Ni Siri Kuu - The Great Mystery

Ni Siri Kuu - The Great Mystery
"Wakati ule Yesu akajibu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga. Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyopendeza mbele zako.

Jumatatu, 24 Novemba 2014

Goodluck Kazili (KGT-TANZANIA) HEAVEN KINGDOM TEACHING

Alhamisi, 28 Agosti 2014

WAJUA KUWA WE NI MFALME NA KUHANI!

kongamano la Maombi ya Shule na Masomo

Na Goodluck Kazili

UMENUNULIWA NA KUFANYWA KUWA UFALME NA KUHANI KWA MUNGU KATIKA NCHI
 
Si hadithi wala simulizi, bali ni kweli na hakika kuwa Kristo alichinjwa akawanunua watu wa kila kabila , lugha, jamaa, na taifa na akawafanya kuwa ufalme na makuhani wanamiliki juu ya nchi.
Si tu bahati kupata nafasi ya kusoma na kusikia habari hii, bali pia ni neema ya MUNGU kwako, hivyo nakusihi kwa upendo wake Yeye aliyetuumba uzitafakali habari hizi kwa kina nazo zitakufaa na kukusaidia kwa wakati wake.
Kwa msaada wa Roho Mtakatifu nalipenda nikushirikishe habari za nafasi yako kwa MUNGU, katika kanisa, katika nchi/taifa au jamii na familia yako. Si rahisi kujua nafasi yako, lakini imekupasa kuifikiria kwa kuwa hakuna atakayefikri kwa ajiri yako bali ni wewe mwenyewe.
Iko nafasi mhimu na kubwa mbele za MUNGU uliyo nayo, hivyohivyo ulivyo, japo nyumbani wanaweza wakawa wanakudharau na kukuona kuwa si lolote. Lakini mimi leo kama sauti ya MUNGU kwako jijue kuwa una nafasi kubwa na ya heshima mbele za MUNGU. Na nafasi hiyo ni ya mhimu sana kwako . haijalishi una maisha ya dhambi kiasi gani, lakini bado MUNGU ni m,wema kwako, maana maandiko yanasema “Tena zitokazo kwa Yesu Kristo shahidi aliye mwaminifu, mzaliwa wa kwanza wa waliokufa na mkuu wa wafalme wa dunia. "Yeye atupendaye na kutuosha dhambi zetu katika damu yake. Na kutufanya kuwa ufalme na makuhani wa MUNGU, naye ni Baba yake ; utukufu na ukuu una Yeye hata milele na milele amina”. (ufunuo 1:5-6)
Mpendwa katika Kiristo Yesu, nakusihi kwa neema hii; basi ujitahidi kumpenda MUNGU na kutafuta sana kumjua Yeye ili kwa msaada wake maisha yaweze kukamilika. Maana hakuna maana ya maisha pasipo MUNGU mwenye kuyafanya maisha. Na kwa kuwa sisi tuliompokea Kristo tulifanyika kuwa watoto wa MUNGU, basi imetupasa kuyatambua haya ya kuwa yapo kwa ajiri yetu.
Ni mhimu kukumbuka kuwa, jambo lililo jema huja kwa wakati wake, basi hakika hili ni jambo jema. Kwa kuwa kama ungelijua tangu hapo kuwa wewe ni kuhani juu ya nchi katika ufalme wa MUNGU, basi pengine ungekuwa na hatua kubwa. Hata hivyo nakukumbusha kuwa hakuna wakati utakao kuwa mwema kwako zaidi ya wakati huu.
Hivyo nakusihi ufikiri kama mtu mhimu, ambaye anategemewa sehemu nyingi na watu wengi.  Tena maneno haya usiyasahau, elimu ipo ili kukupa maarifa, na kwa kuwa kuna namna mbili, basi ni mhimu kuwa na maarifa ya pande zote, kwa kuwa unaishi pande zote. Ni hatari sana kutokuwa na maarifa juu ya nmna hizi mbili.
Kwa hakika yapo maarifa ya roho na yapo maarifa ya mwili. Maarifa haya yote ni mhimu sana kwako, japo maarifa ya roho yanaonekana kuwa na thamani kubwa. Yanaonekana ya thamani kwa kuwa si wengi wanaobahatika kuyapata, kwa sababu hawayatafuti. Sasa sikushauri wewe ujaribu kutoyatafuta, itakuwa hatari sana. Tafuta maairfa ya roho na haya ya mwili kwa kuwa yote yatakusaidia katika maisha yako yote ya sasa na ya badae, hata baada ya kufa.
Ningeweza kukuandikia mengi, lakini kwa ufupi huu, naomba utafakari sana jinsi unavyowaza na unavyoenenda, je namna hiyo itakusaidia kufika hapo alipokukusudia MUNGU? Ikiwa ni ndiyo MUNGU akutie nguvu katika juhudi hizo, na ikiwa siyo basi MUNGU  akusaidie ili ujitahidi kwa dhati kuubadili mwenendo na mawazo yako. Uyatambue haya kuwa yamekujia kwa wakati sahihi wa wewe kubadilika na kuanza kufikri sawasawa na makusudi ya MUNGU aliyekuumba. Usipoteze muda ni wakati wako maana “ Nao waimba wimbo mpya wakisema wastahili kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua mhuri zake,kwa kuwa ulichinjwa ukamnunulia MUNGU kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa, ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi” ufunuo 5:9-10
Haya ndiyo nalipenda nikushirikishe japo kwa ufupi, MUNGU akubariki .
Goodluck Kazili  0765-129960

SIRAHA MOJA MHIMU YA VITA YA KIROHO



KUHANI GOSPEL TEAM (KGT)TANZANIA)



SIRAHA MHIMU ZA UFALME WA MUNGU

Linapotajwa Neno siraha, kuna kitu kinajengeka ndani yako, na wakati mwingine utapata picha fulani. Hata hivyo suala la siraha lipo ikiwa tu kuna vita au ulinzi au uharibifu. Kama ilivyo katika mwili pia katika ulimwengu wa roho  zipo siraha, na zinamatumizi mbalimbali.

Mpendwa katika Kristo, ni wazi kuwa, siraha hizi za ufalme wa Mungu, ni mhimu kuzijua zote pamoja na matumizi yake, lakini pia umhimu wake.
Waefeso 6:10, inaeleza kuwa tuzidi kuwa hodari katika uweza wa Mungu na nguvu zake, lakini anasema uhodari wetu upo kwa kuzivaa siraha zote za MUNGU. Hapa unagundua kuwa zipo siraha nyingi za MUNGU, na ikiwa zipo nyingi zaidi ya moja kama maandiko yanavyothibitisha, basi ni hakika kuwa, zinatofautiana katika matumizi pia.

MUNGU alipotengeneza siraha tofauti tofauti, alikuwa na maana kubwa, na siraha hizo hutumika kwa wanadamu tu na zipo zitumikazo kwa malaika, ila hatutazungumzia hizo za malaika ila tutazungumzia zilizowekwa kutumiwa na wanadamu au duniani. Kama nilivyoeleza kuwa siraha hizo zinatofautiana kwa namna nyingi.


Mtumiaji wa siraha
Huyu ni mtu mhimu sana kwa kuwa siraha za Mungu zilizotengenezwa kwa ajili ya wana wa ufalme wa MUNGU hapa duniani, haziwezi fanya kazi hadi awepo mtumiaji, na kama mtumiaji atakosa maarifa basi siraha hizo zitafanya kazi kwa kiwango cha maarifa alichonacho mtumiaji.

AINA ZA SIRAHA ZA UFALME WA MUNGU

SIRAHA YA IMANI
Hii ni siraha ya kwanza, si kwa ukubwa ila inayobeba siraha nyingine pia. Kwa mjibu wa waebrania 11:1 imani ni kuwa na hakika), si kitu cha kubahatisha, ila ni uhakika ambao mtu anakuwa nao juu ya jambo Fulani, tena jambo hilo lisiwe la wakati huo ila liwe la wakati ujao na lazima liwe halionekani. Ukisikia kitu kisichoonekana ina maana kuwa kitu hicho ni cha kiroho.

Kwa maana nyingine tunaweza kusema, imani ni namna ya roho inayosimama kama nguvu, siraha, mamlaka, uwezo, uhakika na kuamini, inayotarajia kutekeleza au kutekelezwa kwa jambo fulani. Kwa msingi huo imani si kuamini tu kuwa Mungu anaweza ila ni zaidi ya kumwamini MUNGU.  Mwili una kawaida ya kutokuamini vitu vya rohoni, hivyo wakati mwingine mwili unaweza kukutia moyo kuwa Mungu anaweza kila kitu ila ikifika kwenye tatizo mwili utakuambia hili siyo la kawaida. Lengo la kukuambia hivyo ni ili kukuondoa kwenye imani halisi ya utendaji ambayo ndiyo kubwa.

Kuna imani ya kumwamini Mungu kuwa anaweza, lakini pia kuna imani zaidi ya kumwamini Mungu kuwa anaweza. Ukweli ni kuwa kitendo cha kumwamini Mungu kuwa anaweza ni hatua ya kwanza ya imani, kuishia hapo hakuwezi kusaidia kitu zaidi ya kuwa na tumaini tu, lakini ukitaka kuiona, imani ikifanya kazi yake, lazima kuamini huko ukufanye kuwa kitendo.

Mfano mama hana mtoto, na ameomba na kuhitaji sana kupata mtoto na hajapata, kwa hakika ni kuwa mama huyo anaweza akawa anamwamini Mungu lakini kumwamini Mungu huko hakuwezi kumsaidia asilimia nyingi kupata mtoto, isipokuwa kinachoweza kumsaidia ni pale anapoweza kubadili ile hali ya kuamini, iwe tendo.

Mfano mama anaweza kuamua na kusema, kwa kuwa imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo na ni yale mambo yasiyoonekana, hivyo basi itampasa kuwa na uhakika ndani kuwa, mwakani atakuwa na mtoto na inampasa kufanya maandalizi  kwa kuanza kununua vifaa vyote vya mtoto atakayemzaa, na wakati huo pengine hata mimbabado.  Mungu akiiona imani hiyo hakika lazima amfanyie mama huyo hata kama mpango haukuwepo.

Ukisoma maandiko matakatifu, unagundua kuwa wakati Yesu alipokuwa akiendelea na huduma kati ya vitu alivyokuwa anaangalia ilikuwa imani ya mtu, wakati mwingine hata kama mtu alikuwa hasitahili kutendewa lakini kwa imani yake ilimulazimu Yesu kumfanyia haja yake.

Nakuomba usome kwa umakini mistari hii uione imani jinsi ilivyo na hapa ndipo Roho alipokusudia kukufundishia suala la imani
“(Mathayo 15:22-28), Natazama, mwanamke mkananayo wa mipaka ile akatokea, akampazia sauti akisema, unirehemu, Bwana, mwana wa Daud; binti yangu amepagawa sana na mapepo. 23 Wala Yeye hakumjibu neno. nao wanafunzi wake wakamwendea, wakamwomba, wakisema mwache aende zake; maana anapiga kelele nyuma yetu.  24 Akajibu, akasema, sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.    25 Naye akaja akamsujudia, akasema Bwana, unisaidie. 26 Akajibu, akasema, si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa. 27 Akasema, Ndiyo, Bwana, lakini hata mbwa hula makombo yaangukayo mezani pa bwana zao. 28 Ndipo Yesu akajibu, akamwambia, mama imani yako ni kubwa; na iwe kwako kama utakavyo. Akapona binti yake tangu saa ile”

Sijui umepata kitu gani, lakini kwa kweli huwezi kuielewa imani vema hadi umeyapima mazingira na mazungumzo ya huyu mama na Yesu. Maneno yaliyolazwa ni kauli za mama mkananyo, maneno yaliyokolezwa na hayajalazwa ni ya Yesu mwenyewe na mengine walisema wanafunzi.

 Kama umefuatilia kwa nia ya kuijua imani sawasawa ni kuwa umegundua, yule mama alikuwa na mambo mawili makubwa, kwanza alikuwa na msimamo pili alikuwa na uhakika na anachokiomba majibu yake yapo. Uhakika ulimpa msimamo na msimamo ulimsaidia kulinda imani na kupata alichokuwa anakihitaji.
Jambo la ajabu, ni majibu ya Yesu, mstari wa 26 aliposema kuwa chakula alichonacho ni kwa ajili ya watoto wake na siyo kwa ajili ya mbwa, kwa lugha nyingine alimuita yule mama kuwa ni kama mbwa kwake. Hivi mfano wewe ukamwendea Yesu na kumsihi ukimuomba, halafu akakujibu kuwa ana majibu ya maombi ya watoto wake tu na siyo mbwa; unaweza ukafanyaje. kwa haraka haraka, inaweza ikawa ndio mwanzo na mwisho habari zako na Yesu, maana kama umemwendea kwa kumsihi na ukitegemea atakusaidia halafu bado ni Mungu, lakini anakupa majibu ambayo hata mpagani mwanadamu asingekupa kama umemwendea kwa unyenyekevu kiasi hicho.

Lakini hebu mtazame mama yule kwa unyenyekevu anamkaribia Yesu na kusema “ndiyo Bwana” kisha akajenga hoja asiyoitegemea Yesu, ni kweli mimi ni mubwa na pengine sistahili kula chakula ulichoandalia watoto wako, “ lakini hata mbwa hula makombo yaangukayo mezani pa bwana zao” Yesu alishangaa sana, maneno ya mama huyo yalikuwa na maana hii; kwa kuwa sistahili kula chakula ulichowaandalia watoto wako kwa sababu  mimi ni mbwa wako na siyo mtoto wako, basi uniruhusu tu nile makombo yaliyoanguka mezani pako maana hiyo ni haki yangu kama mbwa wako.

Hii ndiyo imani halisi inayotakiwa kwa watu wa MUNGU, ni wazi kuwa hujawahi kujibiwa kama huyu mama alivyojibiwa na alivyokatishwa tamaa na Yesu mwenyewe, lakini kwa imani yake alisimama akasema nina hakika na ninatarajia kupokea kwa namna yeyote. Na alipojenga msimamo huo Yesu akamtazama akasema Mama imani yako ni kubwa, na iwe kwako kama utakavyo, akapona binti yake tangu saa ile.

Ukisoma kwa kutafakari, na kwa undani unagundua kuwa, Yesu hakumuombea Yule mama juu ya mtoto wake, ila alimwambia iwe kwako kama utakavyo. Hebu fikri kama yule mama angekuwa anataka awe tajiri mimi nakuambia saa ile ile yule mama angekuwa tajiri. Si kwa maombi sana kuwa alipata alichotaka ila kwa imani yake, maana kama ni kuomba aliomba vizuri tena kwa unyenyekevu mkubwa; kama umesoma vema yale maombi ya yule mama yalikuwa ya unyenyekevu sana kuliko ya kwako unayoyaomba, hebu yatazame “akampazia sauti akisema, unirehemu maana yake unihurumie Bwana, mwana wa Daudi, lakini Yesu hakumjibu neno. Wanafunzi walipomtazama yule mama wakamhurumia na wao wakamwendea Yesu wakamsaidia kuomba wakasema mwache aende zake, maana yake mtendee ili aende zake maana anaendelea kupaza sauti. Bado Yesu hakujali maombi ya mama yule hata kwa kubembelezwa na wanafunzi wake, na badala yake akwaambia hakuja kwa ajili ya yule mama ila kwa wana wa Israeli waliopotea. Mama hakurudi nyuma japo kwa maneno hayo ilimtosha kuishi hapohapo, ila ajabu kuu aliendelea pamoja na kwamba Yeye hata kujibiwa hakujibiwa, ila wanafunzi walimsaidia ili angalau ajibiwe, bado anajibiwa kuwa Yesu hakuja kwa ajili yake. kwa hiyo ilimaanisha kuwa asitegemee kuwa anaweza kutendewa chochote kama anavyoomba, kama ni kuondoka aondoke tu. Yule mama baada ya kuambiwa hivyo akasogea akamsujudu, kuonesha kuwa hata kama hukuja kwa ajili yangu ila mimi nakuamini, alipomsujudu akaomba tena akisema, Bwana unisaidie. Baada ya Yesu kuona huyu mama anang’ang’ania akasema maneno magumu sana ambayo sasa yule mama kama si imani kubwa aliyokuwa nayo angekufulu palepale.

Swali langu kwako ni hili; huyu mama ana utofauti gani na wewe? Je Yeye hakuwa mwanadamu kama wewe? Je Yeye hakuwa na haja kama wewe ulivyo na haja? Na je umewahi kuomba ukakatishwa taamaa angalau robo ya huyu mama? Umewahi kujibiwa majibu kama alivyojibiwa huyu mama?. kwa kujiuliza hivyo, angalia imani yako, utagundua huna imani, na ndicho chanzo cha kutokupata kile unachotakana kuomba.

Hebu ngoja nikuambie jambo moja hapa la ajabu ili uone imani inavyofanya kazi kwa mhitaji lakini pia kwa yule anayeombea. Mathayo 17:14-16 inaeleza kisa kimoja, “Nao walipoufikia mkutano, mtu mmoja akamjia, akampigia magoti akisema. Bwana umurehemu mwanangu, kwa kuwa anakifafa, na kuteswa vibaya; maana mara nyingi huanguka motoni, na mara nyingi majini. Nikamlete kwa wanafunzi wako, wasiweze kumponya.” Ukiendelea kusoma unaona Yesu akichukia kwa ajili ya yule mtu, na juu ya wanafunzi wa Yesu kwa kuwa hawakuwa na imani. Ila alipomaliza kuwasema aliamuru wamlete kwake kisha akakemea yule pepo akamtoka yule mtoto.  Wanafunzi wake walipoona hivyo, hawakulidhika wakamwendea  mstari wa 19 “kisha wale wanafunzi wakamwende Yesu kwa faragha wakasema mbona sisi hatukuweza kumtoa? 20 Yesu akawaambia, kwa sababu ya upungufu wa imani yenu, kwa maana, amini, nawaambia, mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali, mtauambia mlima huu, ondoka hapa uende kule, nao utaondoka; wala hakutakuwa neno lisilowezekana kwenu”

Naamini umeona kazi ya imani na jinsi imani ilivyo, ila ukisoma sehemu nyingine wanafunzi walipoambiwa hivyo waliomba waongezewe imani ndipo Yesu akawaambi mngelikuwa na imani hata chembe ya haradali , kwa maana kuwa hawakuwa na imani hata ndogo japo walikuwa ni wanafunzi wa Yesu na walikuwa wanamwamini Yesu. Hapo unagundua kuwa imani ni zaidi ya kumwamini Yesu, lakini pia amesema  hakutakuwa na neno lisilowezekana kwenu. Unafikri kwa nini mambo mengi hayawezekani kwako, ni kwa sababu huna imani japo unamwamini Mungu. Ni wazi kuwa ungekuwa unaweza ungeniuliza swali sasa hiyo imani ya zaidi ya kumwamini Mungu iko je? na ndio unafanya je?. Roho mtakatifu alijua kuwa utahitaji kujua na ameweka majibu ya maswali yako hapa chini. Ila nakusihi sana isiwe tu kusoma na kuelewa bali iwe kusoma na kutenda hicho unachogundua na kukielewa.

Ukisoma hapo kwenye mathayo 17 lakini mstari wa 21 umetoa majibu. “ lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kuomba” hapo humaanisha kuwa namana hiyo ya imani inayoweza kutoa nguvu za namna hiyo haiwezekani isipokuwa kwa kufunga na kuomba. Maana yake ni kuwa kuna kiwango cha imani unachoweza kukipata kwa kuamini na kufanya kile unachokiamini kiwe hakika na kutenda vile unavyoaamini, lakini kiwango halisi cha imani hupatikana kwa kufunga na kuomba.
Hii ni kwa sababu mwanadamu ana namna ya mwili sana kuliko namna ya roho na kwa kweli hakuna mahali popota ambapo mwili unakubali na kumruhusu mtu kuwa na imani hasa ya utendaji, hivyo kufunga maana yake ni kuutiisha mwili ili kupandisha ile nafasi ya roho, hivyo kumfanya mtu kuwa na hali ya roho kuliko ya mwili. Pia kufunga huko kunaudhoofisha mwili ambako kudhoofika huko huifanya roho kuwa na nguvu.

Pia kuomba hutifua au hunyanyu hali ya roho, au hunyanyua hali ya kimungu ndani ya mtu, na hupunguza kasi ya mwili kufikri kimwili na kuifanya akili ikae kwa namna ya roho ambapo ni rahisi sana kuwa na imani na kuona kuwa kila kitu kinawezekana kwa Mungu, na kwa kuwa unakuwa kwa namna ya roho zaidi utasikia msukumo ambao unakusukuma kufanya kile unachokiamini na unapofanya kwa kuwa unafanya kwa uhakika lazima kitokee.

Mpendwa katika Kristo, siraha ya imani ni siraha kubwa sana, na wakati mwingine imekupasa kufanya mazoezi ya imani, hata pale ambapo watu wote wanaona ni ngumu, wewe unawaambia inawezekana, pale akili yako inapokuambia hapa ni ngumu unalazimisha ikubali kuwa inawezekana hata kama kwa jinsi ya kawaida haiwezekani.

Kikubwa jitahidi kuamini, na kufanya kile unachokiamini kiwe kweli, yaani kama unaamini Mungu anaweza katika jambo Fulani weka uhakika, na kisha lifanye ikiwa unomba uambiwe omba ukijua nikimaliza kuomba nitakuwa nimepokea, na ukimaliza hata kama hujaona majibu anza kujiaminisha kuwa umepokea taratibu taratibu utaanza kusikia amani moyoni na kuona lile jambo likikamilika.

Mungu wa mbinguni akujalie kujua vema siraha za ufalme wake ili uwe askari mwema na mtetezi wa wokovu wako na kuujenga mwili wa Kristo. Hata hivyo ujue kuwa ziko siraha nyingine kama siraha ya Neno, Siraha ya Maombi, Siraha ya Wokovu. Hizo ndizo siraha kuu za ufalme wa Mungu. Na hata siraha hiyo ya imani imeelezwa kwa ufupi hivyo endelea kusoma kwenye maanidiko juu ya imani na vitabu vya Neno la Mungu, semina, mikutano, na zaidi shuhuda mbalimbali. Maana imani chanzo chake ni kusikia ambako huja kwa Neno la Kristo. Mungu wa mbinguni akujalie mema yote.

“mjue sana Mungu ili uwe na amani”

Mwl: Goodluck Kazili

Ijumaa, 4 Julai 2014

KARIBU UTUMIKE NASI- KUHANI GOSPEL TEAM (KGT)

Karibu Katika Huduma ya KGT (Kuhani Gospel Team) Tanzania.

Ijumaa, 2 Mei 2014

SOMO LA KUJUA MISING YA NCHI NA NAMNA YA KUOMBA




KONGAMANO LA 8 LA MAOMBI YA TAIFA TANZANIA 2013

MADA: KUOMBA TOBA NA UPATANISHO KWA AJIRI YA SELIKARI ILI KUPATA 
              KIBARI NA  KUWA NA UHUSIANO WA KUDUMU MBELE ZA MUNGU

Daniel 9:1-27


MUHIMU KUHUSU MADA ILIYOTANGULIA:

Mada ilikuwa: "KUJENGA NAFASI HALISI YA KANISA KATIKA NCHI"
Katika mada hii, tuliangalia na kuomba juu ya lango la kanisa kuwa imara katika nchi. Tuliomba toba juu ya kuhusuriwa Kwa lango hilo, tukaomba kuimarishwa kwa lango hilo, tukaomba kutumiwa vema na Mungu ili kufanya mapenzi yake, tukaomba juu ya kuchukua wajibu wake wa kuiongoza selikali katika njia bora ya kiMungu. Tulikuwa na mfululizo wa makongamano 3 ya kuombea kanisa, ambapo tulianza terehe 10/4/2012 na kukamilisha 15/12/2012.
Wakati huu tumepewa “kuomba toba na upatanisho kwa ajiri ya selikari ili kupata kibari na kuwa na uhusiano wa kudumu mbele za mungu”. eneo hili tutajifunza yale ambayo Mungu anataka tuyajue juu ya nafasi Yake katika selikali, pamoja na nafasi ya selikali mbele za Mungu, na wajibu wa kanisa katika selikali.

DONDOO
Nafasi ya selikari mbele za Mungu
Nafasi ya Mungu katika selikari
Wajibu wa kanisa katika selikali mbele za Mungu

UTANGULIZI:
Ni jambo la mhimu sana katika nchi, kuwa na mtazamo chanya juu ya misingi ya nchi na uwepo wake katika dunia inayoonekana na ile isiyoonekana yaani ulimwengu wa roho. Imani yangu ni kuwa unajua  kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama, bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho, Waefeso 6:13”. Misingi ya nchi yoyote hujengwa katika ulimwengu wa roho kwanza kabla ya kujengwa upande wa mwili. Ni wazi kuwa, kwa kuwa kuna falme, mamlaka na jeshi la pepo wabaya katika maeneo haya haya ya dunia, swali la kujiuliza ni hili, je huo ufalme, mamlaka na jeshi la pepo linafanya kazi juu ya nani au jeshi hilo linamrinda nani na lipo kwa ajili ya kupigana na nani?

Ni hakika kuwa ulimwengu huu ni mwendelezo wa ulimwengu wa roho, ambapo mfumo na namna unavyoongozwa inafanana kwa sehemu kubwa na ile ya ulimwengu wa roho, ndio maana huwa kuna kuathiliana kati ya watu wa dunia yaani wa mwili na wale wa roho. Hata hivyo tunajua kuwa yako madaraja kadhaa yanayoikamilisha dunia kwa upande wa watu. Kwa mfano kuna mtu, familia, ukoo,kijiji,kata, tarafa,wilaya, mkoa, kanda, taifa, bara,dunia. Madaraja haya huadhili au kuathiliwa kuanzia mtu hadi dunia. Athali haiwezi kutokea ambayo chanzo chake itakuwa nchi, bali kwa mtu au familia/kundi dogo linaweza kuvuluga hali ya nchi, pia mtu au familia/kundi dogo linaweza kuiweka nchi katika hali njema, hata maandiko yanathibitisha “ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao, 2 Nyakati 7:14”.

Karibu Usome na Kujifunza, Roho Mtakatifu yuko tayari kukusadia vema; Amina
UFAHAMU JUU YA NCHI/TAIFA LA TANZANIA
Hadi sasa Tanzania ina miaka 51, lakini Tanganyika ina kadiliwa kuwa na miaka 10,000 tangu watu waanze kuishi, kwa ushahidi wa kiakilojia. Hatuwezi kutazama hali ya nchi kwa kuitazama miaka hiyo 51, bali tunatakiwa kutazama tangu kuwepo kwa aridhi ya Tanzania, na pale watu walipoanza kuishi.
Japo ni vigumu sana kupata histori, lakini kujua ukweli kwa namna ya roho inawezekana kwa kuwa kisichokuwepo ni ushahidi wa kimwili, ila ushahidi wa mambo ya roho upo, “kwa maana twajua torati asili yake ni ya rohoni-Warumi 7:14a”.

Wakati Mungu anaiumba dunia, Tanganyika iliyozaa Tanzania aliiumba, na kusudi lile lile tunalolisoma kwenye Maandiko la Mungu kuiumba dunia ndilo kusudi la Mungu kuiweka Tanganyika-Tanzania, (tunatumia Tanganyika kwa kuwa ndiyo asili, kwa kuwa Tanzania imepatikana kisiasa, yaani baada ya kuungana na Zanzibar). Na kwa kuwa kila jambo analolifanya Mungu huwa na maana kubwa, basi uwepo wa Tanganyika una maana sana kwetu tuliowatanganyika na wazanzibari,  kwanza mbele yetu wenyewe, mataifa mengine na mbele za Mungu mwenyewe aliyetuweka.
Nchi yetu iliumbwa kwa ajiri ya Mungu, nasi tukawekwa ili kutawala, nchi hii ni mali ya Mungu, kwa kuwa dunia na vyote viijazavyo ni mali ya Mungu. Hata hivyo sisi tunaoishi humu, tumepewa kazi moja kuu, kuitawala nchi na kila kilicho ndani na juu ya nchi kwa maana ya kilicho aridhini na kilichoko juu ya aridhi “Mwanzo 1:26-31”.
Hivyo ni mhimu kukumbuka kuwa kusudi la Mungu juu ya Tanzania halijakuwepo kuanzia mwaka 1961-64, bali lilikuwepo tangu ilipowekwa misingi ya dunia. Na kwa kuwa kusudi la Mungu ilikuwa kuwa na utawala mwingine wa namna ya mwili huku duniani, na ikampendeza kuiweka Tanganyika, basi ni mhimu kulitazama kusudi hilo ili kuijua Tanzania na mstakabali wake katika misingi ya roho na mwili.

Tanganyika iliumbwa kama nchi na wala siyo taifa, kwa kuwa hakuna mahali palipoumbwa kama taifa, na tukishataja suala la nchi basi tunagusa lasiri mali, kwa kuwa nchi ni aridhi. Na kusudi la Mungu haliko kwa watu wa Tanzania, bali kwa nchi ya Tanzania, kwa kuwa angeweza kuzaliwa yeyote Tanzania, na kama kusudi lingekuwa kwa watu, basi tusingetawaliwa na kuongozwa kwa muda wa miaka zaidi ya 85,(wakati wa ukoloni) ambao ni umri unaoizidi Tanzania, lakini bado mambo yaliyofanyika yana maana kubwa katika kukamilisha kusudi la Mungu juu ya nchi.

Nchi hukamilika inapokaliwa na watu, na hapo ndipo kusudi la Mungu hukamilika. Kwa kuwa ukamilisho wa kusudi la Mungu ni pale nchi inapokawaliwa na watu, na kutawala kwa misingi ya Mungu.
Tanzania ina  eneo lenye ukubwa wa kilomita za muraba laki tisa elfu arobaini na tano na mia mbili na tatu (945,203), ni nchi ya 31 kwa ukubwa wa eneo, katika eneo hilo aridhi ni asilimia 93.8 katika 100, na eneo la maji ni asilimia 6.2 ya jumla ya eneo lote. Idadi ya watu kwa mujibu wa sense zilizowahi kufanyika sense ya kwanza mwaka wa 1967= milioni 12 laki 3 elfu 13 mia 469,( 12,313,469) sense ya pili mwaka wa 1978= milioni 17 laki 5 elfu 12 mia 610,(17,512,610) sense ya tatu mwaka wa 1988= milioni 23 elfu 95 mia 885 (23,095,885) sense ya nne mwaka wa 2002= milioni 34 laki 4 elfu 43 mia 603 (34,443,603).
Sense ya tano ya 2012 inakadiliwa kuwa na watu milioni 45,798,475, kadilio la miaka ijayo, kufikia mwaka  2020 inakadiliwa kuwa  57, 102,896. Kwa idadi hiyo inaonesha kuwa nchi ya 30 kwa idadi ya watu. Kwa kila eneo la kilomita mbili linakaliwa na watu 46, msongamano huu, unaiweka kuwa nchi ya 124 kwa msongamano wa watu, ndio nchi kubwa zaidi Afrika ya Mashariki.

Tanzani inajulikana kama nchi masikini sana Duniani, katika viwango vya kimataifa, japo katika uhalisia Tanzania si nchi masikini, bali ni Taifa masikini. Kwa maana utajiri ulio kwenye aridhi ya Tanzania ni zaidi ya utajiri ulio kwenye mataifa yanayohesabika kuwa nchi tajiri.
Kabla ya ukoloni hatukuwa na taifa la Tanzania, wala Tanganyika, isipokuwa kulikuwa na koo, pamoja na makabila mbalimbali yaliyokuwa na utawala wao, hivyo hatukuwa na jamii moja ya  Tanganyika wala Tanzania kwa kuwa haikuwepo mipaka halisi ya nchi kiutawala. Mnamo mwaka wa 1884, katika nchi ya ujerumani iliyoko uraya, ulifanyika mkutano wa kuigawa afrikana ili kuiweka chini ya utawala (ukoloni). Wakati huo ndipo mipaka ilipochorwa na Tanganyika ikawa taifa na nchi yenye mipaka halisi, iliyotambuliwa na umoja wa mataifa baadae. Wakati huo ndio ulikuwa mwanzo wa kuja kwa habari za Kristo, kwa njia ya umisheni, ulikuwa unafanywa na wazungu. Hata hivyo, jamb  la kuleta habari njema kama maandiko yalivyokuwa yametangulia kusema, bado ilionekana kuwa ni tatizo kwa kuwa ilihusisha masuala ya utawala wa kinyonyaji yaani ukoloni.

NAFASI YA SELIKARI MBELE ZA MUNGU
Selikari kwa maana ya utawala, ni chombo kilichowekwa/kinachowekwa na Mungu kwa kusudi la kusimamia/kuhudumia watu wake katika mambo yote ya mwili. Selikali siyo mtu bali ni mamlaka(authority) ambayo ipo kwa ajiri ya kutekeleza mambo makuu matatu. Kujenga uchumi imara kwa watu wake, kuwa na siasa safi, na kutoa huduma zote za kijamii

KUJENGA UCHUMI IMARA:
Uchumi wa nchi na watu wake anayehusika kuujenga ni selikali, hili ni jambo moja mhimu linalotambulisha utendaji wa selikali (mamlaka). Japo kuna vitu ambavyo huisaidia selikali kujenga uchumi imara kwa watu, hata hivyo vitu vyote ni wajibu wa selikali kuwa navyo, isipokuwa tu maliasili ambazo ziko nje ya uwezo wa mwanadamu. Uchumi wa nchi uko kwenye nchi, ikimaanisha kuwa uchumi wan chi uko kwenye aridhi. Lakini hatuwezi kutaja uchumi bila watu. 

Maana  ya uchumi, ni kuzalisha na kutumia lasilimari zilizoko ili kukidhi mahitaji yaliyopo, lasilimari hizo ni kama zile za asili na zisizo za asili, lakini hata hivyo zisizo za asili hutokana na zile za asili.

UFAHAMU WA KIROHO JUU YA UCHUMI
Hapo mwanzo hapakuwepo na uchumi, kama tuuonavyo leo, lakini mara ya kwanza kabisa Mungu alimwagiza Adamu kuilima aridhi na kuitunza, huo ulikuwa mwanzo wa uchumi katika kitabu cha “Mwanzo 1:28-31”. Pia watoto wa Adamu, Kaini na Habiri, walikuwa wakifanya kazi zilizotambulisha nafasi yao na uchumi wao.
Dhambi inaonekana kuwa tatizo la uchumi, kama vile lilivyo tatizo la uzima wa milele “Mwanzo 3:17” dhambi iliathili aridhi, na hauwezi kuwa na uchumi bila kuwa na aridhi ukiwa kama taifa au nchi. Wakati Mungu alipoilaani aridhi, kwa sababu ya dhambi ilikuwa na tafsiri ya kuulaani uchumi, kwa kuwa maisha ya mtu kwenye mwili yalitegemea sana ardhi Akamwambia Adamu, kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajiri yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako, michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni; kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia aridhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa;  kwa maana u mavumbi wewe nawe mavumbini utarudi. Laana hii vipengele vyake vyote vinagusa uchumi tu, kwa kuwa kipengele cha kifo hakikuwa laana bali yalikuwa matokeo ya kuvunja sheria, na aliambiwa mapema kuwa akila hayo matunda hakika atakufa.
Dhambi iliharibu suala la uchumi, kuwepo kwa dhambi kulifanya suala la uchimi kuwa tatizo, kwa maana ya kuwa ilifanya mtu ahangaike ili kuwa na uchumi mzuri, hali njema ya uchumi tunayoiona kwa baadhi ya watu, na kwa baadhi ya nchi/mataifa, ni kidogo sana ukilinganisha na ilivyokuwa imekusudiwa, kabla ya dhambi kuvuruga.

Lakini hata hivyo, kwa maana halisi ya uchumi tuijuayo leo, inaonesha kuwa uchumi uliletwa na dhambi, maana ya sasa ya uchumi “ ni kutumia malighafi zisizotosheleza ili kukidhi mahitaji ya mwanadamu” hivyo kama kuna utoshelevu basi suala la uchumi tusingekuwa nalo, lakini kwa sababu ya upungufu uliopo, tunalazimika kuwa na wazo la kusuruhisha tatizo na kuzalisha na kutumia lasilimali kidogo zilizopo ili kutimiza mahitaji yaliyoko, Na tunajua kuwa bila dhambi huo upungufu usingekuwepo.
Adamu ni mzaliwa wa kwanza, nje ya nafasi ya Yesu, na kwa kuwa yeye ni lango la wanadamu wote na mataifa yote, hivyo wote huhesabiwa kuwa wametenda dhambi ileile aliyoitenda Adamu. Jambo hili ni kwa sababu ya, kila mtu hupita kwenye lango lilelile la Adamu, hivyo kinachosababisha tuhesabiwe kuwa tumetenda dhambi si kutenda dhambi kwenyewe bali mahali tunapopita  na kutokea tunapokuja duniani ndipo panapofanya tuhesabiwe dhambi.

Baraka kuu ya hapa duniani ni uchumi imara, wala siyo wokovu, kwa kuwa wokovu haupo kama Baraka, bali ni neema ambayo ipo kwa kila mtu. Lakini suala la uchumi si neema ambayo imewekwa kwa kila mtu, bali ni maarifa, ujuzi na ufahamu wa namna ya kuujenga ili uwe imara, ndicho kigezo kikuu. Ukisoma maandiko, kuanzia kitabu cha mwanzo, habari za Ibrahimu hadi kufika kwenye agano jipya, mafundisho na Baraka zilizoamriwa nyingi ni za uchumi, hata hivyo agano la kale lote lemetaja Baraka kuu mbili, nayo ni ya uchumi na afya tu. Agano jipya limetaja wokovu pekee kwa wingi sana na msisitizo uko kwanye wokovu  uletao uzima.

Mfano Mungu alimuahidi ibrahimu kumrithisha kizazi chake nchi ya kanani, ambayo imejaa maziwa na asali, lakini ni ukweli kuwa nchi ya kanaani haina hivyo vitu kwa kiwango tunachosoma kwenye maandiko, hii ni kwa sababu kilichokuwa kinaelezwa ilikuwa zaidi ya maziwa haya tuyajuayo kwa jinsi ya mwili. Kwa kuwa lugha ya roho huweza kutumia kitu kiletacho taswira tu kwenye ulimwengu wa mwili, kwa mfano Mungu alipozungumza suala la maziwa, ni hakika kuwa alitaja vitu vyote vijulikanavyo kuwa bora na hasa vyakula, pia ilipotajwa asali ilimaanisha vitu vyote vilivyo vitamu kwa aina yake kuwa vitakuwa vimejaa katika nchi ya Kanaani.

Hata hivyo kuna uhalisia wa sasa katika vitu hivyo vilivyotajwa katika nchi ya Kanaani ambayo sasa ni Israel. Kwa maelezo haya bado inaonesha kuwa jambo kubwa lilikuwa la uchumi, hata kilichosababisha wao kwenda Misri ilikuwa haja ya uchumi na hata kilichowakwamisha kutokutoka Misri ni uchumi uliokuwa umeunganisha na miungu ya misri.
Ukisoma  maandiko kwenye agano la kale hakuna mahali ambapo uzima  wa milele umetajwa, kama tuujuavyo leo, hata kwa wale waliopata kuelewa, walichojua kuwa wakisha kufa watalala pamoja na ndugu zao, wala hapakuwa na ufahamu juu ya siku ya mwisho, hadi kufikia wakati wa nabii Amosi karibu mwaka 750 K.k.

Amri 10 za Mungu na sheri zaidi ya 420 walizopewa wana wa Israel, karibu zote zilikuwa zinagusa hali ya uchumi wao. Hii ina maana kuwa zilikuwa za kujenga uhusiano mwema na Mungu ambapo matokeo yake ilikuwa kupata uchumi mzuri pamoja na afya, tofauti na sasa ambapo matokeo makubwa ni uzima wa milele.
Ukiangalia vema, utagundua kuwa, walipovuja sheria hizo, hali yao ya uchumi na afya ilileta shida, kwa maana ya kuwa uhusiano wao na Mungu ulipokuwa mubaya, basi matokeo yalikuwa kwenye uchumi na afya zao. Na hapa utagundua kuwa , suala la dhambi haliachani na uchimi pamoja na afya ya mtu. Baraka za afya na uchumi zimetajwa kwenye “Kumbukumbu la torati 28:1….”
Uchumi wa mtu, una misingi yake katika roho au una mlango wake  ambao hujulikana kama agano, hutofautiana na ngazi ya Taifa japo taifa na uchumi wake huanzia kwa mtu, mwisho huwa kuna uchumi wa mataifa. Ni mhimu kuelewa mgawanyo huu wa makundi matatu yanayopokea uchumi kutokana na mfumo wa ulimwengu wa roho.

Kwenye ulimwengu wa roho, uchumi hukaa ndani ya mtu, ila kuna muda unaoamriwa juu ya mtu huyo na uchumi ulio juu au ndani yake. Hata hivyo majira yapo kwa kila mtu kulingana na uhusiano wake ulivyo katiaka ulimwengu wa roho. Mfano, ndoto ya Farao“Mwanzo 41:1….”  Haikuwa inagusa uchumi wa misri pekee bali hata ule wa kanaani. Lakini kilichofanyika ni kuwa Farao alikuwa na  uchumi ndani yake, lakini Baraka yake ilikuwa Kanaani ambyo ilikuwa ndani ya Yusufu. Yusufu alikuwa na maarifa juu yauchumi, pia alikuwa na Baraka ya uchumi, ndio maana alipoingia kwa Potifa, maandiko yanasema Mungu alimfanikisha Potifa mambo yake kwa mkono wa Yusufu. Lakini Yusufu mwenyewe hakuwa na uchumi, ila akifika mahali penye uchumi basi Baraka yake ilikuwa inauchanua ule uchumi.

Jambo hili ni mhimu sana kwa kuwa wako watumishi wengi ambao wana Baraka za uchumi, lakin wao hawana uchumi, si ajabu mtu kumuombea awe na uchumi imara, na akafanikiwa kwa maombi na namna alizopewa na mtumishi huyo, lakini unaweza kumkuta mtumishi huyo ana hali mbaya. Kwa hili kinachofanyika Mungu anamuunganisha na watu wenye uchumi, ili Yeye aachilie Baraka yake na atakapofanikiwa basi haitakuwa kwa ajiri ya huyo mtu peke yake bali pia itakuwa kwa ajiri ya huyo mtumishi.
Mali zilizopatikana baada ya Yusufu kuingia misri zilikuwa kwa ajiri ya misri na watu wa nyumbani mwa Yusufu. Hata katika habari ya watumishi waliowekwa na Mungu kuwahudumia watu katika Israeli, Mungu aliweka utaratibu huu, Kiongozi alipewa Baraka, ambazo akiziachilia kwako, unafanikiwa katika mambo yako, ambapo sasa itakubidi kuchukua sehemu ya mafanikio yako na umpe huyo kiongozi/mtumishi, na huo ndio ujira wa Mungu katika Baraka anazozitoa.

Mfano mwingine, nabii Eliya wakati wa njaa, alimtaka Yule mwanamke amtengenezee mikate, lakini Yule mama alitaka kulalamika kwa kuwa alikuwa ameishiwa, Eliya akamshrutisha amalizie unga huo uliobaki, baada ya mama Yule kufanya Kama alivyoagizwa, matokeo yake ilikuwa kupata chakula tele,Kwa kuwa chombo kile kilijazwa mara dufu. Hapa tunaomna kuwa Eliya alikuwa Na Baraka, Ni mhimu kujua mahali ambapo au mtu ambaye ana Baraka zako, Kama marekani walivyogundua kuwa Baraka yao iko Israeli, wakafanya kuwafadhili na kuwatunza kwa uwezo wao wote na sasa ndio nchi pekee yenye uchumi imara duniani.

Uchumi wa Taifa

Uchumi huu wa taifa huwa na msingi wa mtu/familia, uchumi huu una misingi ya kwenye aridhi na kisha humalizikia kwa watu. Mfano Israeli walikuwa wakitembea Na Baraka za uchumi, hivyo nchi ya kanaani haikuwa na Baraka hiyo wasipokmuwepo wana wa Israel, ndio maana hata kama mtu ataitumia ile aridhi, haitatoa mazao, lakini ikitumiwa na mtu wa uzao wa Israel hutoa mazao sana.
Uchumi wa dunia
Ni uchumi ambao chanzo chake huanzia kwenye mtu/familia kasha huja taifa ndipo tunapopata uchumi wa dunia, uchumi huu hutegemea Baraka zilizoko kwenye mataifa. Mfano halisi ni Baraka aliyopewa Ibrahimu juu ya mataifa, “Mwanzo 22:18”, alifanya agano na Mungu lililokuwa linagusa maisha ya uzao wake na mataifa. Wakati ibrahimu alipewa haki ya kuwa Baraka kwa uzao wake na mataifa, Daudi alipewa ufalme Isaya 11:1, wakati Yakobo alipewa haki ya taifa, ndio maana hadi leo tuna taifa la Israel ambalo ni jina lake.
Kwa maelezo haya yanaonesha wazi kuwa Israel kama taifa na nchi ina dhamana kubwa katika uchumi, utawala na taifa katika dunia.

Tangu hapo mwanzo Mungu alipoilani aridhi, hakukuwa kana namana ya kusitawi uchumi mpaka kwa Baraka maalumu, na jambo hili lilianza kwa Ibrahimu, na Mungu aliunganisha hali ya mafanikio ya watu na mataifa kwa Ibrahimu, “Na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia; kwa sababu umeitii sauti yangu Mwanzo 23:18”.  Na katika ukweli huu, unagundua kuwa hakuna taifa lisilomkiri Ibrahimu ua Yesu kwa aganola Ibrahimu lenye uchumi imara. Hata hivyo yako mengine yawezayo kutokea ili kukamulisha maandiko yanayotaja siku za mwisho, ambapo wale wasio wa Kristo watapata nguvu za Kiuchumi, na kuitawala dunia. Mafano mataifa yanayoanza kupata nguvu nje ya kumkubali Kiristo ni moja ya alama ya kutimiza ufunuo huu.

Wakati Yesu alipokuja duniani, kulifanyika mabadiliko ya aina tata
Uchumi, ufalme ambapo ndani yake tunapata wokovu, na taifa. Na katika kuutazama ukweli huu utagundua kuwa kabla ya Yesu kuzaliwa mataifa/falme zilizokuwa zinatawala dunia hakuna inayojulikana kwa sasa, kwa kuwa yalitokea mabadiliko makubwa sana kwenye maeneo hayo matatu mhimu katika dunia. Mfano, falme kama z aroma, uyunani na uajemi, babeli, zilizokuja kufuatiwa na Iraq hazina nguvu hata kidogo. Ujio wa Yesu ulifunga mlango wa ustawi ambapo ilikuwa tangu kwa Adamu, Wakati huo Yesu alichukua hiyo nafasi akafanyika kuwa mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote wa walio hai na walio kufa.
Utagundua kuwa nchi karibu zote zina mafanikio yatokanayo na misingi ya Kiroho, mfano nji ya malekani ina mafanikio makubwa kwa sababu ya Israel, hata  ulaya pia ina mafanikio kwa sababu ya kumabariki ibrahimu, na wakati wanapopunguzi zile Baraka hata uchumi wao unayumba, na marekani kwa kuwa anajua hili, ndiye aliyebaki na msimamo juu ya Israeli na ikiwa atalegeza msimamo wake basi huu ndio utakuwa mwisho wa kustawi kwake, amtaifa yaliyobaki nai yale yanayoembea kwa Baraka za ishimael kwa kuwa naye alipewa Baraka hizo japo hazikuwa kubwa kama za Isaka. Mfano mataifa ya uarabuni yote yanauchumi unaoelekeana na Baraka za Ishimaeli, na ndio maana hawawezi kuwa sawa na mataifa mengine yasiyo kuwa na Baraka hizo wala walio chini ya Isaka mwanzo  21:8….”
 
Hivyo ugonvi wa mataifa yanayopokea Baraka kupitia kwa ibrahimu, nay ale ya Ishimaeli hayako kwenye uchumi ila yako kwenye ufalme. Kwa kuwa tofauti za imani, hazina uhusiano na uchumi ila ni mambo ya kifalme au utawala, hivyo unagundua kuwa lango la Ibrahimu kwa upande wa uchumi ni kubwa,na ndio msisitizo mkubwa ulio kwenye agano, msisitizo wa agano jipya upo kwenye ufalme- uzima wa milele.
Hapa unakumbuka kuwa matazamo wa watu waliookoka na kushika tu agano jipya, huzingatia na msisitizo wao uko kwenye habari za ufale-uzima wa milele, sualala uchimi hawahangaiki nalo,  lakini Mungu aliviweka vyote kwa maana nzuri sana, kwa kuwa wokovu ni kwa ajiri ya roho, uchumi ni kwa ajiri ya mwili. Na kwa kuwa hapo mwanzo kwenye agano la kale msisitzo war oho haukuwepo sana zaidi ulikuwa wa mwili, ndio maana Baraka zote ambazo zimetajwa kwenye maandiko zinahusu uchumi na afya tu, wakati wa agano jipya  msismitizo ulikuwa kwenye roho, mwili umeonekana kuwa adui, ndio maana ukisoma barua za Paulo, amezunguzia sana kuwa mwlil ni Adui Warumi  sura ya 6 hadi ya 8. Pia kwenye Mathayo 6:31 “bali utafuteni kwanza ufalme wake(mbinguni) nahaki yake; na hayo yte mtazidishiwa”

Wapo waonao kuwa ni bora kuwa na uchimi kwanza kasha wokovu ndipo ufuate, wakiamini kuwa usipokuwa na uchumi bsi hata suala la wokovu litakusumbua. Na wengine wanaona bora kuwa na wokovu kwanza kwa kuwa huo uchumi hata ukiukosa bado una tumaini la uzima wa milele. Lakini tukiyatazama hayo maneno ya Yesu, yanatupa uhakika kuwa ndani ya ufalme kua uchimi pia , kwa kuwa aliposema na mengine mtazidishiwa alimaanisha na  uchumi. Lakini p[ia katika mfano alioutoa wa lazalo, unaonesha kluwa unaweza kuwa na uzima bado uchumi usiwe nao wakati uwapo duniani, pia  unaweza kuwa na uchumi lakini uzima usiwe nao.
Hata hivyo suala la wokovu na uchimi kwa nchi zinazoendelea, bado ni changamoto kubwa, kwa kuwa hata sehemu kubwa ya mahubiri na mafundisho yao yanahusu uchumi, na muujiza wao mkubwa ni wa uchumi na afya. Hata hivyo ukweli wa mambo ni kuwa wengi wao maarifa ya uchumi hawana lakin suala la uzima na afya kwa ujumla lina kipaumbele sana. Mafano kama utasikia tangazo la mkutano wa injili kwa hakika vittajwa vitu viwili, yaani wokovu na uponyaji wa magonjwa, hii ni kwa sababu mafanikio katika uchumi ni kidogo sana hata katika sala zao, angalau kuna mafanikio katika maombi ya magonjwa japo hata hivyo wengi wao wamekuwa wakihusianisha na nguvu za giza. Lakini hapo yako matabaka mawili, kuna wale waishio mjini na hasa angalau wenye mafanikio ya kiuchumi, ambao ni daraja la wafanyabiashara, wasomi, wafanya kazi, hawa wao hupendelea mahubiri na mafundisho yanayohusu habari za uchumi, mfanokatika wanafunzi wengi wao hupenda mafundisho na mahubiri yanayowapa msaada wa namana ya kufanikiwa katika masomo na uchumi kwa ujumla, habari za wokovu na maarifa ya roho kwao ni changamoto.
Kwa ngazi ya taifa, ni kweli kuwa kila taifa linakipaumbele chake katika masuala ya roho, vivyo hivyo kila mtumishi anakipaumbele chake. Na ukivichunguza utagundua kuwa vipo vinavyolalia upande wa agano la kale, na vingine viko upande wa agano jipya,
Mfano
Afrika kuna vipaumbele kama wokovu na uchumi, msisitizo wa kenye wokovu uko kwenye uzima wa milele pamoja na afya ya mwili, pia kupata mafaniko ya kiuchumi.
Amerika na ulaya kuna vipaumbele kama kuabudu, hii ni kwa sababu wao hawana shida sana ya kiuchumi wala kiafya, hivyo kwa upande wa Mungu ni watu wenye kupenda kuabudu kuliko kuomba na kutaka msaada wa Mungu. Kusema hivi haimaanishi kuwa wao hawaombi, isipokuwa mkazo wao hauko kwenye mambo ya uchumi na afya.
Mashariki ya kati hasa Israel, kuna vipaumbele viwili, ufalme na ibada, huko ndiko kuna mambo ya kifalme pamoja na moyo wa ibada.
Uarabuni na asia, kuna vipaumbale vya wokovu na kuabudu.
Vipaumbele hivi vyote vina chanzo na sababu zake, mfano kwa upande wa Amerika na ulaya si mahali ambapo mtu anaweza kuwahubiria habari za kuwa na uchumi na afya kwa kuwa wamejaliwa katika hayo. Sawa na upande wa Israeli, habari za utawala kwake ni mhimu sana kuliko vyote kwa kuwa, wao ndio saa ya dunia, hivyo kila mabadiliko yanayotokea kwao yanaigusa dunia.

Kutokana na maelezo yote hayo juu ya uchumi ni wazi kuwa suala la uchumi lina misingi yake zaidi ya vile linavyotazamwa kwa baadhi yetu. Kwa kuwa hakuna mahali popote ambapo uchumi umehusianisha na shetani, bli uchumi huhusianishwa na dhambi. Hivyo katiuka kuomba juu ya uchumi ni mhimu kujua misingi iliyojengwa kabla imesimamia kwenye nini, sulemani aliomba hekima akapewa na utajiri. Kama hakuna hekima basi ni ngumu sana kuwa na utajiri. Kwa kuwa mataifa mengi yalipofanikiwa kiuchumi walimsahau Mungu kabisa, uchumi uliwalewesha wakaona kuwa ndio kila kitu.
Hivyo katika kuombea nchi yetu, ni mhimu tushugulike na dhambi pamoja na hekima ya utawala, hapo tunaweza kufanikiwa katika kunusuru hali ya nchi yetu kwa upande wa uchumi.

Katika suala la utawala, ni jambo mhimu sana katika selikali, nchi isipokuwa na viongozi wazuri ni hakika kuwa haiwezi kuendelea, kwa kuwa suala la maendeleo linagusa uongozi pamoja na mfumo ulioko. Kwa hali hii, tukitaka amani iwepo katika nchi, ni lazima tushugulike na uongozi pamoja na lango lake ambalo huwa kwenye mawazo na imani.
Suala la uongozi lina uhusiano mkubwa na suala la familia na marafiki, kwa kuwa kuna uongozi wa wito, na ule wa kujiita au kuitwa na marafiki, dini, au familia. Hata hivyo ni mhimu kujua kuwa suala la uongozi si Baraka bali ni mfumo na mtu aliyewekwa kuwa kiongozi.

Kwa mfano kiongozi wa kwanza wa Israeli katika habari ya wafalme alikuwa Sauli, katika utawala wake, kitu kinachoitwa utii hakuwa nacho, na mtu asiye na utii, ina maana hana hekima ya kutosha, na kama hana hekima ya kutosha, basi huyo lazima atakosea. Na kosa la kiongozi wan nchi ni pigo kwa nchi.
Nafasi ya uongozi ni mhimu sana katiaka nchi, kuliko kiongozi mwenyewe, kwa kuwa kiongozi ni mtu tu, lakini ile nafasi anayopewa inamfanya awe zaidi ya mtu. Hivyo jambo kuwa si kiongozi bali ni ile nafasi ya kiongozi na kitu ambacho imebeba. Hata hivyo ni mhimu kujua kuwa kiongozi hafanyi yaliyo yake, bali hufanya ya Yule aliyempa nafasi ya kukaa kwenye hiyo nafasi. Hakuna mtu awezaye kutimiza kiu na haja ya mioyo ya watanzania wanaokaribia milioni 47 kwa akili na hekima yake, bila msaada wa roho. Pia ni jambo bay asana kama hakuna maaono yoyote, tunaweza kulaumu mfumo uliopo kila siku lakini kama hakuna maono ya Mungu juu ya nchi basi, hakuna jambo tuwezalo kulifanya. Hivyo kwetu waombaji ni mhimu kuwa na maono ya juu ya nchi, kasha tusimamie hayo.

Hivyo katika yote yako mambo makuu matatu, moja ni maono, mbili ni nafasi yenyewe ya utawala kwa lugha nyingine tunaweza kusema kiti chenyewe, na tatu ni mtu mwenyewe yaani kiongozi mwenyewe.
Mfano mzuri unaogusa kiongozi mwenyewe na nafasi yake kwa watu wake ni huu wa mfalme Daudi
Ndipo moyo wake Daudi ukamchoma baada ya kuwahesabu hao watu. Naye Daudi akamwambia BWANA, nimekosa sana kwa haya niliyoyafanya; lakini sasa Ee BWANA, nakusihi uondoilee mbali uovu wa mtumishi wako; kwani nimefanya upumbavu kabisa. Na Daudi alipoondoka asubuhi, neon la BWANA likamjia nbii Gadi, mwonaji wake Daudi, kusema, Nenda, nenda ukanene na Daudi, BWANA asema hivi, nakuwekea mambo matatu; katika haya uchague moja, nikutendee hilo. Basi Gadi akamwendea Daudi, akamweleza, akamwambia, basi, miaka ya njaa ikujilie katika nchi yako? Au miezi mitatu ukimbie mbele ya adui zako, huku wakikufuatia? Au siku tatu iwe tauni katika nchi yako? Fanya shauli sasa, ufikiri ni jawabu gani nimrudishie aliyenituma. Naye Daudi akamwambia Gadi, nimeingia katika mashaka sana; basi sasa natuanguke katika mkono wa BWANA; kwa kuwa rehema zake ni nyingi; wala nisianguke katika  mkono ya wanadamu . basi BWANA akawaletea tauni tangu asubuhi hata wakati ulioamriwa; nao wakafa watu kutoka Dani mpaka beer-sheba sabini elfu Samweli 24:10-16”
ni hakika kuwa ukisoma maneno haya, unaweza usitamani nchi yetu kuwa kwenye nafasi hiyo mbele za Mungu, ukitazama yanayofanya na baadhi ya viongozi. Kwa kuwa kama kosa la kiongozi linaweza kusababisha uchungu wa msiba kiasi hicho, ina maana kwa uongozi wetu basi wat wangeisha. Ni bora kuwa hivi kuliko kuwa na nafasi kubwa mbele za Mungu, bila kushugulikia nafasi ya kiongozi na kiongozi mwenyewe.

WAJIBU WA SELIKALI KATIKA MAMBO YA KIJAMII MBELE ZA MUNGU
Huduma zote za jamii kama vile, hospitali, umeme, maji, shule, soko, n.k ni wajibu wa selikali, lakini hata hivyo mambo haya yameunganishwa na uchumi, kwa kuwa uchumi usipokuwa mzuri basi huduma hizi hazitatolewa vyema.Hivyo mambo makuu mawili yanalifanya hili liwe sawa.
WAJIBU WA KANISA JUU YA SELIKALI

UHUSIANO WA LANGO HILI LA KANISA NA NCHI PAMOJA NA TAIFA:
Kama ilivyoelezwa mwanzo kuwa lango la kanisa kuhusianishwa na nchi na taifa ni kuwa: mpango wa kwanza kabisa wa Mungu ilikuwa nchi na taifa vitawaliwe kwa sheria za mbinguni au za ulimwengu wa roho. Na wakati mwanadamu alipokuwa kwenye  bustani ya edeni namna iliyokuwa inamuongoza ilikuwa namna ya roho. Lakini ulipotokea uasi ulipindua ile namna ya roho iliyokuwa imewekwa kumuongoza mwanadamu na kuchukuliwa na namna ya mwili. Lengo la Mungu kuweka namna ya roho ni kwa kuwa vitu vya roho viko imara na ni vya uhakika, na kwa kuwa Mungu ni roho basi ilikuwa ni lazima mwanadamu aongozwe na namna ya roho na Mungu alikuwa amemfunika na namna ya roho inayotosha kuongoza dunia.

      Kwa kuwa dhambi ilitokea na kuvuruga mfumo huo, mwanadamu alikuwa anaishi kwa kuongozwa na namna ya dunia na wara siyo ya Mungu, isipokuwa kwa wachache waliopata neema ya kumuelekea Mungu aliwapa namna hiyo ya roho. Mfano Henoko.
Ilipofika wakati wa Ibrahimu Mungu alipoingia Agano na Ibrahimu baada ya kuona kuwa Ibrahimu atamuelekea Mungu. Baada ya miaka mia nne Mungu alianza kutekeleza Agano lake. Alimtumia Musa kutekeleza mambo ya agano lake na Ibrahimu, lakini wakati huo bado hata wana wa Israeli walikuwa wanatawaliwa na namna ilele ya mwili. Na kwa kuwa ili uishi na Mungu ni razima uongozwe na taratibu za Mungu ambazo ni za urimwengu wa roho, Mungu alimchukua Musa na kumueleza utaratibu mpya wa maisha yao wanayotakiwa kuishi na wara si kama zamani. Walipewa amri kumi na sheria ndogondogo zilizoikamilisha utaratibu wanaotakiwa kuishi, ikumbukwe sheria hizi zilikuwa zimetoka kwenye ulimwangu wa roho wa Mungu Baba Mwenyezi, kwa kuwa hakuna sheri itokayo kwa Mungu isiyo ya ulimwengu wa roho( Warumi 7:14). 

Hapo Mungu alitaka kuwatengenezea maisha aliyokuwa ameyakusudia tangu mwanzo kwenye bustani ya Edeni kabla ya uasi. Baadae wakati wa nabii samweli  Wana wa Isreli walikataa kuwa chini ya utawara wa Mungu badara yake wawe na mfalme atakayewaongoza, ambaye watakuwa wanamuona na kuenda naye vitani kama ilivyokuwa kwa mataifa mengine.
Mungu aliwakubalia na akafanya ule Mlango aliokuwa anautumia katika kuwaongoza akauweka juu ya namna hiyo ya utawara waliyoitaka ya kuwa na mfalme mwanadamu. Mlango huo ulikuwa kanisa, na uliwekwa kuwa kiongozi wa selikari ya mwili waliyoitaka, hivyo japo kuwa alikuwepo kiongozi wa mambo ya mwili, lakini bado Mungu aliweka kiongozi katika lango lile la kanisa kuwaongoza watu na mfalme wao (1 Cor 6:4). Na ni ukweli kuwa hukuna mfalme aliyewekwa katika Israeli na asipewe kiongozi yaani nabii wa kumuongoza, hata kama angekuwa imara kiasi gani lakini bado kwenye lango la kanisa kuna kiongozi aliyewekwa kuwaongoza wote. Hata wakati wa Daudi japo alionekana kuwa imara sana mbele za Mungu, lakini hiyo ilikuwa nafasi ya kifalme , kwenye nafasi ya kanisa manabii walikuwepo kama Mwongozo,(2Samweli 24:10-19)
      Maelezo hayo yanaonesha kuwa kusimama kwa nchi na taifa kunategemea pia namna kanisa lilivyosimama.
Kanisa ni mwangalizi na kiongozi wa selikali na watu wake, na tunaposema selikali na watu wake inamaanisha kuwa  kanisa linaiongoza selikali kufanya sawasawa na mapenzi ya Mungu ili Mungu asiadhibu nchi hiyo na taifa hilo.
Pia kanisa ndiyo kiongozi wa viogozi wa selikali, mwenye wajibu wa kuwafanya watimize mapenzi ya Mungu katika nchi na taifa kwenye lango hilo la uongozi katika mwili.(1 Cor 11:16).
Nabii Danieli aliyekuwa amewekwa kusimama kwenye lango la kanisa alipoona mambo hayako sawa aliingilia kati na kuomba maombi mazito ya kuepusha hasira ya Bwana isiipate nchi na taifa lake, (Danieli 9:3-19), pia Ezekieli alipewa kazi ya kufanya ili kufuta uovu wa nchi na taifa lake kwa kuwa yeye alikuwa kwenye lango la kanisa (Ezekieli 4:4-9).

Roho Mtakatifu akujaze zaidi ya ulichosoma na kujifunza

kwa msaada zaidi niandikie kwenye email: gkazili@yahoo.com, au tuma ujumbe no 0765-129960

Mwl. Goodluck Kazili



UTATU MTAKATIFU NA KUSUDI KWA MTU (MUNGU BABA, MUNGU MWANA, MUNGU ROHO MTAKATIFU)



UTATU MTAKATIFU NA KUSUDI KWA MTU
(MUNGU BABA, MUNGU MWANA, MUNGU ROHO MTAKATIFU)

DONDOO:
UTANGULIZI
SEHEMU YA KWANZA
Ø  NAFASI YA MUNGU BABA KATIKA DUNIA/MWANADAMU/MTU
Ø  NAFASI YA MUNGU MWANA KATIKA DUNIA/MWANADAMU/MTU
Ø  NAFASI YA ROHO MTAKATIFU KATIKA DUNIA/MWANADAMU/MTU
SEHEMU YA PILI
NYAKATIA TATU MHIMU
Ø  KUUMBWA ULIMWENGU
Ø  BAADA YA UUMBAJI AGANO JIPYA
Ø  UJIO WA KRISTO: AGANO JIPYA
SEHEMU YA TATU
UGAWAJI WA MADALAKA
Ø  KUTOKA KWA MUNGU HADI KWA YESU KRISTO
Ø  KUTOKA KWA YESU KRISTO HADI KWA ROHO MTAKATIFU
SEHEMU YA NNE
MAMLAKA NA UHUSIANO BAADA YA UGAWAJI MADALAKA
Ø  MAMLAKA YA MUNGU NA UHUSIANO WAKE NA MWANADAMU
Ø  MAMLAKA YA YESU NA UHUSIANO WAKE NA MWANADAUMU
Ø  MAMLKA YA ROHO MTAKATIFU NA UHUSIANO WAKE NA MWANADAMU
SEHEMU YA TANO
UMHIMU NA ULAZIMA WA KUJUA NA KUFUATA UTARATIBU HUU
Ø  KUSUDI LA MUNGU KWA MWANADAMU
Ø  UTILIMILIVU WA KUSUDI
Ø  HITIMISHO

SEHEMU YA NNE
MAMLAKA NA UHUSIANO BAADA YA UGAWAJI MADALAKA
Ni mhimu kufahamu kuwa utendaji kazi wa Mungu umebadilika sana kulingana na vipindi ambavyo vimepita. Hali hiyo inapelekea mfumo pia wa mwanadamu kutakiwa kubadilika katika uhusiano wake na Mungu. Kitu kilichowakwamisha wayahudi hadi leo wengi wao wasimwamini Kreisto ni kutokujua mabadiliko ya utendaji kazi wa Mungu na uhusiano wake na wanadamu. Japo maandiko yalikuwa yametangulia kueleza wazi kuwa kutakuwa na mabadiliko: Yeremia 31:3
Hakika Mungu ni mmoja lakini mwenye nafsi tatu za utendaji kazi, kusema mwenye nafsi tatu ni mhimu kuelewa kazi ya nafsi ni kupambanua na kufanya maamuzi. Hivyo kwa ufupi na tafsiri ya karibu tunaweza kusema kuwa Mungu anapambanua na kufanya maamuzi katika maeneo matatu au kwa namana tatu. Hivyo kwetu wanadamu husema yuko Mungu Baba, Mungu mwanaNeno, na Mugnu Roho Mtakatifu: kwa maana wako watatu washuhudia[mbinfuni, Baba, na Neno, na Roho Mtakatifu, na watatu hawa ni umoja. Kisha wako watatu washuhudiao duniani], Roho, na maji, na damu na watatu hawa hupatana kwa habari moja, (1Yohana 5:8-9a)
Hata hivyo ni mhimu kujua kuwa, utenfaji kazi huo, ambao umebadilika katika vipindi maalumu ambavyo vina maana kubwa kwetu.
Ukisoma kwenye maandiko matakatifu utakutana na wakati ambao Mungu alikasilishwa na akaamua kumupa mamlaka malaika ya kuwaongoza wana wa Israel; kutoka 32: 34: basi sasa uende ukawaongaze watu hawa mpaka mahali paloe ambapo nimekwambia habari zake; tazama Malaika wangu atakutangulia; pamoja na hayo siku nitakayowajilia nitawapatiliza kawa ajili ya dhambi yao.

Hata hivyo tuna wakati wa kujiuliza kwa nini Mungu hakuwapa Mwana  ndiye awaongoze; hakika yake ni kuwa muda wa Mungu kujifunua kupia Mwana ilikuwa bado, pia ni wazi kuwa nafasi ya taifa moja hakukuwa na ulazima wa kujifunua kupitia mwana wakati ulimwengu mzima ulikuwa na shida, hivyo kwao malaika alitosha, hata hivyo ukiendelea kusoma unaona kuwa Musa alikataa kwenda na malaika.
Na jambo hili ndilo ambalo limefanyika kwa wayahudi japo si kwa kukataa kwenda na Yesu ila kwa kutokujua kuwa utendaji kazi katika dunia hauko tena chini ya nafsi ya Mungu Baba bali Mungu mwana.
Ilipofika kipindi Fulani cha wakati kama unabii ulivyokuwa umeonyesha Mungu alihamisha mamlaka yake ya kuisimamia dunia na kuweka chini ya Nafsi yake iliyo mwana yaani nafsi ya pili ya utendaji kazi ambayo ni Mwana;  
Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa Tumepewa motto mwanamume na uweza wa kifalme utakuwa bagani mwake; naye ataitwa jina lake, Msahuri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani (Isaya 9:6). Pia kaitka Mathayo  1:21Naye atazaa mwana , nawe utamwita jina lake Yesu, maana ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao, Hayo yamekuwa ili litimie neon lililonenwa na Bwna kwa ujumbe wa nabii akisema, Tazama bikra atachukua mimba naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi.  


Ugawaji wa mamlaka hii ulikuwa na maana kubwa sana, hasa kwa ajili ya ukombozi wa mwanadamu, kwa maana ya kuwa Mungu aliamua aitoe nafsi yake ambayo ni mwana ili aifanye kuwa upatanisho kwa dhambi kati ya wanadamu na Mungu. Hii humaanisha kuwa Mungu hatamtazama mwanadamu tena moja kwa moja isipokuwa ataitazama nafsi yake/mwana kisha ndani yake atamuona mwanadamu. Na kwa kuwa katika nafsi hiyo ilitolewa damu ambayo huwasafisha dhambi zao, hivyo Mungu hataiona dhambi kwa kuwa watakuwa wametakaswa.
Haikutosha tu kuzaliwa kwa Yesu na kuwapa msingi wa namana ya kuishi maisha mpya yaani ya Kikristo, bali walitakiwa wakae nae ili kupata msaada zaidi wa kuendelea kuufahamisha ulimwengu hiyo namna mpya na ukombaozi ulioletwa na Mungu kwa wanadamu kupitia nafsi Yake. Na kwa kuwa kazi ya nafsi ya pili yaani mwana ilikuwa kutoa damu na maji kwa ajili ya ukombozi na utakaso wa dhambi, kazi ya kuendelea kushuhudia ukombozi hou haikuwa ndani ya nafsi mwana balili ilikuwa ndani ya uwezo wa nafsi Roho Mtakatifu; hivyo baada ya nafsi Mwana kumaliza kazi yake ilikuwa ni lazima nafsi nyingine ije kwa ajili ya ukamilisho.
Hapa huwa kuna changamoto kubwa kwa kuwa watu wengi wanaishia kwenye nafsi ya pili yaani mwana; wakijua kuwa baada ya kuokoka, kubatizwa na kutakaswa kwa damu ya Yesu hudhani kuwa mambo tayari, na wakati mwingine hufikri wanaweza kuyaishi hayo maisha ya utakatifu walioupata kupitia kwa mwana. Kumbe ni lazima kumalizia na hatu nyingine mhimu sana ya nafsi ya tatu yaani Roho Mtakatifu kwa kuwa huyo nidye kila kitu baada ya mtu kuokoka, kubatizwa na kutakaswa.
Maandiko yameweka wazi mambo haya japo watu hawayazingatii, na ndio maana wanakwama sana katika huduma zao, imani yao, na hata katika kutunza wokovu hou walioupata.
Ukisoma habari za Yesu ni baada tu ya kubatizwa alichukuliwa na Roho kwenda kujaribiwa nyikani. Kwa hali ya kawaida kulikuwa na haja gani ya Yesu kuchukuliwa na Roho Mtakatifu; (Math 4:1). Baada ya Yesu  kukaribia kuyondoka kwenda mbinguni aliwaambia wanafunzi/ mitume; Lakini mtapokea nguvu, akisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu;nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria na hata mwisho wa nchi, (matendo 1:8)
Hawa hawakuwa na sifa ya kuwa mashahidi wa Yesu kabla Roho mtakatifu hajawajilia, ni mhimu kujiuliza vema maana hawa wanafunzi walikuwa wamekaa na Yesu mda wa miaka mitatu na nusu akiwafundisha tena wakitembea naye na wakihubiri  na kufanya ishara na maajabu mengi, lakini bado kuondoka kwa Yesu walikuwa hawana sifa za kuwa mashahidi wake hadi Roho mtakatifu atakapowajilia. Ukijiuliza unagundua kuwa  kazi hiyo haikuwa ya Yesu/Mwana bali ilikuwa imewekwa ndani ya Roho Mtakatifu. 
Kwa uelewa zaidi kuna wakati wanafunzi wa Yesu hawakuwa wanapendezwa na taarifa za kuwa Yesu ataondoka, kisha Yesu akawaambia; Lakini mimi nawaambia iliyokweli; yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana mimi nisipoondoka, huyo msaidizi hatakuja kwenu, bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu,(Yohana 16:8). Hapa unaona kuwa kumbew Roho Mtakatifu yupo, lakini hajapewa hiyo kazi, na Yesu anasema nitampeleka kwenu halafu ukiendelea kusoma zinatajwa kazi atakazozifanya ambazo amepewa mamlaka haimaanishi ndizo kazi anazoziweza tu ila kwa duniani amekuja kufanya hizo; Naye akisha kuja huyo natauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na  hukumu, (Yh 16:9).

 Ukipendezwa na somo hili na unahitaji mwenelezo wake tuma email gkazili@yahoo.com au tuma ujumbe no ya simu 0752165609 au 0716050663.


Kunihusu

Picha yangu
"Wakati ule Yesu akajibu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga. Naam, baba , kwa kuwa ndivyo ilivyopendeza mbele zako. (Ni Siri Kuu)

Tafuta katika Blogu Hii