
Email:   gkazili@yahoo.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni


Kunihusu

Picha yangu
"Wakati ule Yesu akajibu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga. Naam, baba , kwa kuwa ndivyo ilivyopendeza mbele zako. (Ni Siri Kuu)

Tafuta katika Blogu Hii