UAMUZI WA DHATI KUHUSU KUOMBA
Ili
uweze kuomba vema na kufanikiwa katika kuomba kwako, pamoja na mambo mengine ni
lazima uwe umefanya maamuzi ya kuomba. Maamuzi yanakuja kama matokeo ya sababu
ya kutaka kuomba. Si mara nyingi sana watu wanaingia kwenye kuomba wakiwa
wamefanya maamuzi, ni mara chache sana mtu anaweza kuingia kuomba akiwa
amefanya maamuzi ya kuomba.
Unaweza
kuwa na sababu za kuomba lakini usifanye maamuzi ya kuomba, hivyo ukaoma tu kwa
sababu inakubidi uombe, ngoja niombe lakini hujafanya maamuzi ya kuomba. Mara
nyingi hatuombi kwa sababu tumeamua kuomba, bali tunaomba kwa sababu
imetulazimu kuomba, na kwa kuwa hakuna njia nyingine, au pamoj na njia nyingine
ngoja pia niombe tu.
Kwa nini ni lazima kufanya maamuzi wa dhati
ndipo uombe
ü
Uamzi ndiyo siraha pekee ya mtu kuweza kuomba na
kufika mwisho, au kuweza kufaidi uombaji anao uomba
ü
Utaelewa thamani ya kuomba ikiwa tu umeomba kwa
maamuzi
ü
Utapata unachopata kwa uzuri halisi ikiwa
utaomba kwa maamuzi
ü
Utajifunza zaidi katika uombaji wako ikiwa
utaomba kwa maamuzi
Ukioba
bila kuamua kuomba,
§
hutaona thamani ya kuomba
§
hutapata kilicho katika kuomba
§
hutatambua nafasi yako katika kuomba
§
hutajua Mungu anahusikaje wakati unapoomba
§
hutajua unaathili upande wa adui kiasi gani ,na
§
hutakuwa na msimamo katika kuomba
Uamuzi wa kuomba
Ni
matokeo ya picha unayoiona ya jambo/mtu/kitu ambacho ni hitaji kwako. Picha
hiyo ni ya imani, inayokuelekeza umuhimu
na thamani ya kuomba, matokeo ya kuomba, maelekezo ya kuomba, nguvu na mamlaka
ya kuomba.
Uamuzi
wa kuomba unakuja baada ya kuona umuhimu na thamani ya kuomba, tena ni pale
unapokuwa umeona/unaona matokeo ya kuomba hupo utakapoomba, siyo imani ya
kuamini tu bali unaona katika ufahamu hayo matokeo, tena ni hapo yanapokuja
maelekezo ya kuomba, na katika hayo yote unahisi na kusikia nguvu ya kuomba na
kuwa na mamlaka ya kiuombaji kuhusu hilo hitaji.
Namna ya kufanya maamuzi ya kuomba unapotaka kuombea jambo/mtu
Mambo
haya 4 ni lazima uwe na uwezo wa
kuyafanya au kuyapata ndipo utakapofanya Maamuzi
Ø
Tafuta
kwanza ufahamu wa kiroho kuhusu jambo/eneo/mtu/kitu unachotaka kuombea
Danieli
alifanya maamuzi ya kuomba; maamuzi hayo yalitokana na ufahamu alioupata kuhusu
jambo analotaka kuomba, ufahamu ambao aliupata kwa kuvisoma vitabu
vilivyoandika habari za kiroho kuhusu Yerusalemu. hapa maandiko hunena “katika
mwaka wa kwanza wa kumiliki kwake, mimi Danieli, kwa kuvisoma vitabu,
nalifahamu miaka ambayo Neno la BWANA lilimjia Yeremia nabii, ya kuutimiza
ukiwa wa Yerusalemu, yaani miaka sabini, nikwamwelekezea Bwana Mungu uso wangu,
ili kutaka kwa maombi, na dua, pamoja na kufunga, na kuvaa nguo za magunia
na majivu. (Danieli 9:2-3)”
Ø
Kutambua
umuhimu na thamani ya kuomba
Maamuzi ya
dhati yanategemea thamani unayoiona katika jambo unalotaka kulifanya, thamani
hii inategemea msingi uliyonayo katika kuomba, na unaamini kuomba kwa asilimia
ngapi, na tafisiri ulizonazo na shuhuda kuhusu kuomba. Unaweza ukawa una
historia mbaya kuhusu mafanikio ya kiuombaji, yaani huna imani sana na
mafanikio yanayopatikana katika uombaji. Mtu anayejua uombaji ni nini na uwezo
wake huthamini sana kuomba na huona kuomba kuwa kitu cha thamani kwenye maisha
yake kuliko chochote kile. Jambo hili linawezekana tu kwa mtu ambaye
amefuatilia masuala ya kiuombaji, shuhuda mbalimbali kuhusu uombaji, ahadi za
kiuombaji katika Neno la Mungu, mafanikio ya watu walioomba katika maandiko.
Twafahamu
habari za Mwanamke Hanna, jinsi alivyofanya maamuzi ya kuomba, na kufanikiwa
vema kupata alichotaka. (1Samweli
1:10) ukiendelea unaona matokeo
ya kuomba kwake, na jinsi tena alivyozidi kuomba kama shukrani yake kwa Mungu. (sura
ya 2)
Elisha akaomba
kusema na Bwana kuhusu kumfumbua macho mjakazi wake ili aone ulinzi aliowawekea
Bwana dhidi ya maadui waliokuwa wamewazunguka (2 Wafalme 6:17) Twafahamu
habari ya Hezekia; “Basi Hezekia akajigeuza, akaelekeza uso wake ukutani, akamwomba BWANA,
akasema, Ee BWANA. Ikawa, Neno la BWANA likamjia Isaya, kusema, Enenda
ukamwambie Hezekia, BWANA, Mungu wa Daudi, baba yako, asema hivi, Mimi
nimeyasikia maombi yako, nimeyaona machozi yako; tazama nitaziongeza siku zako,
kiasi cha miaka kumi na mitano. (Isaya 38:2,4,5)”
Ø
Matokeo
unayoona wakati utakapokwisha kuomba
Hupaswi
kuona matoke ya kuomba baada ya kumaliza kuomba, bali matokeo huwa yanaonekana
kabla ya kuomba. “Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya
mambo yasiyoonekana. (Waebrania 11:1)”. Eliya alimwambia Ahabu kuwa
nvua inakuja kabla hajaomba, alipoenda kuomba ilimgharimu kuomba mara saba,
kama si maamuzi ya kuomba aliyokuwa ameyafanya ambayo yalitokana na kuona matokeo
ya kuomba kabla hajaomba, angeishia njiani kwenye kuomba kwake.
Kuona
matokeo ya kuomba hiyo ndiyo imani halisi. Maandiko hunena wazi kuwa “imani ni
kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana”. Ni
kusema kuwa, kuwa na uhakika, ni kuona kile kitu ambacho hakionekani bado kwa
macho ya nyama. Imani inakupa uhakika wa kitu kabla ya wewe kukipata, imani
inkuonyesha kitu ambacho hakionekani nje ya imani, ndiyo maana imani ni kwa
vitu visivyoonekana tu basi. “Akasema nitawaficha uso wangu, nitaona
mwisho wao utakuwaje; Maana, ni kizazi cha ukaidi mwingi, watoto wasio imani
ndani yao. (Kumb 32:17)”
Imani
si kuamini tu, bali ni kuona ambako ndiko kunakopaswa kukupe kuamini. Kuamini
ni ile inayokuja baada ya kuwa na uhakika, uhakika ambao umekuja baada ya kuona
ishara au hali au kitu au kidokezo kinachothibisha hilo jambo japo bado
halijadhilika au halijatimia au halionekani wazi. Imani ni ule uhakika anaokuwa
nao mtu ndani yake kuhusu jambo, hali, kitu, mtu n.k.
Kuwa
na imani ndogo au kubwa ni kiwango cha uhakika ulionao juu ya hilo jambo/kitu
katika kutenda kwake, kutimia kwake, kufanikiwa kwake n.k
Huo
uhakika, ili uwepo, ni hadi mtu awe na hati milki ya uwezo, nguvu, mamlaka,
neema na rehema ndani yake vilivyo vya Mungu. Ambavyo mara zote vinakuja
kutokana na kumjua Mungu. Imani chanzo chake ni kusikia kusikia ambako huja kwa
Neno la Kristo. Kusikia huko si tu kule kusikia Neno la Mungu, ni kusikia
ambako kumekuja kama neno lakini Neno la imani. Neno lenyewe ambalo ni imani
linaingia ndani yako ndipo unapokuwa na uhakika. Neno la Mungu ndiyo Kweli,
hivyo huwezi kuwa na uhakika yaani ukweli kama si Neno la jambo hilo.
“Lakini
pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima
aamini kwamba Yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao. (Waebrania
11:6)”
Kuwa
na imani kunahusisha mambo mengi, moja kubwa ni kumjua Mungu, ambako kunatiwa
nguvu na wema, maarifa, kiasi, saburi, utauwa, upendo. (2 Petro 1:5-7) - (9)
Ø
Maelekezo
ya kuomba
Maelekezo
ya kuomba yanakusukuma kufanya maamuzi, ambao unatokana na utayari unaoupata
kwa kuwa unamaelekezo ya kuomba.
Kuomba
ni safari, ambayo kuianza au kutoianza kunategemea uhakika wa safari (Imani),
kunategemea Maelekezo ya safari, tena kunategemea umuhimu wa safari.
Maelekezo
ya namna ya kuomba ni nyenzo muhimu katika kukusukuma kufanya maamuzi ya
kuomba. Maelekezo kuwa nayo au kutokuwa nayo kunategemea na kiwango cha neno
ulichonacho kuhusu jambo hilo, pia inatokana na kiwango cha uhitaji kinachoonekana
ndani yako, tena inategemea mazoea uliyonayo kuhusu kuomba, tena inategemea
kiwango cha imani uliyonayo katika Mungu, na zaidi sana inategemea uhusiano
ulio nao na Roho Mtakatifu. Kuwa na maelekezo ni sawa na kupata utaratibu wa
namna utakavyofanya kazi fulani, jambo hilo litakusukuma kuwa tayari kuifanya,
kadhalika maelekezo kuhusu kuomba yanakusukuma kufanya maamuzi maana unajua kwa
hakika unachotakiwa kufanya na mwisho wake utakuwa upi.
(Daniel
9:1-22)
Ø
Mamlaka, nguvu
na kibali cha kuombea jambo hilo
Kuwa
na kibali au mamlaka ya Mungu ndani yako inakusukuma kufanya maamzi ya kuombea
jambo. Kama ndani yako husikii kuwa na mamlaka, utaombea jambo bila kufanya
maamuzi, kwa sababu huwezi kufanya maamuzi kama ndani husikii kuwa na mamlaka
au kibali cha jambo hilo. Yesu alisema, ni nani atakaye kujenga mnara,
asiyeketi chini kwanza na kuhesabu gharama?, huwezi kufanya maamuzi ya
kuomba ikiwa hujisikii kuwa na uwezo wa
kuombea jambo hilo na kufika mwisho.
Hivyo
ili mtu uweze kufikia kufanya maamuzi katika kila hitaji unalotaka kuomba, ni
lazima ujitahidi kuwa na hayo mambo manne. Ni vema sana mtu ukiwa nayo ya
kudumu, si kwa ajili ya hitaji moja tu.
Msisitizo kuhusu maamuzi katika kuomba
Maamzi
ni msingi muhimu sana, katika kufanikisha kuomba kwako. Ni mara chache sana
kutokea kuomba ukiwa umefanya maamuzi kisha usifanikiwe katika kuomba kwako.
Kati ya msingi unaowakwamisha wengi katika kuomba kwao ni kuomba kabla/bila
kufanya maamzi ya kuomba. Huwezi kuona rahisi kuwa unaweza kuomba bila kufanya
maamuzi, na unaweza kujiuliza tuna maana gani kusema kuwa mtu anaweza kuomba
bila kufanya maamuzi. Lakini ni wazi na ni kweli na wengi wanaomba bila kufanya
maamzi, maana ukienda kwenye ibada ya maombi, kisha ukaambiwa tunataka tuombee
jambo furani, ukaomba kama Dakika 10, je! Utafuatilia kama lile jambo
uliloliombea kwenye kipindi limefanikiwa au bado?, ni adimu sana kutokea
kuuliza.
“Lakini
mwenye haki wangu ataishi kwa imani; naye akisita-sita, roho yangu haina furaha
naye.(Waebrania 10:38)”
Huwezi
kusema wakati unaomba ulifanya maamuzi, maana kama ungekuwa umeombea jambo
ulilolifanyia maamzi lazima kwenye kuomba kwako ungepata majibu hapo hapo, si
jibu lile la suruhu ya jambo lakini hata ile tu kujua kuwa ni nini kimefanyika na unategemea matokeo gani,
na hapo utayangoja ili uyaone kwa hakika.
Kuna
maombi machache sana kwenye maisha yako ambayo unaweza kuwa umeyaomba ukiwa
umeyafanyia maamuzi. Na utagundua kuwa karibu kila jambo uliloombea kwa kufanya
maamzi basi ulijibiwa/ulifanikiwa.
“kuomba
kwake mwenye haki, kwafaa sana akiomba kwa bidii” (Yakobo 5:16b)
Maamuzi
ya kuomba siyo yale ambayo mnafanya maamuzi kwa kusema tumeamua kuombea kitu
fulani. Bali ni ile ya maamuzi ya kuomba kwa hakika bila kuchoka wala kukata
tamamaa hadi upate unachotaka. Inakuja kutokana na uhakika wa njia hii ya
kuomba kuwa ndiyo pekee itakayokufikisha katika hali au jambo unalolihitaji.
Mfano
mtu anasema nimeamua niombee jambo hili kwa wiki mbili huku nikifunga ili jambo
hili liishe.
Mfano
halisi wa mtu aliyefanya maamuzi ya kuomba ni habakuki. Maandiko yanatueleza
hivi “
Mimi nitasimama katika zamu yangu, nitajiweka juu ya mnara, nitaangalia ili
nione atakaloniambia, na jinsi nitakavyojibu katika habari ya kulalamika
kwangu. (Habakuki 2:1)”
Kadhalika
Eliya, alifanya maamuzi ya kuomba, hapa maandiko hunena kwanza “Eliya
alikuwa mwanadamu mwenye tabia moja na sisi, akaomba kwa bidii mvua isinyeshe,
na nvua haikunyesha juu ya nchi muda wa miaka mitatu na miezi sita, akaomba
tena, mbingu zikatoa mvua, nayo nchi ikazaa matunda yake. (Yakobo 5:17-18)”
Eliya,
anatajwa kuwa ni mwanadamu mwenye sifa/tabia kama za kwetu, lakini katika uwepo
wa maamuzi aliomba na kufanikiwa. Kilichomfanikisha ni kitu gani ni maamuzi,
maana kama siyo maamuzi asingeomba kwa bidii. Na alipoomba mara ya kwanza na
hakupata mafanikio angekata tamaa na kuacha, lakini kwa kuwa alishafanyia
maamuzijambo analotaka kulifanya hivyo kuomba kwake haikuwa tu kuomba, bali
kuomba hadi apate anachoomba.
Hapo
juu tumesoma habari za Daniel, ambaye aliomba maombi yasiyokuwa ya kawaida na
akafanikiwa, lakini kama ukitazama kilichomsaidia utaona kuwa, ni maamuzi
aliyoyafanya ambayo yalikuwa yanatokana na ufahamu alioupata katika kuvisoma
vitabu.
Mwl. Goodluck Kazili (Ni Siri Kuu – The
Great Mystery)