SK-Siri Kuu
POWER OF VISION (NGUVU
YA MAONO)
Na Mwl; Goodluck Kazili
“Wakati ule
Yesu akajibu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na chi, kwa kuwa
mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga.
Naam, baba, kwa kuwa ndivyoilivyopendeza mbele zako. (Ni Siri Kuu)
Dondoo
muhimu za kujifunza kuhusu Maono (kwa ufupi)
Ø Tafsiri ya maono
Ø Maono kuhusu maisha
Ø Nvugu ya maono
Ø Namna ya kuwa na maono
Ø Funguo za maono
Ø Kiapo katika maono
Ø Mipango ya maono
Ø mwisho
TAFSIRI YA MAONO
Maono
ni picha ya mbele kuhusu jambo/ kitu/hali/ inayopigwa na kudhihilishwa kabla,
ili kutengeneza mazingra ya kufanikiwa kwake
Maono
yanaeleza jambo lisilokuwapo bado kwa wakati uliopo sasa lakini lipo mbele,
hivyo ile picha inayopigwa na kuletwa kwa mtu ili afanye jambo kwa ajili ya
kufanikiwa kwake.
Hata
hivyo maono yapo ya aina nyingi, lakini maana hiyo inagusa maono karibu ya
namna zote. Katika somo hili, maono yanayolengwa ni yale yanayohusu maisha ya
mtu.
MAONO KUHUSU MAISHA
Kila
mtu katika maisha ana viengele 4 vinavyogusa maisha yake, vitu hivyo ni Yeye
kuhusiana na Mungu, uchumi, afya na familia.
Hivyo,
mtu analazimika kuwa na maono yanayogusa mambo hayo manne . kwa ulazima huo,
binafsi ni lazima uwe na:-
1.
Maono ya
Kiutumishi (spritual Vision)
2.
Maono ya
kiuchumi (economical vision)
3.
Maono ya
kifamilia (family vision)
4.
Maono ya
kiafya (health vision)
Hata
hivyo, haiwezekani hayo yote kuwa maono halisi ndani yako kisha ukayafanikisha vema.
Unapaswa kuwa na maono makuu, ambayo huwa ni moja. Unakuwa na maono
ambayo ni makuu (main vision), kisha unakuwa una maono yaliyo chini ya maono
makuu (sub vision).
Mfano
mimi Goodluck Kazili maono yangu ni haya “Kumtumikia Mungu kwa kiwango cha juu
cha kwanza, katika yote, kwa vyote, sawa na mapenzi yake” (to serve the LORD
GOD to the best level of all, with all in His will). Kwangu haya ndiyo maono
makuu (main vision), lakini chini yake nina maono mbali mbali ya kiuchumi, ya
kiafya, na ya kifamilia. Mfano katika maono ya uchumi, nina picha (maono) ya
kuwa na shule pamoja na chuo, tena nina picha (maono) ya kuwa na miradi kadhaa
ya fedha, n.k.
Hivyo
ninachofanya ni lazima haya maono yawe chini ya maono makuu ambayo ni ya
kumtumikia Mungu. Hivyo, pamoja na kuwa nitamiliki chuo, shule, miradi, bado
itakuwa sehemu ya utumishi wangu kwa Mungu ili kuwa wa juu na wa kwanza kwa
vyote na katika vyote sawa na mapenzi yake Mungu.
NGUVU YA MAONO
Huwezi
kufanikiwa vema katika jambo lolote kubwa usipokuwa na maono nalo. Maono
yenyewe kama yalivyo ni nguvu, tena ni imani, tena ni ulinzi, tena kichocheo
(catalyst), ni Zaidi ya jitihada unazoweza kuzifanya katika jambo lolote. Maano
yanaelezea na yanalihakiki jambo kuanzia mwisho wake kuja mwanzo wake, hivyo
unaona unakoenda na jinsi unavyofanikiwa hata kabla hujafanikiwa wala kufikia.
Ni
muhimu kufahamu kuwa kazi ya akili ni kuutumia ubongo kutekeleza wazo au
adhimio lolote lililo ndani ya mtu liwe baya au jema. Akili inatengeneza mbinu
mbalimbali kwa kuutumia ubongo ili kufanikisha adhima yoyote ile iliyoadhimiwa
na mtu. Hivyo ukiwa na maono, yale maono mbali na kuhifadhiwa sehemu nyingine
kama moyoni, pia hukaa kwenye akili, hivyo akili wakati wote hutumia ubongo
kufanya namna mbali mbali ili kutekeleza hilo ambalo ndiyo maono.
Pia
kinyume chake ni kuwa kama hauna maono, unaifanya akili yako itekeleze kila
jambo linalokuja ndani yake karibu kila siku. Mfano mtu akikusema vibaya, kama
huna maono na kama hayana nguvu ndani yako, unaifanya akili yako kutwa nzima
ishinde inatafuta namna ya kufanya ili kutekeleza hilo la huyo aliyekusema.
Kama ni jambo ambalo akili itashindwa kupata suruhu, ina maana akili
haitaridhika na itapelekea kuliwaza kila wakati na kukwama katika mambo
mengine.
NAMNA YA KUWA NA MAONO
Huwezi
kuwa na maono nje yako, hata Mungu hawezi kukuletea maono nje yako,
ikimaanishwa kuwa ni lazima yawe maono ambayo kwa kweli ndiyo wewe, na ndivyo
ulivyo. Kuna maono ya kuletewa na kuna maono ya kutengeneza wewe mwenyewe, na
mara nyingi ukitengeneza maono wewe mwenyewe kwa namna ya kawaida utayaacha na
huwa yatabadilika.
Mbali
na yale ya kuletewa, wewe unaweza kuwa na maono ambayo yanazaliwa ndani yako.
Hilo si jambo la kufikri ila linazaliwa kama wewe ulivyozaliwa. Maana kila mtu
ndani yake kuna maono, ambayo mara mnyingi hayako wazi kwake, hivyo ni kazi ya
kuyatambua na kuyajua. Hii ni hatua ambayo mtu anaingia kwa makusudi na
kwa dhamili hatua hii ni hatua ya ufunuo, Kimungu yaani unafunuliwa kilichoko
ndani yako, hivyo unakitambua na kukielewa. (vision recognition and
understanding)
Ili
kutambua maono, ni lazima uwejifahamishe wewe mwenyewe kukuhusu, maana maono
yako ndiyo wewe mwenyewe. Hivyo ukishaweza kujijua vema ulivyo, undani wako
usiobadilika ambao ndiyo asili yenyewe hapo unaweza kutambua maono yaliyoko
ndani yako. Na kwa kuwa tumetofautiana uwezo wa utambuzi, unweza kuomba
usaidizi ili kutambua maono yako, ikiwa ni wewe mwenyewe kwa Mungu au mtu
kukusaidia.
FUNGUO ZA MAONO
Hapo
kwenye maono, kuna vitu ambavyo vinashika hayo maono ambavyo ni lazima
vijulikane na tena uwe navyo wakati wote ili viwe kwenye akili itumie ubongo
wakati wote kuvitekeleza.
Nitumie
mfano wangu:
Maono
yangu ni “kumtumikia Mungu, kwa kiwango cha juu, cha kwanza, katika vyote na
kwa vyote sawa na mapenzi yake” kwa kingereza “to serve the LORD GOD, to the
best level of all with all to His will”
Katika
maono haya, funguo zake ziko 5
1.
Kumtumika Mungu (serving Lord God)
2.
Kiwango cha juu na cha kwanza (best level)
3.
Katika yote (of all)
4.
Kwa vyote (with all)
5.
Mapenzi yake (His will)
Kwa
hiyo, huu unakuwa ndio msingi wangu wa maonowa vitu ninavyo paswa kuvitekeleza
wakti wote
KIAPO/ COMMITMENT
Ili
uweze kufanikiwa katika maono yako ni lazima uwe na kiapo juu yako mwenyewe.
Mfano mimi ili kufikia maono yangu kwa jinsi yalivyo na funguo zake, nimejiapia
kuwa “Goodluck Kazili katika kila jambo ni lazima nimtumikie Mungu, tena kwa
kiwango cha juu na cha kwanza, tena sawa na mapenzi yake”
Kama
unavyojua kiapo ni kitu ambacho kikishakuwa ndani yako, huna uhuru wa kuchagua
kutekeleza au kutokutekeleza. Hivyo kila wakati utajikuta unakumbuka ufanyapo
jambo na kuliangalia kama liko sawa na maono yako tena kama linaongeza jambo
kwenye maono yako
MPANGO MKAKATI (STRATEGIC PLAN)
Hii
ni mipango tofautitofauti inayohusu maono na inayopaswa kutekelezwa ambayo
kufanikiwa kwake ndio kufikiwa kwa maono. Hapa ndipo akili inapofanya kazi
zaidi kufikia maono ambayo yako ndani yako.
MWISHO
Wakati
wote kumbuka kuwa , kama huna maono utatumikia maono ya watu wenginge. Na
ukweli ni kuwa hukuzaliwa ili utumikie maono ya watu wengine, lakini kama huna
lazima utumikie tu, aidha kwa kujua au kwa kutokujua.
Pia
maono yanakua, hivyo upana wa maono yako kwa sasa au ya kipindi flani
hayatabaki na ukubwa au upana uleule. Maana kwa kadri wewe unavyokua ndivyo na
Yeneyewe yanavyokua.
Maono
makuu yanapaswa kuwa ya kumtumikia Mungu, na mengine yote kuwa madogo.
Mungu
wa mbinguni akujalie kuwa na maono yanayoujenga ufalme wake.
Mwl.
Goodluck kazili
Email:
gkazili@yahoo.com
Phone:
0765 129 960
Blog:
Kazili.blogspot.com