Ni Siri Kuu - The Great Mystery

Ni Siri Kuu - The Great Mystery
"Wakati ule Yesu akajibu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga. Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyopendeza mbele zako.

Jumapili, 5 Novemba 2017

Tarehe 5, Jumapili ya NI SIRI KUU

Juma pili, ni siku maarufu kuliko siku yoyote kote ulimwenguni, ni siku ambayo haifanani na siku yoyote. Siku ya jumapili moja, umaarufu wake unalinganishwa na siku zote za wiki.  Pia thamani ya jumapili moja, inalinganishwa na sikukuu ya Krismasi au Pasaka au mwaka mpya ambayo imefanyika siku za kawaida. Siku nyingine zote huitwa siku za kawaida, lakini siku ya jumapili haiitwi siku ya kawaida.

Katika ulimwengu wa sasa, siku ya jumapili, ndiyo inayojulikana sana kuwa siku ya mapumuziko, hata katika nchi yetu siku hiyo kiselikali na katika taasisi karibu zote ni siku ya mapumuziko. Siku hii imewalazimisha hata wale ambao kwao isingewafaa kupumuzika, kupumuzika, kwa kuwa iko kisheria kuwa siku ya mapumuziko. 

Siku hii huitwa siku ya kuabudu, tena huitwa siku ya mapumuziko, tena huitwa siku ya mwisho wa wiki, japo wengine huiita mwanzo wa wiki.
Waadventist/wasabato, wanaona kitendo hiki cha kuifanya siku ya jumapili kuwa siku ya mapumuziko siyo sawa, tena siyo sawa kabisa kuifanya siku ya kuabudu. Hivyo ukienda maaeneo ambayo wanapatikana wengi, kama ni kijijini, siku ya jumapili wakati hawa wakitembea kwenda kanisani, wao utakutana nao wakiwa wameweka jembe begani wakielekea shamba. Kama ambavyo, na hawa wengine jana juma mosi walibeba jembe kwenda shamba.

Ukiangalia katika torati, suala la kushika sabato ni moja ya Amri kuu. Ambapo mtu aliyeivunja hukumu yake ilikuwa kifo.  Mfano mwanamke mmoja anatajwa katika maandiko aliyeokota kuni siku ya sabato, na kwa kuwa huyo alikuwa wa kwanza kufanya kitendo hicho tangu amri zilipotoka, basi wengi walingoja kuona nini atafanywa mtu yule. Lakini kama ilivyokuwa imeandikwa, mwanamke yule aliuawa na hakuna aliyejaribu kufanya kazi tena siku ya sabato.
Mambo ni tofauti zama hizi, siku hii ya jumapili, hata kwa hao wanaoiita sabato yao, yaani pumziko lao bado huwa wanafanya kazi. Mbali na ile kwamba siku imebadilishwa kutoka juma mosi na kuwa jumapili, lakini bado pia jumapili hii, haitendewi haki.
Kabla ya kuzungumuzia kuhusu mabadiliko ya kuibadilisha sabato kutoka juma mosi na kuwa jumapili tuitazame jumapili kama sabato japo tutazungumzia mabadiliko hayo kwa kina.

JUMAPILI
Jumapili siku ya kupumuzika/sabato, je ni kweli Wewe huwa unapumuzika? Juma pili siku ya kuabudu je wewe unakusanyika pamoja wenzako kuabudu?. Maana hata baada ya Israeli kutoka Misri waliamuliwa kukusanyika sikua ya kwanza na ya saba. Na kusanyiko hilo liliitwa Takatifu. “siku ya kwanza kutakuwa kwenu na kusanyiko takatifu, na siku ya saba kutakuwa kusanyiko takatifu; haitafanywa kazi yoyote katika siku hizo, isipokuwa kwa hiyo ambayo kila mtu hana budi kula, hiyo tu ifanyike kwenu. (Kutoka 12:16)”
Maana ya sabato  ni pumuziko, kama kweli juma pili ni sabato kwa nini haupumuziki, mbona ndiyo siku ya kufanya biashara, mbona ndiyo siku ya kufua, mbona ndiyo siku ya kusoma, mbona ndiyo siku ambayo wengine hata kazini huenda. Usabato wa siku ya jumapili uko wapi? Hilo ni swali lako, ujiulize.
Nina hakika kuwa, hakuna anayefanya hivyo ambaye ana ushahidi unaomruhusu kufanya hivyo.  Najua wengi tutatumia agano jipya kuweka utetezi na hasa ile Yesu aliyomponya siku ya sabato. Ni kweli, kama wewe daktari basi nenda kafanye huduma maana yafaa sana, Kama unatoa huduma ya uokozi basi fanya hivyo maana yafaa sana na ni haki. Lakini kama unaenda kufanya biashara, umegeuza kuwa siku ya kufua, umegeuza uwa siku ya kusoma na hasa mitihani ikikaribia, tena umegeuza kama siku ya kumalizia kazi zako zilizobaki, tena umeigeuza kama siku ya kusafiri, tena ofisi wanakulazimisha kwenda kazini nawe umekubali, huitendei haki hata kidogo siku hii ya jumapili, tena humtendee haki Yeye aliyeamuru mapumuziko na ibada kwa siku hiyo.

Sasa nitaeleza kitu hapa nawe utajishauri. Mwaka 2009/, Mungu alisema nami, kuwaambia wanafunzi ambao walikuwa wakienda kujisomea siku ya jumapili waache na badala yake wapumuzike na kuitumia siku hiyo kumtafakari Mungu na kujisomea Neno la Mungu, Lakini hawakusikia. Nakumbuka sana wakati huo, nilikuwa kiongozi wa maombi, wapendwa hawa walikuwa na kawaida hii, Walikuwa wanaamuka asubuhi wanaenda kwenye ibada ya kwanza, ikifika saa 3 asubuhi wanakuwa wametoka kwenye ibada tayari, kisha wanachukua vitabu na kwenda shule kujisomea hadi jioni.

Tena walitengeneza mtandao wa kuombea mitihani yao miezi 3 hivi kabla ya mtihani kufika, wanafunzi hao walikuwa kitado cha sita. Niliposema nao kuhusu hilo, hawakunielewa, basi nikawaacha. Walipoendelea na kazi hiyo ya kusoma, basi nikiwa njiani naelekea kanisani kwenye kipindi nikifika karibu na uwanja wa ndege pale Dodoma, Sauti ikanijia kusema, watu hawa hawajaniheshimu, kwa sababu hiyo, hawatafanikiwa kama wanavyotazamia sitawafanikisha ijapokuwa wananiomba kwa bidii. Tulipkutana kwenye kipindi, nilisema maana nilitajiwa na matokeo ambayo wangeyapata. Nakumbuka sana wakati huo walikuwa wameshamaliza mtihani wa mock. Na walikuwa wamefaulu sana, hivyo nilipowaambia matokeo watakayopata kwa sababu wameshindwa kufuata maelekezo ya kuiheshimu siku ya jumapili/sabato kwa kupumuzika, lakini ni kama walibeza na kuona kama mtu nichezae na jambo lisilowezekana.

Basi tuliendelea katika hali hiyo, yuko mtu mmoja ambaye alitii na kuacha ambaye alikuja kuniambai kama ushuhuda. Matokeo yalipotoka, wale wapendwa hawakuamini kilichotokea, na kwa ushahidi yule mmoja aliyeacha akafaulu kwa daraja la kwanza na hakutegemewa hata kidogo. Wakati huo waliofaulu vizuri walikuwa 2 miongoni mwetu tuliokuwa katika kundi lile, japo mimi nikiwa kidato cha tano.  Wako walioelewa kilichotekea na wengine hawakuelewa mpaka leo. Mungu hakuwafanikisha vile alivyokusudia, japo baadhi walifaulu kwa arama za kuwawezesha kuendelea na vyou lakini si kiwango kizuri kilichokusudiwa na walichotazamia.

Jumapili ni siku ya mapumuziko, mwanafunzi usisome, mfanya biashara usifanye biashara, mfanya kazi usifanye kazi kama si kazi iliyoainishwa yaani hizo za huduma ya uokozi, mama na Dada nyumbani usiitumie kufua nguo, usiitumie kumalizia kazi zako au kupunguza, usiitumie kujipa kazi. Sote tusiitumie kusafiri. Siku ya jumapili itumie kupumuzika kwa kumwabudu Mungu, kumtafakari, kujifunza Neno, kumsifu, kuwatia moyo wengine, kuwafariji wengine, kuwahubiria wengine nakwa ujumla kuujenga mwili wa kristo.

Jumamosi, 4 Novemba 2017

ZAWADI KWA ALIYEOKOKA

 SIKU MUHIMU KATIKA MAISHA YAKO
ziko siku pengine nyingi zilizo za Muhimu sana kwa mwanadamu katika kuwepo kwake hapa Duniani. Siku muhimu ya kwanza ni siku uliyozaliwa, na siku ya pili ambayo ni kubwa kuliko zote tangu kuzaliwa ni siku hii/hiyo uliyo okoka, na siku ya tatu muhimu ni siku utakapopumzika katika Kristo Yesu.

PONGGEZI KUU KWAKO
Hakika, unastahili pongezi kuu kwa uamzi ulioufikia sasa, uamzi wa kumwamini na kumkiri Yesu kuwa BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAKO, ni uamuzi wa maana na hatua kubwa kuliko hatua yoyote katika maisha. Hii ni kwa sababu pia watu wengi hawapati neema ambayo wewe umeipata, hivyo Huduma ya (Ni Siri Kuu, kupitia Mwl. Goodluck Kazili) na waamini wote pamoja na walioko mbinguni tunakupongeza kwa uamuzi wako. Ni wazi umuhimu wake unaweza usionekane haraka, lakini thamani yake ni kubwa kuliko mambo yote kwako hapa Duniani.

THAMANI ULIYOIPATA
Uko ufalme wa nuru (MUNGU), tena uko ufalme wa giza, hivyo wewe siyo tena wa ufalme wa giza bali ni wa ufalme wa nuru yaani wa MUNGU mwenyewe aliyeumba mbingu  na  nchi katika Kristo Yesu Pamoja na Roho Mtakatifu. Thamani kubwa kwanza uliyoipata ni ile ya kuondolewa kaitka    ufalme wa giza   shetani na kuingizwa katika ufalme wa Mungu. Na      apa inathibitishwa hivi
“Naye alituokoa kutoka katika nguvu za giza akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake, ambaye katika Yeye tuna ukombozi, yaani msamaha wa dhambi (Wakolosa 3:13-14)”
Thamani hii imetokana na upendo wa Yesu, ambaye aliitoa Damu yake kusudi kwa hiyo uweze kutakaswa, hapa anasema, “Yeye atupendaye na kutuosha dhambi zetu kwa damu yake. (Ufunuo 1:5b)”
Hata hivyo jua kuwa ulipokuwa haujaokoka/ haujazaliwa mara ya pili kwa roho haukuwa na thamani katika ufalme wa Mungu, na usingeweza kuuona wala kuuingia kwa hakika, maana Yesu mwenyewe anasema Lakini wewe sasa kwa njia ya Roho, umezaliwa mara ya pili, hivyo umepata sifa ya kuuona na kuuingia ufalme wa Mungu. Sasa wewe ni wa thamani sana mbinguni na Duniani.

UMUHIMU WA KUOKOKA/WOKOVU
Kuokoka au kupata wokovu si suala la dini, wala suala la kanisa fulani, wala haki ya dhehebu fulani, bali ni mpango mahususi tena kamili wa Mungu kumuokoa na kumkomboa mwanadamu kwa njia ya imani, maana hapa maandiko husema “kwa sababu ukimkiri Yesu Kristo kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako  ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, UTAOKOKA. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu. (Warumi 10:9-10)” na si jambo jema hata kidogo kufikiri kuwa wokovu ni wa watu wa dhehebu fulani. Bali ni baraka tena ni haki tena ni faradhi kufikiri na kujua kwa hakika kuwa wokovu ni mpango wa Mungu wa kumuokoa kila mwanadamu. Ni vibaya sana dhehebu kujimilikisha wokovu, na ni vibaya sana dhehebu kuukataa wokovu na kuona kuwa ni kitu cha watu fulani.
Ni kweli na hakika kuwa mtu asiyeokoka, hawezi kuuona wala kuuingia ufalme wa mbinguni. Hapa Yesu anasema “amini amini nawaambieni mtu asipozaliwa mara ya pili hawezi kuuona ufalme wa mbinguni. (Yohana 3:3). lakini maneno haya kwa wengine yalionekana kuwa magumu, kwa kujiuliza inawezekanaje mtu kurudi tumboni mwa mama yake na kuzaliwa tena mara ya pili? Katika fahamu zetu kama wanadamu haiwezekani kabisa, lakini hapa Yesu anabainisha tena kwa msisitizo zaidi kwa kusema ““amini, amini, nakuambia mtu asipozaliwa kwa Maji na kwa Roho hawezi kuuingia ufalme wa Mungu (Yohana 3:5)” Katika mafafanuzi ya usemi huu, anasema “kilichoza; liwa na mwili ni mwili nakilichozaliwa kwa roho ni roho”, hapa alimaanisha kuwa unapozaliwa mara ya kwanza unazaliwa katika tumbo la mama yako, hapo wewe ni mwili kabisa, lakini mwili hautaurithi ufalme wa mungu. Hivyo kama umezaliwa na mama yako ambaye ni mwili, basi hata wewe ni mwili, na kwa sababu hiyo usipozaliwa katika roho huwezi uuona wala kuuingia ufalme wa Mungu. Kuzaliwa katika roho ni kwa njia ya imani ya kumwamini Kristo Yesu, na kutiwa muhuri yaani kubatizwa. Lakini hapo kinachohitajika tena ni ile kukiri hicho unachokiamini, yaani huyo Kristo unayemwamini moyoni mwako kumkri, ambapo kukirki huko kunakufanya uokoke, kunakufanya upate wokovu. awaye yeyote asikudanganye wala kukuhubiri injili yoyote inayokanusha habari hizi, maana huo ndio uzima wako, wala jambo liwalo lolote lisikutoe katika kuamini huko kunakotajwa maana thamani          yake ni zaidi ya chochote. Hapa Yesu ananena “kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake? (Mathayo 16:26)”. Hakuna uwezacho kutoa na kuwa fidia ya nafsi yako, bali wokovu pekee ndio jibu na uzima wa nafsi.
WOKOVU NI MCHAKATO
Suala la wokovu huanza siku moja, lakini halikamiliki ndani ya siku moja hiyo hiyo, maana ni mchakato ambao unamhitaji mtu mwenyewe kuhusika kikamilifu kwa msaada wa huyo Roho Mtakatifu. Ndiyo maana kati ya vitu muhimu ambavyo mtu anavihitaji mara anapo okoka, ni kumpokea Roho Mtakatifu.
Kuokoka na kutokuwa na roho mtakatifu ni sawa na kumvua samaki wa kufuga kisha ukamwacha bila maji, lazima tu atakufa, ndivyo alivyo mtu anayeokoka na kuendelea kuishi bila ujazo wa Roho Mtakatifu. Ama ni kama mtu anunuaye gali na kuiendesha bila kuwa na oili, gali hiyo lazima itanoki injini na itakufa kabisa.
Ndugu uliyeokoka, unahitaji Roho Mtakatifu sasa, ili uingie katika hatua nyingine ambayo sasa utaanza kumjua Mungu. Maana ni kweli kuwa hatupati uzima wa milele ile tu kuokoka, bali kuokoka ni hatua ya msingi wa kutupeleka kwenye hatua  za kumjua Mungu ambao ndio uzima wa milele. “kama vile ulivyompa mamlaka juu ya wote wenye mwili, kusudi wote uliompa awape uzima wa milele. Na uzima wa milele ndio huu, wakujue wewe Mungu wa pekee, wa kweli na Yesu kristo uliyemtuma. (Yohana 17:2-3)”. Wokovu unafikia hatua ya utimilifu mara unapofika kiwango cha kumjua Mungu katika kweli. Hatua hii huwezi kuiingia bila kuwa na Roho Mtakatifu       
 Maa     na hakuna ajuaye mambo ya Mungu ila Roho Wa Mungu. Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ua binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu. (1Wokorintho 2:11)”
Hivyo hakuna awezaye kumjua Mungu asipojulishwa na Yesu kwa njia ya Roho Mtakatifu. Na ndiyo sababu Yesu aliwasisitiza sana wanafunzi, kuwa ni muhimu sana Yeye aondoke ili kusudi Roho Mtakatifu naye aje ambae atawafundisha kumjua Baba yaani Mungu kwa huyo Roho ambaye watampokea mara baada ya Yesu kuondoka. “lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana mimi nisipoondoka, huyo msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu. Naye akisha kuja huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu. (Yohana 16:7-8)”
Hivyo maadamu umeokoka, kwa maana ya kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yako, hapo umestahili kumpokea Roho Mtakatifu. Ambaye Yesu anampeleka kwako makusudi tu akufunulie kumjua Mungu. “Akasema, nimekabidhiwa vyote na baba yangu; wala hakuna amjuaye Mwana, ila baba; wala hakuna amjuaye Baba ila Mwana, na yeyote ambaye Mwana apenda kumfunulia. (Mathayo 11:27)”
Kwa ufafanuzi huo, wokovu huanza na Imani moyoni, kisha kukiri kile ulichokiamini. Huo tunaita kuokoka, lakini mara baada ya kuokoka, sasa unapaswa kumpokea/kujazwa Roho Mtakatifu, ili akufikishe mahali unapotakiwa kufika yaani kumjua Mungu.
Si wewe tu ambaye umeokoka na inawezekana ukawa huna Roho Mtakatifu, bali wako wengine. Tena kwenye maandiko wanatajwa watu ambao walikuwa wameokoka lakini hawajui hata kama kuna kitu kinaitwa Roho Mtakatifu maana hata kusikia tu hawakuwahi kusikia.
“Paulo akiisha kupita kati ya nchi za juu, akafika Efeso; akakutana na wanafunzi kadha wa kadha huko; akawauliza, je! Mlimpokea Roho Mtakatifu mlipoamini? Wakamjibu, la, hata kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu hatukusikia. (Mdo 19:1-2)”
Lakini haikuwa haki kwao kuokoka na kuishi bila kuwa na Roho Mtakatifu. Hapo sasa ndipo walipoamini upya kwa kubatizwa kisha wakampokea Roho Mtakatifu wote kwa idadi yao. “Na Paulo alipokwisha kuweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao; wakaanza kunena kwa lugha, na kutabiri. Na jumla yao walipata wanaume kumi na wawili. (Mdo 19:6-7)”


Mwl. Goodluck Kazili
(NI SIRI KUU/THE GREAT MYSTERY)
Hakiuzwi/ kimeamuliwa na Mungu kama Sadaka

NGUZO YA KUKUFANIKISHA KATIKA KILA OMBI UOMBALO

UAMUZI WA DHATI KUHUSU KUOMBA

Ili uweze kuomba vema na kufanikiwa katika kuomba kwako, pamoja na mambo mengine ni lazima uwe umefanya maamuzi ya kuomba. Maamuzi yanakuja kama matokeo ya sababu ya kutaka kuomba. Si mara nyingi sana watu wanaingia kwenye kuomba wakiwa wamefanya maamuzi, ni mara chache sana mtu anaweza kuingia kuomba akiwa amefanya maamuzi ya kuomba.

Unaweza kuwa na sababu za kuomba lakini usifanye maamuzi ya kuomba, hivyo ukaoma tu kwa sababu inakubidi uombe, ngoja niombe lakini hujafanya maamuzi ya kuomba. Mara nyingi hatuombi kwa sababu tumeamua kuomba, bali tunaomba kwa sababu imetulazimu kuomba, na kwa kuwa hakuna njia nyingine, au pamoj na njia nyingine ngoja pia niombe tu.
Kwa nini ni lazima kufanya maamuzi wa dhati ndipo uombe
  • Uamzi ndiyo siraha pekee ya mtu kuweza kuomba na kufika mwisho, au kuweza kufaidi uombaji anao uomba
  • Utaelewa thamani ya kuomba ikiwa tu umeomba kwa maamuzi
  •  Utapata unachopata kwa uzuri halisi ikiwa utaomba kwa maamuzi
  •  Utajifunza zaidi katika uombaji wako ikiwa utaomba kwa maamuzi
Ukioba bila kufanya Maamuzi,
  • §  hutaona thamani ya kuomb
  • §  hutapata kilicho katika kuomba
  • §  hutatambua nafasi yako katika kuomba
  • §  hutajua Mungu anahusikaje wakati  unapoomba
  • §  hutajua unaathili upande wa adui kiasi gani ,na
  • §  hutakuwa na msimamo katika kuomba
Uamuzi wa kuomba
Ni matokeo ya picha unayoiona ya jambo/mtu/kitu ambacho ni hitaji kwako. Picha hiyo ni ya imani, inayokuelekeza  umuhimu na thamani ya kuomba, matokeo ya kuomba, maelekezo ya kuomba, nguvu na mamlaka ya kuomba.
Uamuzi wa kuomba unakuja baada ya kuona umuhimu na thamani ya kuomba, tena ni pale unapokuwa umeona/unaona matokeo ya kuomba hupo utakapoomba, siyo imani ya kuamini tu bali unaona katika ufahamu hayo matokeo, tena ni hapo yanapokuja maelekezo ya kuomba, na katika hayo yote unahisi na kusikia nguvu ya kuomba na kuwa na mamlaka ya kiuombaji kuhusu hilo hitaji.
Namna ya kufanya maamuzi ya kuomba unapotaka kuombea jambo/mtu
Mambo haya  4 ni lazima uwe na uwezo wa kuyafanya au kuyapata ndipo utakapofanya Maamuzi
Ø  Tafuta kwanza ufahamu wa kiroho kuhusu jambo/eneo/mtu/kitu unachotaka kuombea
Danieli alifanya maamuzi ya kuomba; maamuzi hayo yalitokana na ufahamu alioupata kuhusu jambo analotaka kuomba, ufahamu ambao aliupata kwa kuvisoma vitabu vilivyoandika habari za kiroho kuhusu Yerusalemu. hapa maandiko hunena “katika mwaka wa kwanza wa kumiliki kwake, mimi Danieli, kwa kuvisoma vitabu, nalifahamu miaka ambayo Neno la BWANA lilimjia Yeremia nabii, ya kuutimiza ukiwa wa Yerusalemu, yaani miaka sabini, nikwamwelekezea Bwana Mungu uso wangu, ili kutaka kwa maombi, na dua, pamoja na kufunga, na kuvaa nguo za magunia na  majivu. (Danieli 9:2-3)”
Ø  Kutambua umuhimu na thamani ya kuomba
Maamuzi ya dhati yanategemea thamani unayoiona katika jambo unalotaka kulifanya, thamani hii inategemea msingi uliyonayo katika kuomba, na unaamini kuomba kwa asilimia ngapi, na tafisiri ulizonazo na shuhuda kuhusu kuomba. Unaweza ukawa una historia mbaya kuhusu mafanikio ya kiuombaji, yaani huna imani sana na mafanikio yanayopatikana katika uombaji. Mtu anayejua uombaji ni nini na uwezo wake huthamini sana kuomba na huona kuomba kuwa kitu cha thamani kwenye maisha yake kuliko chochote kile. Jambo hili linawezekana tu kwa mtu ambaye amefuatilia masuala ya kiuombaji, shuhuda mbalimbali kuhusu uombaji, ahadi za kiuombaji katika Neno la Mungu, mafanikio ya watu walioomba katika maandiko.
Twafahamu habari za Mwanamke Hanna, jinsi alivyofanya maamuzi ya kuomba, na kufanikiwa vema kupata alichotaka.  (1Samweli 1:10)  ukiendelea unaona matokeo ya kuomba kwake, na jinsi tena alivyozidi kuomba kama shukrani yake kwa Mungu. (sura ya 2)
Elisha akaomba kusema na Bwana kuhusu kumfumbua macho mjakazi wake ili aone ulinzi aliowawekea Bwana dhidi ya maadui waliokuwa wamewazunguka (2 Wafalme 6:17) Twafahamu habari ya Hezekia; “Basi Hezekia akajigeuza, akaelekeza uso wake ukutani, akamwomba BWANA, akasema, Ee BWANA. Ikawa, Neno la BWANA likamjia Isaya, kusema, Enenda ukamwambie Hezekia, BWANA, Mungu wa Daudi, baba yako, asema hivi, Mimi nimeyasikia maombi yako, nimeyaona machozi yako; tazama nitaziongeza siku zako, kiasi cha miaka kumi na mitano. (Isaya 38:2,4,5)”
Ø  Matokeo unayoona wakati utakapokwisha kuomba
Hupaswi kuona matoke ya kuomba baada ya kumaliza kuomba, bali matokeo huwa yanaonekana kabla ya kuomba. “Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana. (Waebrania 11:1)”. Eliya alimwambia Ahabu kuwa nvua inakuja kabla hajaomba, alipoenda kuomba ilimgharimu kuomba mara saba, kama si maamuzi ya kuomba aliyokuwa ameyafanya ambayo yalitokana na kuona matokeo ya kuomba kabla hajaomba, angeishia njiani kwenye kuomba kwake.
Kuona matokeo ya kuomba hiyo ndiyo imani halisi. Maandiko hunena wazi kuwa “imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana”. Ni kusema kuwa, kuwa na uhakika, ni kuona kile kitu ambacho hakionekani bado kwa macho ya nyama. Imani inakupa uhakika wa kitu kabla ya wewe kukipata, imani inkuonyesha kitu ambacho hakionekani nje ya imani, ndiyo maana imani ni kwa vitu visivyoonekana tu basi. “Akasema nitawaficha uso wangu, nitaona mwisho wao utakuwaje; Maana, ni kizazi cha ukaidi mwingi, watoto wasio imani ndani yao. (Kumb 32:17)”
Imani si kuamini tu, bali ni kuona ambako ndiko kunakopaswa kukupe kuamini. Kuamini ni ile inayokuja baada ya kuwa na uhakika, uhakika ambao umekuja baada ya kuona ishara au hali au kitu au kidokezo kinachothibisha hilo jambo japo bado halijadhilika au halijatimia au halionekani wazi. Imani ni ule uhakika anaokuwa nao mtu ndani yake kuhusu jambo, hali, kitu, mtu n.k.
Kuwa na imani ndogo au kubwa ni kiwango cha uhakika ulionao juu ya hilo jambo/kitu katika kutenda kwake, kutimia kwake, kufanikiwa kwake n.k
Huo uhakika, ili uwepo, ni hadi mtu awe na hati milki ya uwezo, nguvu, mamlaka, neema na rehema ndani yake vilivyo vya Mungu. Ambavyo mara zote vinakuja kutokana na kumjua Mungu. Imani chanzo chake ni kusikia kusikia ambako huja kwa Neno la Kristo. Kusikia huko si tu kule kusikia Neno la Mungu, ni kusikia ambako kumekuja kama neno lakini Neno la imani. Neno lenyewe ambalo ni imani linaingia ndani yako ndipo unapokuwa na uhakika. Neno la Mungu ndiyo Kweli, hivyo huwezi kuwa na uhakika yaani ukweli kama si Neno la jambo hilo.
“Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba Yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao. (Waebrania 11:6)”
Kuwa na imani kunahusisha mambo mengi, moja kubwa ni kumjua Mungu, ambako kunatiwa nguvu na wema, maarifa, kiasi, saburi, utauwa, upendo. (2 Petro 1:5-7) - (9)
Ø  Maelekezo ya kuomba
Maelekezo ya kuomba yanakusukuma kufanya maamuzi, ambao unatokana na utayari unaoupata kwa kuwa unamaelekezo ya kuomba.
Kuomba ni safari, ambayo kuianza au kutoianza kunategemea uhakika wa safari (Imani), kunategemea Maelekezo ya safari, tena kunategemea umuhimu wa safari.
Maelekezo ya namna ya kuomba ni nyenzo muhimu katika kukusukuma kufanya maamuzi ya kuomba. Maelekezo kuwa nayo au kutokuwa nayo kunategemea na kiwango cha neno ulichonacho kuhusu jambo hilo, pia inatokana na kiwango cha uhitaji kinachoonekana ndani yako, tena inategemea mazoea uliyonayo kuhusu kuomba, tena inategemea kiwango cha imani uliyonayo katika Mungu, na zaidi sana inategemea uhusiano ulio nao na Roho Mtakatifu. Kuwa na maelekezo ni sawa na kupata utaratibu wa namna utakavyofanya kazi fulani, jambo hilo litakusukuma kuwa tayari kuifanya, kadhalika maelekezo kuhusu kuomba yanakusukuma kufanya maamuzi maana unajua kwa hakika unachotakiwa kufanya na mwisho wake utakuwa upi.
(Daniel 9:1-22)
Ø  Mamlaka, nguvu na kibali cha kuombea jambo hilo
Kuwa na kibali au mamlaka ya Mungu ndani yako inakusukuma kufanya maamzi ya kuombea jambo. Kama ndani yako husikii kuwa na mamlaka, utaombea jambo bila kufanya maamuzi, kwa sababu huwezi kufanya maamuzi kama ndani husikii kuwa na mamlaka au kibali cha jambo hilo. Yesu alisema, ni nani atakaye kujenga mnara, asiyeketi chini kwanza na kuhesabu gharama?, huwezi kufanya maamuzi ya kuomba  ikiwa hujisikii kuwa na uwezo wa kuombea jambo hilo na kufika mwisho.
Hivyo ili mtu uweze kufikia kufanya maamuzi katika kila hitaji unalotaka kuomba, ni lazima ujitahidi kuwa na hayo mambo manne. Ni vema sana mtu ukiwa nayo ya kudumu, si kwa ajili ya hitaji moja tu.
Msisitizo kuhusu maamuzi katika kuomba
Maamzi ni msingi muhimu sana, katika kufanikisha kuomba kwako. Ni mara chache sana kutokea kuomba ukiwa umefanya maamuzi kisha usifanikiwe katika kuomba kwako. Kati ya msingi unaowakwamisha wengi katika kuomba kwao ni kuomba kabla/bila kufanya maamzi ya kuomba. Huwezi kuona rahisi kuwa unaweza kuomba bila kufanya maamuzi, na unaweza kujiuliza tuna maana gani kusema kuwa mtu anaweza kuomba bila kufanya maamuzi. Lakini ni wazi na ni kweli na wengi wanaomba bila kufanya maamzi, maana ukienda kwenye ibada ya maombi, kisha ukaambiwa tunataka tuombee jambo furani, ukaomba kama Dakika 10, je! Utafuatilia kama lile jambo uliloliombea kwenye kipindi limefanikiwa au bado?, ni adimu sana kutokea kuuliza.
“Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye.(Waebrania 10:38)”
Huwezi kusema wakati unaomba ulifanya maamuzi, maana kama ungekuwa umeombea jambo ulilolifanyia maamzi lazima kwenye kuomba kwako ungepata majibu hapo hapo, si jibu lile la suruhu ya jambo lakini hata ile tu kujua kuwa ni  nini kimefanyika na unategemea matokeo gani, na hapo utayangoja ili uyaone kwa hakika.
Kuna maombi machache sana kwenye maisha yako ambayo unaweza kuwa umeyaomba ukiwa umeyafanyia maamuzi. Na utagundua kuwa karibu kila jambo uliloombea kwa kufanya maamzi basi ulijibiwa/ulifanikiwa.
“kuomba kwake mwenye haki, kwafaa sana akiomba kwa bidii” (Yakobo 5:16b)
Maamuzi ya kuomba siyo yale ambayo mnafanya maamuzi kwa kusema tumeamua kuombea kitu fulani. Bali ni ile ya maamuzi ya kuomba kwa hakika bila kuchoka wala kukata tamamaa hadi upate unachotaka. Inakuja kutokana na uhakika wa njia hii ya kuomba kuwa ndiyo pekee itakayokufikisha katika hali au jambo unalolihitaji.
Mfano mtu anasema nimeamua niombee jambo hili kwa wiki mbili huku nikifunga ili jambo hili liishe.
Mfano halisi wa mtu aliyefanya maamuzi ya kuomba ni habakuki. Maandiko yanatueleza hivi “ Mimi nitasimama katika zamu yangu, nitajiweka juu ya mnara, nitaangalia ili nione atakaloniambia, na jinsi nitakavyojibu katika habari ya kulalamika kwangu. (Habakuki 2:1)”
Kadhalika Eliya, alifanya maamuzi ya kuomba, hapa maandiko hunena kwanza “Eliya alikuwa mwanadamu mwenye tabia moja na sisi, akaomba kwa bidii mvua isinyeshe, na nvua haikunyesha juu ya nchi muda wa miaka mitatu na miezi sita, akaomba tena, mbingu zikatoa mvua, nayo nchi ikazaa matunda yake. (Yakobo 5:17-18)”
Eliya, anatajwa kuwa ni mwanadamu mwenye sifa/tabia kama za kwetu, lakini katika uwepo wa maamuzi aliomba na kufanikiwa. Kilichomfanikisha ni kitu gani ni maamuzi, maana kama siyo maamuzi asingeomba kwa bidii. Na alipoomba mara ya kwanza na hakupata mafanikio angekata tamaa na kuacha, lakini kwa kuwa alishafanyia maamuzijambo analotaka kulifanya hivyo kuomba kwake haikuwa tu kuomba, bali kuomba hadi apate anachoomba.
Hapo juu tumesoma habari za Daniel, ambaye aliomba maombi yasiyokuwa ya kawaida na akafanikiwa, lakini kama ukitazama kilichomsaidia utaona kuwa, ni maamuzi aliyoyafanya ambayo yalikuwa yanatokana na ufahamu alioupata katika kuvisoma vitabu.
 Mwl. Goodluck Kazili (Ni Siri Kuu – The Great Mystery)

TAREHE 4, JUMA MOSI YA NI SIRI KUU


TAREHE 4; JUMA MOSI YA NI SIRI KUU

“Wakati ule Yesu akajibu, akasema Nakushukuru, Baba, BWAna wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga, naam Baba kwa kuwa ndivyo ilivyopendeza mbele zako. (Math 11:25)

Kama leo tungekuwa mashariki ya kati na tukiwa kama Wayahudi, leo haingetupasa kufanya kazi yoyote ile Zaidi ya kushinda hekaluni tukimwabudu BWANA na kujifunza kuishi na kushika Amri zake.

Lakini leo mambo ni tofauti kabisa, ni wachache tu miongoni mwetu ambao leo ilionekana kuwapasa kushinda hekaluni/kanisani kumwabudu BWANA na kujifunza kushika amri zake.

Haikanushiki kuwa, ndivyo walivyoagizwa wayahudi, kufanya hivyo siku zote za maisha yao, kadhalika ndivyo walivyoagizwa wanadamu wote tangu uumbaji.

Lakini swali la kujiuliza, ni kwa nini haiko hivyo hivi leo kwa wengi wetu?
Kwa nini jamii tu ya wayahudi kadhaa ndio waliohusika na suala la kuabudu leo, tena kwingineko kote mbali na huko Israeli, ni ndugu waitwao wa Adventist/Wasabato ndio waliofanya hivyo

“kwa maana ameinena siku ya saba mahali Fulani hivi, Mungu alistarehe siku ya saba, akaziacha kazi zake zote; (Wae 4:4)”
Na hapa anaongeza “Basi imesalia raha ya sabato kwa watu wa Mungu. (Waeb 4:9)”

Haipingiki kwamba jumamosi ni siku ya saba kwa majira ya hapo Mashariki ya kati, ambayo ni siku maalumu ya kupumzika. Japo jambo hili, huonekana kama jambo la wayahudi, wasabato, ambao msingi wa kutenda kwao hivyo ni maagizo ya torati.

Lakini tuitazame siku Yenyewe. Juma mosi, ni siku ya kuabudu, tena ni siku ya kazi, lakini pia kwa wengine ni siku ya starehe mbali na pumuziko takatifu/sabato.  Juma mosi Kila mtu anaitumia anavyotaka na anavyoona inamfaa, na wala hakuna sheria yoyote ambayo inawataka watu wote kuitumia siku hiyo kwa matumizi maalumu kama ilivyotajwa kwenye torati.

Katika mazingira yetu, ofisi za selikali baadhi zinafunguliwa, japo ni nusu siku. Ofisi za taasisi binafsi zenyewe hufanya kazi kama kawaida, ukija upande wa wanafunzi, madarasa ya mitihani ya taifa huwa wanaenda, japo si siku rasimi inayohesabika kuwa ya masomo.
Je, siku hii inatendewa haki? Hasa kwa kuzingatia matumizi ambayo Mungu aliyakusudia yatumike. Kama mazingira yangekuwa yale ya bustanini, na kwa agizo lile la kupumuzika siku ya saba, basi ni hakika kuwa, leo wote tungeshinda kwenye nyumba za Ibada kumwabudu Mungu, au lakini tusingefanya kazi.

Mabadiliko mengi, kuanzia uasi, hata  wakati wa ujio wa Yesu, umeifanya siku hii, ipoteze umaarufu wake, na nafasi yake katika wanadamu.

Nani anahusika katika hili? wa kwanza Mwanamke, wa pili Mwanaume, kwa pamoja Adamu. Wa pili Yesu Kristo.  Najua kumtaja Yesu kama mhusika ni kama hatujaenda sawa, lakini anahusika sana, maana kama si ujio wake basi, wote walio wa Imani ya Mungu mwenyezi wangeabudu leo.
Lakini je!, tulioenda kuabudu leo ndio tulio na haki, na tena je sisi tusioenda kuabudu leo hatuna haki katika hili?

Karibu kwenye Tarehe 5, Jumapili ya Ni siri kuu,
Hapo ndipo siri ya siku hizi mbili itakapofunuliwa.

By Mwl. Goodluck Kazili (Ni Siri Kuu – The Great Mystry)

(October)

Kunihusu

Picha yangu
"Wakati ule Yesu akajibu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga. Naam, baba , kwa kuwa ndivyo ilivyopendeza mbele zako. (Ni Siri Kuu)

Tafuta katika Blogu Hii