Tumia
muda wako japo mfupi kusoma haya, na kuyatia katika fahamu zako, maana huendayakakufaa ikiwa Roho wa Mungu atakusaidia kuyafahumu vema.
Unafkiri
vipi ukifanya kitu kwa lengo flani kisha kile kitu ulichokifanya wewe kikakataa
au kushindwa kufanya vile utakavyo, hapo utajisikiaje? Na je! utafanya nini?
Hivi unajua kwa nini dunia iliumbwa! Na kwa nini wewe uliumbwa! na aliyeiumba
hii dunia alikusudia nini! na aliyekuumba wewe alikusudia nini!. Ukimuuliza
mama yako na baba yako kama wako hai watakwambia kwa nini waliamua kukubali
wewe uwepo kwenye dunia hii! Lakini ikiwa wao tu wasioweza kukufanya wewe, ila
tu walitumiwa kukuleta, ikiwa ni kweli walikuwa na malengo na ujio wako, vipi
aliyekufanya kabisa, aliyekupa uhai ndani yako, akili ya kufikri na kutambua,
nafasi yake kwako ni ipi?. Ni sawa kuwa Yeye ni Mungu, lakini kuwa Mungu, na
wewe kumtambua kuwa Mungu haifanyi kitu kikubwa, isipokuwa kikubwa ni yale malengo
ya aliyekufanya yanapokuwa yametekelezwa.
Hayo
unayoyafanya, kabisa ni moja ya malengo ya Mungu, kwamba uyafanye, mbali na
yale yasiyokubalika ambayo unaweza kuwa unayafanya kimakosa. Hivyo mbali na
hayo mabaya, hayo mema ambayo unayafanya na kuyapata, ni sehemu halisi ya
malengo ya Mungu kukuweka kwamba upate kuyafanya. Lakini hayo yanakuridhisha na
kukufurahisha wewe, je unafkri kitu gani ambacho kwa dhahili wewe ukikifanya
chaweza kumpendeza huyo aliyibeba dhamana yako na aliyekuleta kwa malengo makuu
kabisa, ambaye anahuzunika kila siku kwa sababu tu wakati mwingi humfanyii kila
anachotamani kutoka kwako?.
Ijapokuwa huchoki kumuomba na kuhitaji msaada kwake,
lakini je! kwa kuwa wajibidisha katika kumuomba ndilo jambo linalompendeza, au
je ni mzazi gani ambaye anaweza kumfurahia mtoto wake kwa kuwa anamuomba tu
kila siku ikiwa mtoto huyo hafanyi mengine yanaupendeza moyo wa huyo mzazi?.
Je
wewe utafurahishwa na mtoto atakayekuomba na kukulilia kila siku umsaidie katika
mahitaji yake tu? Au hata kama ungekuwa na rafiki ambaye Yeye ni kukuomba tu,
wala hafanyi jambo lolote linaloupendeza moyo wako, hivi kweli utapendezwa na
huyo mtu? Ikiwa hautapendezwa ndivyo
ambayo Yeye aliyekuumba hapendezwi na Wewe kumuomba tu usiku na mchana kwa
ajili ya mahitaji yako, bali ingefaa sana kama ungeomba pamoja kufanya kile
ambacho kinaupendeza moyo wake
Mungu kabla hajakufanya wewe, alikufanyia
kwanza mahitaji utakayoyatumia, wakati wote utakaokuwepo, alipoiumba dunia na
vitu vyote vilivyomo, hivi aliviumba kwa ajili ya matumizi yako. Na wa sababu
hiyo kila kitu unachokiona ni kweli kuwa kipo kwa ajili ya matumizi yako, iwe
vitu vya mbingu, anga na nchi vyote alivifanya kwa ajili ya matumzi yako.
Ikiwa
Yeye alifanya hayo kabla ya wewe kuletwa hapo kwanza, humaanishwa kuwa, anajua
mahitaji yako kuliko wewe unavyojua. Na kuna mengnie aliyoyaweka ambayo bado
hujui matumizi yake lakini nayo aliyaweka kwa ajili ya wewe kuyatumia. Na kwa
sababu hiyo, kila iitwapo leo kinagunduliwa kitu kipya ambacho alikifanya kwa
ajili ya matumizi.
Na mengine hadi sasa hayajagunduliwa lakini yapo, na
aliyaweka kwa ajili ya matumizi yako. Ikiwa Yeye aliyajua vema mahitaji yako na
akayatanguliza kwanza kabla hata ya wewe kuja, imekuwaje sasa kujisumbua sana
kwa ajili ya hayo, hata kumsahau Yeye?
Imekuwaje kutumia muda mwingi kupita
kawaida kwa ajili ya kuyatafuta hayo mahitaji aliyokuwekea kuliko hata
kumtafuta Yeye, au hata kumpendeza Yeye ambaye ni vyote katika vyote?
Swali
hilo, ni la ufahamu tu wa kawaida, ambalo unapaswa kujiuliza, maana ikiwa Yeye
aliyeingia gharama ya kufanyia hayo yote, lakini leo unajisumbua kwa ajili ya hayo
aliyoyafanya tena kwa ajjili yako, lakin leo unakaa mbali naye kwa kuyatafuta
na kuyasumbukia hayo, ni lazima utafakari sawasawa je! unajitendea haki?
Tena
je! Unamtendea haki? Kwa nini uwe kama mtu anayemuonea, je! Itahesabika kuwa
wamuonea Yeye? Maana ijapokuwa kwa sasa itaonekana hivyo, lakini Yeye hata
tahayarika kamwe, maana ameiweka siku moja tu ambayo kila jambo litafunuliwa
wazi, na makusudi yake yatawekwa bayana na hapo, utajichukia wewe na hayo
uliyojidhatiti kuyafanya na utayaona kuwa hayakufaa kitu ni heri ungeyaacha
hata kumtafuta Yeye usiku na machana.
Maana ijapokuwa kwa sasa yanaonekana mbele ya macho ya watu
wote kuwa yanafaa, lakini yatakuwa batili mbele ya macho ya watu wote. Maana si
kwa shauli lake jinsi unavyoishi bali kwa ushupavu wa matakwa yako, tena kwa
mfumo wa dunia ambao unawashurutisha wote kuenenda kwa namna hiyo.
Lakini
Yeye aliyekufanya hatanyamanza kusema nawe hata wakati atakapokutwaa kwa malipo
ya njia zako. Maana ijapokuwa ugumu umeonekana katikati ya watu wote lakini
hataacha kuyathibitisha Maneno yake na shauli lake atalisimamisha mahali pa juu
ili kila mtu atie ufahamu na ambaye hatatia ufahamu atalipwa katika hayo.
Ni
vema kama leo, utaketi chini na kuyatafakari haya, maana ni kwa salama yako
kuyatia katika ufahamu, na kuyapatia ufumbuzi, maana ni hakika kuwa Yeye hana
furaha na Wewe katika mwenendo wa Mambo mengi, hasa kwa kutokufanya lile ambalo
laufurahisha moyo wake. Lakini je ikiwa hauko hivyo, ujumbe huu wakusu wewe?
Hapana wamuhusu huyo asiyefanya jambo hili kwa hakika.
Furaha
ya Bwana, ni kupokea anachostahili kwa uradhi wa moyo wake, alipoumba minguni
alikusudia kitu, na hicho kimefunuliwa wazi hata kwetu. Kadhalika alipoumba
dunia, alikusudia kitu cha pekee, kitu hicho kilifunuliwa wazi majira na
nyakati alipoichukua Nafsi aliyoifanya hapo kwanza, na ku uumba mwili na k uiambia nafsi “kaa ndani ya huu mwili ili utawale hii dunia na vyote kwa ajili yangu”.
Na kama aliiweka hiyo nafsi katika mwili ili itawale dunia kwa ajili yake aliye
mfalme mkuu katika falme zote, basi hii nafsi ilipewa heshima ambayo hata
malaika na wote walioko mbinguni hawakupewa. Maana malaika na jeshi lote la
mbinguni humwabudu Yeye na Yeye ndiye mtawala, lakini kwa nafsi hii ya
mwanadam/ya kwako aliipa heshima ya kumwabudu Yeye na kutawala dunia kwa ajili
yake.
Hata hivyo, nafsi iliasi na kujifanyia utaratibu wa kwake, na kutawala
kwa ajili ya kujifurahisha katika vitu hivyo alivyovifanya kwa ajili ya nafsi
ambavyo ingevitumia vema na kumletea Yeye aliyevifanya utukufu. Nafsi hii, katika
uasi huo na upotofu huo kwa madaganyo makuu, ilipotoka hata kumuacha Yeye
aliyeituma, ikaamua kujitia katika ubatili wa kujifurahisha kwa vitu hivi na
kumpa nafasi yeye aliyeasi hapo kwanza yaani ibilisi.
Ni
kweli, suruhu ya haya ilikuwa kuufuta utawala huo na hizo nafsi alizozifanya na
kuzipa heshima ya kutawala kwa ajili yake. Lakini kwa jinsi alivyoipenda hiyo
nafsi kupita kikomo, alivumilia na kutaka kuikomboa, akiingia gharama kila
iitwapo leo ili kuirejesha katika makusudi yake.
Lakini nafsi hii, ifananishwe
na nini? Maana kama ni upotofu ulioiingia basi umeifungia mbali na makusudi ya
Mungu, kwa kuwa katika kuwaza kwake, huwazi tu kujifurahisha na siyo
kujifurahisha katika kumfurahisha Yeye aliyeifanya. Nafsi hii yautumia mwili
uliopewa kuutumia kwa ajili ya Mungu, yautumia katika ubatili na kumsukumia
mbali Mungu, kwa madanganyo na upotofu mkuu.
Lakini
ingekuwa heri sana, kama utayatia moyoni haya, na kujua kuwa, Mungu anataka
nini leo? Je! Si kujinyenyekesha mbele zake, kumpa sifa na heshima na utukufu
anaostahili, kumfanyia ibada ya kicho cha moyo, kwa kutenga kwanza muda wa
kujisongeza mbele zake, ili Yeye naye ahusiane na hii nafsi aliyoifanya? Tena
ajiburudishe moyo wake kwa hiyo nafsi kwa kurejea mbele zake kila wakati, maana
ikiwa aliipenda kiasi cha kuingia gharama kubwa ya ukombozi, si furaha yake
sana aionapo hiyo nafsi ikijihudhulisha mbele zake, kwa kumpa utukufu kwa kuwa
ndio ijala ya kazi yake na makusudi ya hayo.
Basi
sasa, nakusihi katika pendo lake, uyatie haya katika fahamu zako, na nafsi yako
isipotoshwe na mwili wala mfumo wa dunia hii, bali ugeuke na kurejea nyumbani
katika shauli na kusudi lake, yaani kutenga muda wa kujihudhulisha mbele zake,
ukiwa binafsi na katika wengi, kwa kumpa utukufu na ile tu kukaa mbele zake.
Jambo hilo ndilo jambo analolifurahia, na hilo analitaka sana kutoka kwako! Na
kwa kufanya hivyo, atakuwa Mungu kwako katika uhalisia, nawe utakuwa mtu wake,
naye ataisimamia nafasi yake vema, kwa kuwa nawe uatakuwa umejidhihilisha kwake
katika uhalisi. Hapo ndipo utakapovikwa utukufu kama utukufu ule wa mwanzo
aliokukusudia ambao ni mkuu kuliko ule wa malaika.
Heshima
yako itazidishwa katikati ya mbingu na nchi, na vitu vya mbinguni vitamtukuza
Yeye kwa ajili yako, kwa kuwa alikufanya kwa ajili ya huo utukufu uletwao mbele
zake uwe mkuu sana.
Jitafakari
tena na uyapambanue hayo, ili angalau kwa muda udumuo, ufanye jambo la kufaa,
kwa ajili yako na kulitimiza shauli la kuwepo kwako.
Mwisho:
Ikiwa
utahitaji msaada wa mafafanuzi zaidi, nitumie ujumbe au nipigie, nami
nitamuomba huyu aliyetia haya ndani yangu, akupe ufafanuzi huo wa kukufaa zaidi
UTUKUFU UMRUDIE YEYE
ALIYETUFANYA SOTE NA VYOTE
(Ni Siri Kuu)
Mwl;
Goodluck Kazili
Phone: 0765129960
Email: gkazili@yahoo.com